.
Wakuu nilikuwa naishi na huyu mke wangu, ilikuwa imetimia miaka 4 tayari, kwao walikuwa wananijua na kwetu wanamjua vizuri, alivyo maliza kulea mtoto mwaka juzi tukashauriana ajifunze masuala ya saluni Ili badaye nije nimfungulie duka la vipodozi na saluni hapo hapo Kwa maana Mimi ni fundi gereji.
Mwezi wa 12 mwaka Jana alimaliza kujifunza masuala ya saluni akawa ameshajua Kila kitu, tukashauriana mwezi wa tatu mwaka huu aende Kwa dada yake sumbawanga Ili anunue mahindi Ili tuje tuyauze mwezi wa 11 mwaka huu Ili tufungue Biashara yetu ya saluni na duka, nilimpa milioni mbili na laki 6, na gunia Moja kule ilikuwa ni elfu 25 kipindi kile hivyo nikajua tutanunua gunia nyingi halafu tukija kuuza hata Kwa elfu 70 tutapata Hela nyingi.
Alivyo fika kule tuliwasiliana kama wiki Moja tu wiki ya pili akawa hapatikani, nikawa nampigia dada yake akawa ananiambia eti mke wangu kaenda kijiji Cha mbali kununua mahindi na kule mtandao haupo, hali iliendelea hivyo hivyo ikafikia hatua dada mtu akawa hapokei simu zangu na mwisho wa siku naye akawa hapatikani.
Hali ilivyo endelea hivyo ikabidi nimtafute kaka yake, kaka yake naye akamtafuta mama Yao akamueleza, kaka yake ndo akaja kunipa taarifa eti mke wangu aliolewa mbeya na nilimpa talaka na nilikuwa nampiga sana Kwa kumtuhumu yule mtoto siyo wangu, nilichoka sana dada yangu, Mimi yule mwanamke sijawahi hata kumgusa hata Kwa Kofi la bahati mbaya na yule mtoto nilikuwa na uhakika asilimia mia ni wangu,na kibaya zaidi aliwaambia mtoto yule siyo wakwangu eti kaona Bora mtoto akalelewe na baba yake,
Mpaka muda huu hakuna hata ndugu yangu anaye jua Hali hii ninayo pitia Kwa Sasa na naona hata aibu kumweleza mtu, bado nahisi ni ndoto mpaka muda huu japo imepita miezi mitano.