Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

Mke wangu hapendi kuongozana na mimi barabarani

Wadau heri ya mwaka mpya,

Wife amekuwa hapendi kuongozana nami katika safari mbali mbali misiba, sherehe, outing na kadhalika, sio kwamba anakataa moja kwa moja bali atatafuta sababu ili twende tofauti, na akikubali kwenda anakuwa uncomfortable na uwepo wangu.

Mwezi uliopita wa 12 tulisafiri wote kwenda up country nyumbani kwao mkoani kwa mapumziko ya end year, tulianzia mkoani kwetu, mwisho tukamalizia kwao, sasa tukiwa kwao, mdogo wake wa kike ndie alikuwa akizunguka nami mjini kutalii na kunionesha sehemu mbali mbali, wife alikuwa akinipiga chenga ndipo shemeji akaamua kunipa kampani.

Tuliijadili sana hii tabia ya dada yake ambayo hata yeye akasema ameiona kwa muda mrefu sana, anashindwa kuelewa tatizo ni nini? Sababu sina ulemavu, mwonekano wangu ni wa kawaida, wakiitwa ma handsome siwezi kutoka, lakini pia wakiitwa wabaya pia siwezi kutoka, ni wa kawaida.

Siku ya kuondoka Arusha, tukawa na ugomvi mkubwa sana kwamba nakosaje aibu kiasi kile, kuzunguka na mdogo wake hadi watu kunielewa vibaya, kiasi kuwa akakataa kabisa kwa hasira shemeji asije na sisi Dar maana huwa tunaishi nae, hadi wazazi wao walipomuamuru akakubali.

Tabia hii imenichosha sana kufikia hatua najiona sina thamani, tukienda harusini au outing ya pamoja na marafiki pamoja na waume zao utashangaa kila nikitaka kuchangia mada ananiminya mkono nisizungumze labda nitaongea jambo la kumuaibisha wakati mimi kwanza sio muongeaji, waume wa marafiki zake wataongea wee mimi nipo kimya, mimi nikichangia tu ni ugomvi, ananikosoa mbele yao kila nalochangia tena kwa kunishushua, hivyo nakaa kimya muda wote hadi wengine waulize mbona huongei.

Nilishajiuliza huenda huwa naongea pumba, hata hivyo hapana, mimi huwa ni mtu mwenye kuchagua maneno sana kabla ya kuongea.

Sasa naomba mnisaidie mawazo, tatizo ni nini hasa? Ni suala la muda mrefu hivyo nimeshachoka, nataka kufanya mabadiliko, nahitaji mke mwenye kunithamini na ambae yupo proud of me nahisi huyu hanipendi Ingawa tuna watoto wawili.

Nawasilisha kwenu
pole sana ila kwa asilimia 100 huyo mkeo hakupendi,yuko na wewe kwa sababu fulani ambazo anazijua yeye mwenyewe
 
1. Atakuwa amekuzidi level ya elimu au
2. Atakuwa amekuzidi kifedha au
3. Atakuwa anatibuliwa na marafiki zake kwamba ameolewa na mpolipoli au
4. Aliolewa na wewe akiwa na matarajio makubwa sana juu yako na yamekuwa tofauti.
5. Ni mbaguzi na anaku dharau sana (tena sana) kiasi cha kuona kinyaa kuonekana mbele ya watu akiwa na wewe.

Chukua hatua stahiki mapema.
 
Huyo mwanamke inawezekana anajiona ana class ya juu kuliko wewe kutokana na elimu yake aliyoipata baada ya kuoana na wewe, kupandishwa cheo au kuwa na kipato kukuzidi jambo lililomfanya aone amekosea kuwa na wewe ambae unapwaya kwa vigezo. Kingine ni kuwa, kuna uwezekano anakudharau kwa ujumla kutokana na kukuona huendani nae au yeye mwenyewe hajiamini na ana hofu ya kukosolewa kutokana na kuwa na wewe maana anatamani ungekuwa kama waume wa watu wengine anaowaona wana hadhi. Swala la kukukosoa unapoongea linaweza kuwa linatokana na yeye mwenyewe kutojiamini na kutokuwa na uwezo wa kuzungumza hadharani na hivyo anahofia kuwa wewe unaweza kuchemka katika kutoa hoja kama ambavyo yeye hawezi na kutokana na hilo, anakuwa anakuzuia kuepuka kuaibika kama ambavyo yeye anavyohofia kushindwa kuongea na kuaibika.
Huyo hajakomaa kiakili, mpe muda labda kama hiyo tabia itaanza kuextend mpaka katika kutoka na watu wengine.
 
Mkuu angalia sana personality yako na hygene ya mwili hasa mavazi na kunukia unapo kuwa na wife wako!

