Japo haujaelezea kiundani, Ila kuna namna wote mna makosa, Tuanze kwako, Inaonekana haukumjibu vyema na kwa hekima mama mkwe wako, Inaonekana alikuomba kistaarabu, Ulipaswa kutumia kauli nzuri kumuelezea na sababu muhimu ya wewe kumkatalia ombi lake, Angekuelewa. Pili Mke wako hakupaswa kumsikiliza yeyote na maamuzi ya mwisho kuhusu kubaki au kuondoka yalipaswa kuwa juu yako, Mpaka kufikia hatua ya kudharau maamuzi yako, maana yake kuna level kubwa ya uchoyo na ubinafsi umemuonyesha. Kwa mfano, amekwambia kwamba ana mgonjwa, kikawaida na kibinadamu ulipaswa umruhusu na umpatie nauli, Je kama mgonjwa ni ndugu wa karibu? je angefariki? pia inaonekana huwa haumhudumii vizuri na kuna cases nyingi ambazo haujazielezea mpaka wao kufikia hatua hiyo.
SOLUTION; kaeni chini, wakiwepo wazazi na wazee, mzungumze, yaishe kwa ajili ya watoto.