Hahaha nimecheka kama mazuri!
Kwanza nianze na disclaimer. Binafsi i love flaunting my man around, kwa sababu siwezi kutoka na mwanaume ambae i am not proud of.
Hisia zangu ni kuwa huyu dada hakuwa hivi mwanzo. Atakuwa alimpenda kwa dhati huyu mtoa mada lakini ikafika mahali akawa hayuko proud tena na mumewe. Na suspicion yangu ya kwanza ni kuwa mwanaume anafanya ujinga (labda wa kuwa na affairs) hadharani kiasi kwamba dada anaona aibu kuitwa mke wa fulani.
Mahusiano ni mtihani. Ila mtihani mkubwa ni mwenza kutokuwa proud na wewe. Kama huwezi kurekebisha hiyo kasoro iliyomfanya aanze kukukimbia, jiandae kisaikolojia manake anakupigia mahesabu ya kukuacha aisee. Kama hujui sababu muulize mdogo wake ama rafiki yake wa kike. Wanaume huwa hawaoni sababu za wazi kabisa. Niamini, mwanamke hawezi kukukimbia kwa sababu ya muonekano ila kwa sababu ya how you make her feel!