Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sina apatite yake kitandani tu..... uongo wake sana ni kuhusu kwao na vizinga vya pesa visio uelewaka......mfano mgine habari nilio pata pale jilani kwenye wachimba kaburi kumbe baba yake mzazi walikua ametengana na mama ake kama miaka mitatu nyuma, na baba aka oa mke mgine mie sina habari yoyote, watu wananiuliza mama mkwe mgine unamjua hata na shinda kuwajibu aibu kweli kweli
Tulia ndugu yangu acha hasira. Uongo ni mbaya na mkeo amefanya kosa kubwa sana. Kwenye ndoa kuna changamoto nyingi sana na changamoto yako si kubwa sana kama wanazopitia wengine.Ahsante mkuu, lakini namimi natamani hili jambo liishe haraka iwezekanavyo, ila kulala nae kitanda kimoja naona kama imekua ngumu kwangu, yule mama muongo sana kupitiliza, kaniona mimi boya sana mtaa mzima ulijua kwamba huyu mama anaumwa isipokua mimi tu........
Mkuu ni ushauri mzuri ila mke wangu ni aina ya wanawake wakukataa kata kata, paka mwisho neno sorry ni zito kwake kulitamka, kumhoji anaweza kubadili mada yakazaa mengine.
Mkeo amefanya makosa sana kutokukwambia yote hayo , lakini kabla ya kumlaumu kwa makosa hayo hebu jitathmini na wewe kwanza , inawezekana upo strict na serious sana kiasi kwamba mtu kukwambia Jambo anajishauri Mara mbili mbili,Ndugu zanguni habari zenu, nimekuja kwa ushauri wenu pamoja nakuweza kupanua mawozo yangu nakupunguza stress za kifamilia.
Mimi nina mke na tumejaliwa watoto wawili (2) wakike na wakiume, Mwaka jana mnamo mwezi wa saba (7) mke wangu alinipa taarifa kwamba Mama wake mzazi (mama mkwe) anakuja mjini nijiadae kwenda kumpokea hiyo siku ikifika na ni sisafiri paka nimpokee, kwasababu shughuri zangu nasafiri za nje ya mkoa, nikamuliza amekuja kufanya nini? Eti kufuatilia mafao yake ya pensheni, mmh wakati alisha pokea tangu mwezi wa pili, niliguna tu nikamjibu sawa ntampokea, baada ya kama siku tatu aliniambia amepanda basi, siku hiyo nikaendesha ki 'babywalker' (gari) changu nikaenda standi ya ma basi ya mikoa kumpokea, alingia kama saa sita usiku nikampokea nikaweka mizigo yake ndani ya gari tukaelekea nyumbani vizuri bila kunotisi kitu chocolate.
Baada kama ya siku mbili mie nikasafiri kuenda kwenye kazi zangu, nilirudi baada ya siku tatu (3) nikamukuta bado yupo si ku mind walaa, sisi kiutamaduni na kimila mama mkwe ni mwiko kwangu kuingia chumbani mwake au kumshika mkononi au kutumia choo kimoja kwahiyo nilikuwa namsalimia nikiwa sembuleni kila asubuhi na jioni hiyo wiki nilio kaa sikumtizama sanaa isipokuwa usiku wakati namleta aliendelea kukaa nyumbani kwa takrbani miezi mitatu, mie naenda safari zangu na rudi kila wiki kwa kufichwa na mke wangu.
Kumbe Mama alikuja kufanikisha masuala mawili: hayo yote nilikuja kugundua badaye sana.
Yule mama alikuja kuugulia kwangu auguzwe na mtoto wake (mke wangu) na kuaga watoto wake wengine walioko jijini. Kwangu ndo pakawa kitovu cha mikutano na kuendesha vikao vyao wakati mimi sijui lolote.
Wife kanificha sijawahi ku-imagine kitendo kama hicho. Kumbe mama alikuwa ameshaathirika siku nyingi na virusi vya huu ugonjwa wa kisasa (VVU). Mwili wote ulikuwa umejaa vidonda na ulishabadilika kuwa mweusi na vipele kote.
Kuna siku nilichelewa kutoka nikakuta watoto wake wote watano wako nje, nikashangaa lakini sikumind sana kwasababu wife kaniambia wamekuja kusalimia mama yao. Nikasema poa kumbe kilikuwa kikao cha familia.
Huyu suala la pili baada ya kupokea pensheni yake alikuja kununulia watoto wake nyumba kama kitega uchumi kwasababu siku zake zilianza kuhesabika, kifo kinasongea na hali yake iliendelea kuzorota.
