Mke wangu kaacha ndoa yake kisa kazi

Naona hii issue umeiangalia upande mmoja tu,

Ni kweli jamaa anaweza akawa amekosea ila mambo anayoyafanya mkewe pia yana tia wasiwasi,

Kitendo cha kuwasiliana na mume wa rafiki yake bila huyo rafiki yake kujua unaona kua ni sawa? Hapo ilitakiwa kabla ya kuwasiliana na huyo mume wa mtu,angeunganishwa na huyo rafiki yake ambaye ndiye mke wa huyo jamaa anaye wasiliana nae,

Vipi kuhusu kitendo cha huyo mkewe kumuachia jamaa mtoto mdogo ni sawa?
 
Hiii simulizi nina wasiwasi nayo.. Kwanini neno ''MKE'' limeandikwa kwa herufi kubwa kwenye andiko lote?
 
Nina wazo la kuoa hivi karibuni wewe Tena unayaleta haya

Anyway pole sana
Wewe owa tu mkuu ila mchunguze huyo Mwanamke kuanzia familia yake na sio kumuangalia tu huyo mwanamke peke yake,

Huwezi kuacha kumiliki Gari kisa magari hupata ajali,tafuta mke sahihi anaye jitambua.
 

Hapo inaonyesha alikuwa hawezi labda hata kuchangia au kuwekeza kila mara hana pesa. Walimshauri vizuri

sasa nikawa najiuliza kama anafanya maamuzi ya kutafuta kazi bila kumshirikisha Mme wake hii inakuwaje???

Baada ya Muda wakati anaendelea kutafuta niliamua nimuache kwa kumchora nione Mwisho wake...
Nikaanza uchunguzi taratibu

Ulikuwa hautaki mke wako afanye kazi, na pia haukumpa mahitaji yake akae kwa Amani akiwa Mama wa nyumbani. Wewe unaonekana ndio umembadili mke wako. Ubaili wako kwake, wivu, na kutotaka kabisa has iwe na income yake.

Jirani akaambiwa nae akaona mwanya kumsaidia na mmmh.

Ulitaka mke akae nawe kama housewife, hakikisha unaweza kumtunza na kikubwa kuwa na urafiki na mawasiliano mazuri. Ulivuruga ndoa yako kipekee

Sali ili arudi na ubadilike akija, mtoto mlee Mola akuwezeshe.
 
Mda mwingine hao watu ni virusi lakin ukiwatibu wanajijua na kujielewa. Sikushauri uoe bado ni yale yale. Peleka mtoto nyumbani na uhakikishe kama utamuacha kwa mamako umwajiri msaidizi utafute pesa kwa hali na mali. Wanawake na pesa ni mandugu. Mwanamke kuacha mtoto ni kipengele hapo kuna lililopikwa kitambo na kama kungekua na amani hapo jirani angekushirikisha kuwa ndugu mke wako anaomba nimsaidie hili lakin wakapga kimya so tafuta hela umtunze mtoto wako ndugu yangu hata kama kuna uwezekano punguza matumizi yako mfano kama unaish nyumba nzima tafta ndogo ya kutaftia maisha au kama upo kwako pangisha vyumba hyo hela itunze mtoto na afu na wewe labda mke wako alitaka kupata kazi msaidiane lakin akaitafuta kwa njia isiyo.
 
Kiufupi huyo mwanamke ni either malaya au mtu ambaye hapendi kukaa tu bila kazi so ameshindwa kuvumilia ahadi zako ambazo hazitekelezeki kwa wakati na yeye hataki kuwa kama beki 3 na bado unamzuia kuongea na majirani inamaan hutaki wabadilishane mawazo ilhali yupo tu nyumbani
 
Yawezekana,,, maana hata tendo la ndoa,,, nilikuwa napewa kwa kulazimisha,,,,wakati mwingine anahama kitandani analala chini....ili nisimuombe tendo
Mmmh!Mi mke wangu hua anasingizia kwamba hajisikii manake hana hisia kabisa na tendo lenyewe hapa ndo nazidi kukusanya ushahidi kwamba inawezekana sio kipandikizi alichoweka bali kuna njemba
 
Mmmh!Mi mke wangu hua anasingizia kwamba hajisikii manake hana hisia kabisa na tendo lenyewe hapa ndo nazidi kukusanya ushahidi kwamba inawezekana sio kipandikizi alichoweka bali kuna njemba
Ndicho kinachokuumiza toa hiyo mentality
 
Hiyo comment yako ukiisoma tena kwa utulivu utagundua kua umekosea,ni sawa mke alikua na nia njema kutafta kazi ila njia aliyotumia sio sahihi na kwanini kakimbia mwenyewe hapo unagundua kwamba tayari kashaliwa na uyo mme wa rafiki yake so hataki ijulikane so hata biblia imesema mke akizini mwache.
 
Sijajua sana kama wanandoa ni lazima kuwasiliana nao wote kwa pamoja kwenye vitu vidogo kama mnatafuta kuuziana mali ya familia. Sisi kwetu naweza saidiwa na mke wa baba yangu mdogo, na mumewe asijue. Au nikamsaidia binamu yangu fedha, na mumewe asijue.

Huyo mume alipotafutwa alisema Nia yake ya kumtafutia kazi, hakuficha kuonyesha uovu na wala hakumuhusisha mkewe maybe ni mtu wa kusaidia tu bila kutaka sifa wala kuona kama ni jambo kubwa kafanya. Mwishowe wanawake hawa unamfanya jirani asimangwe na mkeo kisa umewasaidia. Na huyo jirani unaweza kuta kaambiwa na mke wa jirani yake kuwa mumewe anajua hilo ombi la kazi.

Yote hayo yanatoka palepale mwanzoni, miaka mitano bila kazi bila mtaji na super HB mwenyewe hajafanikisha hilo suala dogo kabisa.

Suala la kuacha mtoto ni kosa. Ila suala la kutafuta kazi sio kosa hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…