Mke wangu kaninasa kibao, nifanyeje?

Mke wangu kaninasa kibao, nifanyeje?

Habari za leo wananchi wenzangu wanyonge.
Poleni na msiba wa kiongozi wetu sisi wanyonge.
Ndugu zangu,naombeni ushauri wenu wa mawazo,leo nilikuwa nimekaa na wife tunacheck tv,ikaingia message kwenye simu yangu, wife akaichukua haraka haraka na kuisoma,nikashangaa ameniangalia usoni kisha akanilabua kibao kwenye shavu, akanirushia simu yangu kisha akaingia chumbani, me nikaisoma ile message ilikuwa imetoka kwa mdada mmoja tumezoeana kutaniana, yeye huwa anapenda kunitania kwa kuniita husband nami namuita wife, so nimeshangaa wife wangu hajaniuliza kitu badala yake kanipa kelebu.
Je nifanyaje wakuu?
Una utoto kwa sababu mbili
1. Una mazoea mabaya na mkeo hadi anakulamba kofi tena msimu wa masika !!! na baridi hizi
2. Umeoa halafu bado unabebishana na vidada huko nje, huu ni ufala
3. Baridi zote hizi unakaa na mkeo mnaangalia Tv, tena itakua mnacheki tamthilia ya mama Kimbo😂
 
una utoto kwa sababu mbili
1.una mazoea mabaya na mkeo hadi anakulamba kofi tena msimu wa masika !!! na baridi hizi
2.umeoa alafu bado unabebishana na vidada huko nje, huu ni ufala
3.baridi zote hizi unakaa na mkeo mnaangalia Tv, tena itakua mnacheki tamthilia ya mama kimbo😂
Ushauri wako ni nini mkuu?
 
Ushauri wako ni nini mkuu?
hahaha😂 nyie ndio wale ambao mwalimu katoa notice za advantages za kitu fulani alafu kwenye test akaleta swali utaje disadvantages na bado mnakosa
ukinisoma hapo nimetoa na ushauri kwamba, u act kama mwanaume hapo nyumbani kwako na uache mazoea ya kitoto na vibinti mtaani maana wewe umeoa
 
Sawa mkuu..umeeleweka
 
Ningalikuwa Mimi ningalimshika ningalimsogeza Kisha ningalimpa vifuti vinaitwa dunia hadaa walimwengu shujaa! Hivi huwa vinapigwa kwenye shingo! Kisha ningalimpapasa kwa pigo maarufu liniitwalo mtama lkn mtama huu unakuwa ni mtama uliochangamka yani anapaa kimo Cha mbuzi na kabla hajatua chini akiwa juu juu anakula ngumi mbili za chemba ya moyo Kama sehemu ya kumsindikiza ktk safari yake!

Akitua chini ntahakikisha hapumziki hapohapo naweka pigo moja linaitwa "zunguka huko nami nizunguke huku tumfinye mshenzi" hili ni pigo la pua Yani unampiga kichwa Cha pua na ili liwe tamu zaidi pigo hili linafaa umpige huku umefumba macho! Kisha angali yupo ktk kilio punde si punde unampapasa mbavu zake kwa pigo linaitwa Israel yu malangoni pako! Hilo unapiga kwa kutumia magoti huku ukibana pumzi ili kuhakikisha pigo linapata patamu na kwa spidi ya haramu! Hapa lazima atahema kwa kukosa hewa hivyo akipiga zogo unasimika ngumi ya mdomo ili kuubadilisha usiitwe tena mdomo bali mudomomo!

Narudi..
 
Habari za leo wananchi wenzangu wanyonge. Poleni na msiba wa kiongozi wetu sisi wanyonge.

Ndugu zangu,naombeni ushauri wenu wa mawazo. Leo nilikuwa nimekaa na wife tunacheck tv, ikaingia message kwenye simu yangu, wife akaichukua haraka haraka na kuisoma. Nikashangaa ameniangalia usoni kisha akanilabua kibao kwenye shavu, akanirushia simu yangu kisha akaingia chumbani.

Mimi nikaisoma ile message ilikuwa imetoka kwa mdada mmoja tumezoeana kutaniana, yeye huwa anapenda kunitania kwa kuniita husband nami namuita wife, so nimeshangaa wife wangu hajaniuliza kitu badala yake kanipa kelebu.

Je, nifanyaje wakuu?
Wewe ungekuta meseji kama hiyo kwenye Simu yake ungefanyaje?..

Nakushati tu mtlfate room mkafanye kitu cha makeup... ugomvi uishe[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Habari za leo wananchi wenzangu wanyonge. Poleni na msiba wa kiongozi wetu sisi wanyonge.

Ndugu zangu,naombeni ushauri wenu wa mawazo. Leo nilikuwa nimekaa na wife tunacheck tv, ikaingia message kwenye simu yangu, wife akaichukua haraka haraka na kuisoma. Nikashangaa ameniangalia usoni kisha akanilabua kibao kwenye shavu, akanirushia simu yangu kisha akaingia chumbani.

Mimi nikaisoma ile message ilikuwa imetoka kwa mdada mmoja tumezoeana kutaniana, yeye huwa anapenda kunitania kwa kuniita husband nami namuita wife, so nimeshangaa wife wangu hajaniuliza kitu badala yake kanipa kelebu.

Je, nifanyaje wakuu?

Pole sana mkuu kwa kulabuliwa 😂 Ila ni mambo ya kawaida tu vumilia na siku nyingine usiweke simu kihasara hasara hasa kama uko nae karibu.
 
Habari za leo wananchi wenzangu wanyonge. Poleni na msiba wa kiongozi wetu sisi wanyonge.

Ndugu zangu,naombeni ushauri wenu wa mawazo. Leo nilikuwa nimekaa na wife tunacheck tv, ikaingia message kwenye simu yangu, wife akaichukua haraka haraka na kuisoma. Nikashangaa ameniangalia usoni kisha akanilabua kibao kwenye shavu, akanirushia simu yangu kisha akaingia chumbani.

Mimi nikaisoma ile message ilikuwa imetoka kwa mdada mmoja tumezoeana kutaniana, yeye huwa anapenda kunitania kwa kuniita husband nami namuita wife, so nimeshangaa wife wangu hajaniuliza kitu badala yake kanipa kelebu.

Je, nifanyaje wakuu?
We ni wa Dar sehemu gani?
 
Mkeo hana makosa wala huna haja ya kutaka kumfanya cho chote! Yeye baada ya kuisoma angeminije kama huna uhusiano wa kimapenzi na huyo mwanamke?
 
Wife wako mpole Mimi ningekupiga migumi hyo mpaka ushangae.
 
Back
Top Bottom