Lakini kumbuka mtoto wake wa mwisho ana miaka 27. Alifanikiwa kupata nyumba hapa mjini, alivyofanikisha hayo akawa anataka kuaga kurudi mkoani baada ya kukaa kwangu miezi mitatu bila mimi kujua. Hata hakuniaga, natoka safari zangu nakuta mama kasharudi mkoani wife ndo kanipa taarifa eti amenipa salamu tu.
Kama mtafutaji na asiye na makuu wala kinyongo niliyapuuzia wala wife sikumuuliza tena kuhusu Mama. Nilikaa nyumbani kama siku tano hivi, tena nikawa nataka kusafiri kuenda kwenye biashara.
Kama kawaida nilimuachia mahitaji ya nyumbani nikaondoka. Baada ya siku kama mbili wife kanipigia simu huku analia tena kilio chenyewe cha kwikwi. Nikamuuliza kulikoni, kanijibu mama anaumwa kalazwa hospitali ya rufaa na kawekewa oksijeni.
Niliduwaa kwasababu sikuwa na taarifa yoyote nyuma kwamba alikuwa anaumwa. Nikamuuliza alipata ajali? Akajibu hapana nitakuambia we tuma pesa niende nimuone.
Sikuchelewa nilijipigapiga nikamrushia laki mbili za nauli na kujikimu. Alivyofika nikaanza kumuuliza mama anaumwa nini hanijibu. Nilikazana kweli kweli kumuuliza kweli ila anaishia kuniambia yuko kwenye oksijeni.
Nikagoma kumtumia pesa mpaka aniambie Mama anaumwa nini? Baada ya siku mbili kaniambia ila baadhi ya wake zetu ni waongo tena uongo wa kitoto. Aliniambia eti anasumbuliwa na (ulcers) vidonda vya tumbo, ndo kawekwa kwenye mtungi wa oksijeni!!!!!!!
Ilikua Alhamisi mwezi jana mtu tunayefamiana naye ambaye ni jirani na ukweni pale kanipigia simu kunipa pole ya kufiwa.
Sikutaka kumuuliza nani amekufa angejua kama kuna usiri mkubwa kati yangu na wife na angenishangaa kutojua huo msiba. Niliitikia vizuri na nilihisi atakuwa mama ndo amefariki.
Kusema ukweli wife hakunipa taarifa mpaka saa 11 jioni wakati mtu alifariki saa mbili asubuhi. Nilijiongeza haraka nikapata usafiri mpaka mkoani. Nilifika mapema tu kwasababu nilikuwa na hela ya ziada nikapanda ATCL ya mchana nikidhani mazishi yatakuwa siku hiyo hiyo. Wife anakuja kunipa taarifa tayari nimeshafika kwao, hana taarifa, lengo lake lilikua nishindwe kuhudhuria mazishi.
Mazishi yalipangwa kesho yake saa saba. Wife alidhani kuniambia saa 11 sitaweza kupata usafiri wa haraka ili nikae na wafiwa pamoja na nzengo.
Kusema ukweli nilishindwa kukutana na wife hiyo siku kwasababu hasira na jaziba nikakimbia makaburini kule kushiriki na wachimbaji. Kule ndo nilipata mkanda mzima wa kuugua na kufa kwake mama mkwe wangu.
Watu wana maneno wanadai “alikufa kwa ngoma” eti alienda kujificha kwa watoto wake jijini. Anyway nilipata kila kitu pale vyote wife alivyonificha.
Sasa naomba msaada wa ushauri kwenu. Siku 40 (arobaini) zimetimia na dua ya arobaini tayari. Wife tangu wiki jana ananipigia simu nimtumie pesa za kurudi nyumbani. Nilisita kidogo sijamjibu chochote kwa sababu bado nina hasira nae, kunitumia kama boya-jinga-fala kwa kunificha hayo yote.
Ila vyote umesema sawa ila wanawake wajifunze kuwa wawazi kwa waumme zao.....inauma sana unamwangaikia ila yeye ana yakwake tu.Yaani wife wako kakaa msibani mpaka siku 40 zimeisha?
Hana kazi!?
Hana biashara za kusaidia kusukuma maisha?
Hajali familia yake!?
By the way, msamehe tu mkuu.
Kuna wakati akili huwa inachanganyikiwa.
Na Mambo yanakuwa magumu.
Kuuguliwa sio mchezo hasa pale unapojua mgonjwa Ana ugonjwa mgumu usiokuwa na matumaini ya kupona.