Sasa hadi leo umevaa pekosi suruali imeachia chini imebana juu na shati lako la mchelechele na viatu chachacha nani aongozane na wewe?Hata mm rafikio nitakukimbia tu

Piga JS suit ukipiga na Salvatore Ferragamo shoes nyoa vyema na piga perfume nzuri yy mwenyewe mke ataji feel proud kuongozana na wewe!

Achana na makubazi mkuu ukiwa na wife ehehehe
MKUU mbona amesema mdogo wake yuko peace naye na wanaongozana kila kona mpaka themeji kapata miwivu?! muwe mnasoma na kuelewa mada gwakukaja.
 
MKUU mbona amesema mdogo wake yuko peace naye na wanaongozana kila kona mpaka themeji kapata miwivu?! muwe mnasoma na kuelewa mada gwakukaja.
Mwaisa mdogo wake sio MKE wake!Wife hataki kuongozana na jamaa
 
Mwaisa mdogo wake sio MKE wake!Wife hataki kuongozana na jamaa
nahisi huyu ndugu yetu hana hata mkoko.safari zao ni za mguu na daladala.ushauri wangu atafute hela heshima itarudi! kapendwa Mengi na uzee ule sembuse ndugu yetu hapa hata wajukuu hana.Mwaisa jamaa hapa hana kisu kikali ndio shida.ulofa ni.gharama.
 
Kuna mambo magumu sana kuyafanya kwenye jamii za kiafrika. Hivi unaweza kusema namuacha mke wangu kwa sababu hafuatani na mimi? Wakati anapika, anaangalia nyumba, anaangalia wanao, na akienda kijijini na wewe anakaa nyumbani akipika na kusimamia mambo mengine na anakataa kuenda kubarizi na wewe mitaani?

Mtoa mada anapaswa kuongea na mkewe na kufanyia kazi majibu. Sio kuleta ubabe wa kiume. Mapenzi hayashikiliwi na plasta.
Hahaha umeikomalia hii mada, ila Inaumiza sana kutokukubalika na mwenzi wako.
 
nahisi huyu ndugu yetu hana hata mkoko.safari zao ni za mguu na daladala.ushauri wangu atafute hela heshima itarudi! kapendwa Mengi na uzee ule sembuse ndugu yetu hapa hata wajukuu hana.Mwaisa jamaa hapa hana kisu kikali ndio shida.ulofa ni.gharama.
Yaa kikolo msela wetu hana kitu na dizaini wife ni sista duuh
 
IN A VERY VERY NICE AND LOVING WAY

LIKE DARLING WANGU UNANIPENDA LAZMA AKUBALI AND Y HUPENDI KUONGOZANA NA MIMI AND BLA BLA KAMA KUNA MAHALI NAWEZA KUSEMA JAMBI KIURAHISI NI WAKATI NAPANDA KILIMA WALAH HATA KAMA NI UCHAWI NTASEMA

Wewe bidada unatutamanisha
 
Levels.....?
Au size? Hata sina jibu la moja kwa moja! Mkeo kimeo kama alikuwa hajakuridhia kwa nini alkkubali kusimama kwa mchungaji na kuapa mpaka kifo kiwatenganishe?
 
Anza kujipenda wewe kwanza!halafu una bahati ya kupewa uhuru kwelikweli,wengine wametaitiwa vibaya!
 
Pole sana mkuu,kwanza nikuhakikishie wanawake/wanaume wa aina hii wapo tena wengi usione wachangiaji wanajikakamua hapa inawezekana wanasubiri ili nao watatue tatizo kama lako,niliwahi kua na uhusiano na binti wa kihehe ambae kwa kweli alinipenda na nilimpenda ila alikua na tatizo kama la mkeo yaani tukiwa nyumbani mahaba motomoto ila tukitoka anakua uncomfortable kabisa ilinichukua muda kumuelewa ila nilifuatilia maisha yake ya nyuma alikua ana matatizo mengi sana ya kisaikolojia.
Lakini pia mkuu wa aina ya mkeo wapo wengi ambao wanajisikia wazito kufuatana na wenza wao na wapo ambao wanafuatana tu na wenza wao kwa kua hakuna namna wanaficha hisia zao,inawezekana hata hawa wake zetu wanakenua tukiwa nao matembezini kumbe nao wana ugonjwa kama wa mkeo,muhimu kaa nae chini mjadili kwa kina kujua tatizo ni nini simply siamini kua una muonekano mbaya,unaonge ovyo maana matatizo yangekua hayo naamini wanawake wako fast kuongea kwa matatizo kama hayo.
Nikutakie heri kaka katika ndoa yako Mungu akufanyie wepesi na ili liishe mapema maana ndoa ina changamoto nyingi.
 
Jifanye huna habar nae hata kuongea ongea nae pale inapobid tu..ukipta mwaliko we mpe taarifa tu kuwa unatoka na hakikisha hudikiliz jibu lake...ukiona hkuna mabadiliko kwa juhud zte hizo.. ujue hlo ni jipu linahtaji kutumbuliwa.. !
 
Back
Top Bottom