Mwasapile
JF-Expert Member
- Apr 20, 2020
- 214
- 448
Habari wana JF!
Ebu wadau naombeni ushauri wenu. Nina mke na watoto wawili. Mke wangu ana changamoto moja hataki kupika na pia hajali watoto. Yaani tunaweza kukaa siku mbili tatu tunakula mikate na chai tu. Na yeye ni mama wa nyumbani sio kwamba ana shughuli kivile za kumkwamisha yeye kupika HAPANA.
Nikimwambia kwanini hapiki anadai sijaenda sokoni kununua vitu (asa nawaza si yeye ni jukumu lake kwenda sokoni) maana pesa za biashara tunazofanya ni yeye anashika kwahiyo sio kwamba haendi kwasababu hana pesa.
Kuhusu watoto ndio kabisa hawalishi wala hawaogeshi, na watoto ni wadogo chini ya miaka 5. Yaani watoto wasipojipambania wenyewe kula ndio basi hawali.
Kuna saa nakasirika kinoma lakini nakosa namna. NIFANYEJE