Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Mtafaruku ni Mkubwa. Huu mwaka naona unaisha vibaya Mno. Kama sitakuwa macho nyumba yangu inaweza kuvunjika.
Sorry nianze kwa Salamu maana Leo mtanifaa Sana kwa ushauri Bora.
Assalam alyekum kwa Waislam,
Tumsifu Yesu Kristo kwa Waislam.
Wapagani, salama!!
Nimeoa Miaka tisa iliyopita. Nimejaliwa watoto wawili sasa.
Juzi familia yangu ilipata mualiko kwenda kwenye sherehe ya harusi ambayo ukumbi ulikuwa kwenye Moja ya visiwa vilivyoko bahari ya Hindi karibu na Jiji la Dar.
Basi huko mambo yalienda vizuri kwa upande wangu lakini nilishangaa kuona mke wangu Akiwa Hana furaha.
Sikumzingatia Sana ili asijeiharibu furaha yangu nikiwa nimepanga kumuuliza tukiwa tumerudi nyumbani.
Kufika nyumba, mwanamke amevuta mdomo kama kang'atwa na Nyigu. Kulikoni Mke wangu. Ndipo akaanza kushusha risala ndefu yenye shutuma, lawama na kejeli.
Nilinangwa!
Nilikaangwa!
Oooh! Miaka yote tisa tunapanda Daladala Mpaka tumekariri vituo kama Makonda wa Daladala.
Miaka tisa yote nimevumilia.
Watoto wadogo kina Chief Godlove wamezuka huko wanakupiga bao kama mjingamjinga.
Nikasema kimoyomoyo. toba! Nimekuwa mjinga tena.
Hivi gari la Milioni Saba tuu hata kama ni used umekosa?
Hata kama ni mkwechemkweche gari ni gari.
Alafu unajiita Taikon, taikon gani.
Nitakupeleka kwa Kina Mwamposa wakupe Upako wa Gari.
Nikasema mmmh! Yamefikia huko.
Akaendelea;
Mimi kukupenda usichukulie kama udhaifu wa KUFIKIRI sipendi maisha mazuri. Nataka maisha mazuri Mimi. Nimechoka Baby T kukimbizana na Daladala.
Mambo ya kunukishana mijasho na kubambiwa sitaki.
"Eeeh! Aaa mke wangu Maneno gani tena hayo" nikasema.
Wewe unafikiri mbanano ule wa Daladala nitaachwa kubambiwa na kunukishwa mijasho?
Nikasema, aaaah!
Akaendelea;
Wewe si bingwa wa kuandika mamakala mrefu huko Mitandaoni ambayo hayakuingizii chochote. Alafu unanikeraga Sana.
Sasa niandikie kurasa ishirini za sababu zilizokufanya ushindwe Kununua gari tangu unioe huu mwaka wa Tisa.
Ziwe sababu zilizoshiba.
Akaenda bafuni akiniacha nimetekewa. Alaaah!
Sasa Mimi nitaandika nini jamani!
Yaani hapa kichwa kimefura sijui niandike nini.
Pointi haziji.
Naombeni ushauri. Wenye matusi Leo sitayajibu. Siwezi jibu matusi wakati ndoa yangu IPO taabani .
Leo sipumziki.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam