Mke wangu hana bajeti na hajali, anataka tukipata pesa tutumie hadi ziishe

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Mimi na mke wangu tuna miaka minne sasa na tumebahatika kupata Watoto wawili, awali nilikuwa na maisha magumu sana, lakin kwa sasa ipo nafuu siyo kama mwanzo.

Changamoto ni kwamba mke wangu yeye yuko bize na pesa tu yaani ku-plan pesa ninayoipata tu-balance tufanye jambo la kutuinua kiuchumi yeye huo muda hana, hata kuweka chakula ndani hataki anataka pesa kila siku umuekee mezani.

Hana wazo la biashara, hata ukimpa wazo unataka kufanya kitu flani kwa ajili kuongeza kipato ataitika halafu ataishia hapo wakati mwingine hajali kabisa.
 
Screenshot_2026-01-29_233025.jpg
 
Dalili ya kuongozwa na mwanamke hiyo.
 
Hii ndio ile nilisema kua "Mke kujua kipato chako ni sawa na kuuza ramani ya vita kwa adui"

Mkeo alisha kusoma udhaifu wako toka mwanzo,hukusimama kama kiongozi wa familia,japo bado unayo nafasi ila inaonekana too late.
Seran
Ni sawa ni mwanamke aliyekosa hekima ndio anakuwa na hizi tabia! Oeni wanawake wa mithali 31🤝🏽
 
Pole sana ,zidisha upendo kwake uanze kumbadilisha taratibu kwa kumuelekeza sababu nahisi ameharibiwa na Background yake ,ikishindikana shika usukani wa bajeti ya nyumba yako mwenyewe kwa kila kitu ila ukisimama kama baba mwenye msimamo thabiti usioyumba yumba ila lililodhahiri ni kuwa si kila mwanamke au mwanamme anaweza biashara hivyo usimlazimishe kufanya kitu ambacho hakipo kwenye maumbile yake ,simama wewe kama wewe kuipeleka familia palipo pazuri .

Pole
 
Mimi na mke wangu tuna miaka minne sasa na tumebahatika kupata Watoto wawili, awali nilikuwa na maisha magumu sana, lakin kwa sasa ipo nafuu siyo kama mwanzo.

Changamoto ni kwamba mke wangu yeye yuko bize na pesa tu yaani ku-plan pesa ninayoipata tu-balance tufanye jambo la kutuinua kiuchumi yeye huo muda hana, hata kuweka chakula ndani hataki anataka pesa kila siku umuekee mezani.

Hana wazo la biashara, hata ukimpa wazo unataka kufanya kitu flani kwa ajili kuongeza kipato ataitika halafu ataishia hapo wakati mwingine hajali kabisa.
Kiumbe kama huyo ni wakumfukuza....hana malengo nawewe,
 
Hii ndio ile nilisema kua "Mke kujua kipato chako ni sawa na kuuza ramani ya vita kwa adui"

Mkeo alisha kusoma udhaifu wako toka mwanzo,hukusimama kama kiongozi wa familia,japo bado unayo nafasi ila inaonekana too late.
Seran
It will be just a matter of time. Mke smart anaweza jua income yako hata ufiche vipi. Issue siyo mkeo kujua kipato au fedha ulizonazo. Suala ni je mkeo ana busara? Mkeo kuwa kimeo ndo mzizi wa tatizo. Na kama unaogopa mkeo kujua kipato chako kiasi hicho basi mpe talaka tu.
 
Back
Top Bottom