Mke wangu huwa ananiwekea chakula kidogo kwenye sahani sishibi, kumuambia naona aibu

Familia yako ina watu wangapi? Na unatoaga sh ngapi kwa siku?
 

Yaani hata kumwambia mke wako akuongezee chakula (hujashiba) unataka tukushauri?
Wewe ni mwanamme wa namna gani? naona umeoa ukiwa mtoto
 
Yaan mke ni wa kwako,anaishi kwako,anatumia pesa zako,chakula wanachokula ni nguvu zako bado unaogopa kumwambia akuongezee chakula!???
Usitutie aibu wanaume wenzio.
 
mkuu unategemea upate msaada huku JF ? huyo ni mkeo mwambie
 
Sa utashibia hapa jf?! Na je kwichikwichi usipotosheka unaogopa kuongeza mzunguko😉😉😉😉 Wacha ujinga aloo
 
Pengine amekuona unakula sana akaona kiafya atakupoteza, anakupenda sana huyo mke, anafahamu purpose kwamba maisha sio kula tu. Acha kula hovyo hovyo, wewe ungeoa mke mwenye tabia kama za mke wangu ungekuwa umeshakufa kitambo kwa uzito kutokana na kula chakula kingi. Mke ukirudi nyumbani ukimwambia nimechelewa na nimeshakula hakuelewi anakujazia chakula na ukila kidogo anaona umemdharau, mpaka alivyokuja kunielewa ndoa ilikuwa hatarini kuvunjika. Acha kula hovyo ili ujenge mwili wenye afya iliyobora kuliko kujenga minyama.
 
Mshukuru huyo mtu wa maana sana kwako, alishajua matatizo ya kula sana ndio maana anakupimia kidogo ili usiwe bonge nyanya. Unatakiwa umuelewe, bila shaka utakuwa mnene sana.
 
KAMA HAULETI CHAKULA HUWEZI KUWA NA UJASIRI WA KUMWAMBIA ILA KAMA WEWE NDIO MLETAJI UNAMWAMBIA TU "MKE WANGU NIONGEZEE"
 
Vipi mkuu bado mke wako anakuwekea chakula kidogo au amebadilika.
 
We nae eti unajiita mwanaume, unamuogopa mkeo, na hela wewe ndo unatoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…