Ndugu zanguni habari zenu, nimekuja kwa ushauri wenu pamoja nakuweza kupanua mawozo yangu nakupunguza stress za kifamilia.
Mimi nina mke na tumejaliwa watoto wawili (2) wakike na wakiume, Mwaka jana mnamo mwezi wa saba (7) mke wangu alinipa taarifa kwamba Mama wake mzazi (mama mkwe) anakuja mjini nijiadae kwenda kumpokea hiyo siku ikifika na ni sisafiri paka nimpokee, kwasababu shughuri zangu nasafiri za nje ya mkoa, nikamuliza amekuja kufanya nini? Eti kufuatilia mafao yake ya pensheni, mmh wakati alisha pokea tangu mwezi wa pili, niliguna tu nikamjibu sawa ntampokea, baada ya kama siku tatu aliniambia amepanda basi, siku hiyo nikaendesha ki 'babyseater' (gari) changu nikaenda standi ya ma basi ya mikoa kumpokea, alingia kama saa sita usiku nikampokea nikaweka mizigo yake ndani ya gari tukaelekea nyumbani vizuri bila kunotisi kitu chocolate.
Baada kama ya siku mbili mie nikasafiri kuenda kwenye kazi zangu, nilirudi baada ya siku tatu (3) nikamukuta bado yupo si ku mind walaa, sisi kiutamaduni na kimila mama mkwe ni mwiko kwangu kuingia chumbani mwake au kumshika mkononi au kutumia choo kimoja kwahiyo nilikuwa namsalimia nikiwa sembuleni kila asubuhi na jioni hiyo wiki nilio kaa sikumtizama sanaa isipokuwa ucku wakati namleta aliendelea kukaa nyumbani kwa takrbani miezi mitatu, mie naenda safari zangu na rudi kila wiki kwa kufichwa na mke wangu.
Inaendelea itakua na sehemu mbili ili nisiwachoshe