Mke Wangu katoroka na watoto wetu wa nne. Naombeni ushauri

Sio kweli, mama mkwe sio tatizo. Tatizo ni mke wake kamfungulia mlango mama yake.

Huyo mke sio mtoto wa kuendeshwa na mama. Angekuwa wa kuendeshwa angemsikiliza mume au kuendeshwa na mume
mama mtu ni mtu mzima na ana uzoefu na mambo ya ndoa, ilitakiwa akatae kuingilia mambo ya ndoa ya mwanae.
Sasa hapo inaonesha mama mtu ndio anapenda hizo mambo.
 
Upo sawa mtu huwez kupokea Mwanamke na watoto wanne ngumu sana Cha msingi akuletee watoto
 
Una uhakika ni wa kwako hao watoto au ndo tuseme watoto ni malaika hivyo twapaswa kuwapenda tu.
 
Mkuu mkeo anakujua fika hufulukuti. mama mkwe kabisaa anajua hapa hakuna mwanaume.
Mimi mama mkwe hawezi hata kupiga simu kunambia hivyo.Mkeo navyohisi hii sio mara ya kwanza kwenda nawewe ukamfuata tena kwa kumuomba msamaha huku ukimhakikishia huwezi ishi bila yeye. kwa hali hii kuondoka na watoto4 sio rahisi hivyo wanajua utalilia tu na kumuomba arudi tena.

Ushauri kwa vile una uhakika yupo kwao na anawasiliana na majirani ili arudi funga kabisa kwako uwe unakuja kwa machalee tu akikupgia simu mwambie watoto apandishe kwenye gari na umwambie "WEWE ENDELEA NA UMALAYA WAKO" Mjomba sio mwehu kumwambia arudishe watoto halafu yeye aendelee kula usimbe vizuri unajua wazi mtu akiitwa msimbe.
 
mama mtu ni mtu mzima na ana uzoefu na mambo ya ndoa, ilitakiwa akatae kuingilia mambo ya ndoa ya mwanae.
Sasa hapo inaonesha mama mtu ndio anapenda hizo mambo.
Ndugu yangu, bado haujawafaham wanadamu vyema.

1. Nani alikudanganya wajinga hawazai?
2. Nani alikudanganya wajinga hawawi watu wazima?
3. Nani alikudanganya wajinga hawazeeki?

Kuwa makini na kila mtu, utu uzima na uzee sio kipimo cha HEKIMA
 
mama mtu ni mtu mzima na ana uzoefu na mambo ya ndoa, ilitakiwa akatae kuingilia mambo ya ndoa ya mwanae.
Sasa hapo inaonesha mama mtu ndio anapenda hizo mambo.
Kwanza tu hapo onavyoonekana mama mtu hana mume. Kwanini?

Jamaa kaongelea wajomba wanasema hawawezi kulea watoto wa mtu.

Kwanini aseme wajomba na sio baba ya huyo mke wake. Huyo mama mtu ndoa ilishamshinda na anaharibu ya mtoto.

Halafu tena, mama ndie alimpigia sim mkwe kumwambia ameshindwa kukaa na mtoto wake hivyo hatakaa amuone. Baba yupo wapi hapo? Simuoni na hata yeye huyo muoaji haongelei kabisa habari ya baba wa aliekuwa mke wake😄
 
Mama mtu ni kivuruge anataka avuruge na ndoa ya mwanae.
 
k
 
Poleni
 
Asante mkuu.
 
Sioni:

1. Kwa nini ulimyima kwenda na Mama yake?
2. Kwa nini ulimnyima tena na nauli

Sio kila kitu ni kupambana na mwanamke, kuna siku utaona madhara, kuna vita zisizo za Msingi wewe mwache azishinde vizuri tu kwa amani!
Ushauri wa hovyo kabisa na kama umeona basi wewe ni Mume wa hovyo
 
Ushauri wa hovyo
 
Umemaliza..Ushauri wa kiumeni sana
 
Mrejesho
 
Peleka shauri hili Dawati la Jinsia polisi ya wilaya unayoishi.

Mama Mkwe piga block ya maana
Mke chapa block
Mkutane Dawati ndo wataelewa thamani ya familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…