Alichokosea ni kutosema tu mwanzoni kuwa mama anaumwa amekuja kujiuguza!!
Lakini hata Kama walikuwa wanajadili Mambo yao wewe yasingekuhusu mpaka yawe yanaingilia na familia yako.
We dada unakili sana unaupeo wakuchambua mambo nyuma ya pazia nimependa ushauri wako.Watu wanamshauri huyu bwana kwa kuangalia uwongo wa mwanamke kuhusu ugonjwa wa mama yake mpaka kifo,hapo naona siyo sawa. Inaonekana kuna vitu vingi huyu mama anamdanganya huyu bwana ila Mungu kakuwezesha kunasa hayo machache mazito utafute ufumbuzi wa matatizo ya mke wako. Mtu muongo ni mtu mbaya sana,hata jamaa anavyoogopa kulala nae kitanda kimoja ni sahihi kabisa,ushauri wangu huko aliko ndiyo sehemu sahihi ya kuyazungumza kwani ndiyo kwao. Mwambie nakuja huko kwa mazungumzo hayo wao waandae watu upande wao,na wewe panda na mtu mmoja wa kwenu mkayazungumze. Asitie mguu kwako hadi kieleweke,ikishindikana waachie binti yao huko huko. Uongo ni zao la dhambi nyingi sana,fanyia kazi hayo mapungufu ya mkeo mapema
We dada unakili sana unaupeo wakuchambua mambo nyuma ya pazia nimependa ushauri wako.
Mkuu nashukuru sana kwa ushauri maridhawa.....ila changamoto iliopo ni roho yangu kukubaliana na ukweli kwamba nimsamahe, napokumbuka jinsi alivo kua ananiomba pesa ya nyumbani matumizi yaliongezeka maradufu, wakati inaenda kwa matibabu ya kificho kwa mama inauma sanaaa duh.....
Sawa time heals ila nguvu za kuenda stedi ucku wamanane kuenda kupokea mtu muongo kama huyu cijapata, pia kulala nae kitandani sijui kama I have the guts,......naona mgogoro wa ndani kwandani unaanzia hapo
We naë una gubu
Unataka kukuza mambo badae muishie pabaya wakati tatizo lenu lingeweza kuwa solved na mkaendelea na maisha
Ndoa inahitaji uvumilivu na mtu anaeweza kusamehe unataka ku move on uende wapi[emoji2374]
Ungekuwa umemfuma na mwanaume ningekushauri umpige chini fasta
Huyo alikuficha kwasababu zielewe na mkemee tabia ya usiri msonge mbele
Punguza kubeba mizigo ambayo ni unnecessary unajipa stress za bure
Sorry kwa ku-kwa address kama Dada nisamehe......ila suala la uaminifu hapa Africa tunawana kama dogo wakati ndo mama wa madhambi yote...mkeo hakishindwa kua honesty kwako anaweza kutenda Dhabi kubwa zaidi.Mkuu mimi siyo dada,na nimemshauri mwanaume mwenzangu nikiwa na hasira sana. Hawa dada zetu sijui huwa wanataka nini. Mzungu ukimdanganya akagundua hakuamini tena maisha yake yote. Wanaogopa uongo sana wale jamaa
Yupo hawakua na maelewano kama miaka mitano nyuma japo walikua wanaishi nyumba moja na hilo nililijua siku ya mazishi kwa wachimba kaburiSamahani, baba mkwe yuko?
Sio kweli mie niko simple sana wala sinaga makuu ila nachukia uongo kwasababu nimelelewa kwenye misingi ya diniMkeo amefanya makosa sana kutokukwambia yote hayo , lakini kabla ya kumlaumu kwa makosa hayo hebu jitathmini na wewe kwanza , inawezekana upo strict na serious sana kiasi kwamba mtu kukwambia Jambo anajishauri Mara mbili mbili,
Jaribu kuwa flexible na easy , na usiubebe uanaume wote Kama tunavyotambiana humu ,kwamba bila kuwa hivi au vile wewe sio mwanaume kamiii!! Bro as long tuna kengele hapo down stairs inatosha kuwa mwanaume .
Hii ya ku practise manship over women inatucosts sana na ndio sababu tunakuwa wa kwanza kuaga dunia tukiwaachia neema wake zetu
Kwa ushauri wangu mtumie nauli then unahitaji kumuweka sawa ,alifikiria ilikuwa njia nzuri hiyo ya kuficha !Ndugu zanguni habari zenu, nimekuja kwa ushauri wenu pamoja nakuweza kupanua mawozo yangu nakupunguza stress za kifamilia.