Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

Mke wangu kalipendea nini hili jitu?

😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
Ila mie naye sijui nikoje tu, yaani badala ya nikupe ushauri nimejikuta cheko zimenibana sijui kwanini, hahahahahahahahahah
 
..MKUU POLE SANA, JIKAZE KISABUNI. MI NACHOONA HAPO BINAMU KESHAFANYA YAKE, NA USIPOANGALIA ATAKAA HATA MWAKA
 
Nasubiri mrejesho hapa jamvini. Lakini wanawake mna mateso kiaina sasa kweli uko busy na lijitu wakati mwenzi wako kimbaumbau si ni kumuharibu kisaikolojia.
Bora kimbaumbau kuliko kitambi asee
Mkuu ujue mume mtu ni kitambi meneja tofauti na Lijitu

Cc Smart911
 
[emoji1] kwanini bora kimbaumbau...
Hahahaah niliexpect this question..

Unaeza kuta kimbaumbau ila ana msuliii tofauti na manyamanyama

Though Inategemea na kaziii a.k.a muziikiii wa muhusika regardless kitambi ama mbau mbau

Cc Smart911
 
Teh Wee prince wewe kwahiyo Lijitu ni la mkoani sio??
Linakula linashiba haswa??
Halina muda wa kujipodoa sio?? Ama Sijakuelewa!!???[emoji15] [emoji15]

Cc Smart911
Mikoani ndo kunaongoza kutoa aina ya lijitu kama ilo analolilalamikia jamaa hapo[emoji1] [emoji1]
 
Mhhhhhhhh ningekuwa mimi namfukuza tu maana ni nyumbani kwangu mfukuze au kama unahera kiasi furani kinachoweza kuwasafilisha kwenda sehemu yoyote ambayo mnaweza kupanga chumba hata siku tatu mnamuambia tu kwamba sisi tunasafiri kama linawafuata fanya lolote lile mmtoloke mfunge ndani


Yan wew nae walewale ... Ukimbie nyumba yako ukaishi ka mkimbizi kwenye nyumba za kupanga kisa mtu mmoja.... Akina James Delicious ni wadogo zako nn...
 
kumbe una kitambi mimi ngoja nipite tu maana utakuwa mwanaume wa dar
 
Pole sana aisee, kuna mijitu inaboa.
Leo liite liulize linaondoka lini? Uliambie unalipa siku tatu liwe limemaliza shughuli zake lirudi lilikotoka.
Mzaha mzaha....
 
Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.

Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?

Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?

Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?

Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?

Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.

Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.

Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?

Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
Sasa mgeni kaja lakini ww unajifanya bosi... Hutaki kuwa karibu nae.. Unaenda bonanza kwanini usiende nae.???hapo kusema lijitu nitayari unaonyesha unatabia zakibinafsi nakujisikia kujiona ww mbora kuliko wengine... Ndugu yako unamwita lijitu... Usikute jamaa hata hana Habari nahayo mambo na anawaheshim watu wote humo ndani... Kuvaa Box sijui kufua wengine huwa wanachukulia Lawanda kabisa.. Kuna rafiki yangu huwa naenda nyumbani kwake kumona Mamake akija kutoka mkoa namkuta kakaa namamake mzazi mshikaji akiwa na Box pekeyake... Lakini mm siwezi kabisa ..so binadam tunatofautina. Acha kumchukia ndugu yako..
 
Back
Top Bottom