Mzee Saliboko
JF-Expert Member
- Jan 29, 2018
- 1,311
- 1,018
Umuhimu wa kukaa na familia plus mmepoteza intimate connection
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daaaah! Kwanza nikwambie pole sanaa kwa hiyo changamoto unayoipitia ila kwanza angalia mzani wa mahusiano yenu je, yalikuwa hivyo toka mnafahamiana au tu ni mabadiriko katika safari yenu ya mahusiano? Pia angalia tofauti ya ukiwa mbali ama ukiwa karibu yake ,je kuna utafauti ukilichunguza hilo kwa umakini lazima jibu litakuwa sahihi💘💘 . Lakini kuhusu kujuwa familia imeamkaje, imeshindaje si jukumu la mama au baba pekee yake bali ni jukumu la familia kwa ujumla✍️✍️Aslaam,
Niko na mke takribani miaka 10 Sasa ya ndoa yetu.
Bahati mbaya mda mwingi hatulali na kuamka pamoja, kutokana na harakati za kutafuta maisha.
Huaga natumia siku 5 za wiki kwenda mahala pakazi yangu na siku 2 za mwisho wa wiki kushinda nyumbani na familia yangu, japo mara nyingine ikalazimu hata hizo siku za wiki naweza kuwa nyumbani.
Ila chakushangaza ni hii tabia ya mke kutonisalimia pale anapoamka au wakati flani wa siku.
Nisimpo mpgia mim kumtakia Hali yake na yawatoto ndo basi imeishia hiyo.
Nimejaribu kumuulizia mara nyingi kwanin hanijulii Hali mwenzie hasa pale ninapokuwa mbali na nyumbani?, jibu lake ni kwamba mwanaume ndiye mwenye wajibu wakusalimia familia yake.
Mwanamke na watoto haki yao nikupokea salamu na kujieleza kuhusu Hali zao zilivyo Kwa siku ile.
Nimejaribu mara nyingi kuamka na kukaa kimya bila kumpigia, aisee siku inakatika kabisa hanipigii.
Hili limenishangaza na linazidi kunishangaza kwakweli, yaan mim sina mtu wakunijulia Hali nimeamka naumwa au mzima ni juu yangu.
Kwa wale ambao wameoa au wanakaa na mke hili jambo nikwelii??
Huaga wajibu wakusalimia ni wa mwanaume tu? Hasa pale mnapokuwa mbali na familia zenu?