Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

Mke wangu mtarajiwa hataki mtoto wake aliyempata kabla hatujakutana atumie ubini wangu

[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]sipati haya akale alikopeleka mboga sasa!!!ngoja dunia imcheke na ukute ex na mashosti ndo walimshauri huo ujinga sasa akae atulie!
Na kwa kua alijua kuna ndoa karibu akajua ashakuweza tayari huna maamuzi ten
Dah mwanamke mwenzetu huyo ujue..
Kosa moja na kuachwa juu
Q
Hata kama weee ni single maza mwanaume hana haki ya kubadili jina la mwanao bila kukaa na wewe kwanza na kujadiliana.
Angechukulia tu kibinadam amsamehe kwa kuwa ameomba msamaha kwa majibu mabaya
 
Natarajia kuoa hivi karibuni na mke mtarajiwa ana mtoto wa miaka 5. Huyu mtoto namhudumia kwa kila kitu na namuonesha upendo wote kama baba yake mzazi.

Kuna shida imejitokeza baada ya kumpeleka mtoto aanze shule (nursery school ). Katika kujiandikisha nikampa jina langu la ukoo (Eg. Ngwengwe) madaftari full mkoba jina nimeandika Kelvin Ngwengwe.

Bhana eeh, mama yake alivyoona madaftari amechana chana, kumuuliza kisa nini mbona umechana madaftari ya mtoto?? Jibu alilonipa limeniacha hoi.

Namnukuu "Huyu mtoto baba yake yupo hai kwanini usitumie jina la ubini wa baba yake mzazi badala yake umetumia jina la ubini wa kwenu! Zaa mtoto wako umuite jina la kwenu"

Maamuzi niliyochukua ni kumpiga chini tu

MREJESHO
Jana ugomvi ulikuwa mkubwa ila nilitumia busara nilikaa kimya sikusema chochote alienda mbali zaidi akasema tuachane kimoyo moyo nikasema umeisha.
Leo asubuhi amekuja na mama yake mzazi kusuluhisha ugomvi binti amekiri kuwa amekosa zilikuwa ni hasira tu.
Maamuzi niliyochukua sikupepesa macho nilimwambia mama kuwa siwezi kuendelea na binti yako pia mahari niliyoitoa nimesahmee.
Mpaka sasa simu yangu ina missed call 80 ,sms 30
Na ukirudi umekwisha .
Ukiweza weka block endelea na maisha baadhi ya vitu ni vyema kuchukua maamuzi after first statement.
 
Masingle maza wengi bado akili zao wanashikiwa na baba za watoto zao ndo maana Hata Baba watoto akitaka kumgonga muda wowote anakulaaa tuu yani
Huyo demu mjinga sanaa!na hao ndo wanafanya singo maza wadharaulike yaani!!mshikaji kakataa mtoto tena na familia nzima wamekataa anatokea mtu anakupa hadhi ya kukustiri na hizo matusi bado unadiss kirahisi hvyooo!!!demu jinga sana huyuu atajuta atachekwa mpk na sisimizi!
 
Majibu yake ndo yalikuwa mabaya sana na ya kinyama japo mwanaume nae alipaswa amjulishe kwanza habari ya jina wakat wa kumuandikisha. Kumuacha pia j8 maamuzi ya hasira mnoo
Uko sahihi lakini mdada asingepaniki angemuuliza taratibu mkaka Mimi nnae my friends watoto wake wanatumia ubin wa kwao kwa kua baba alikataa mapacha!na kuhusu kuachwa namuonea huruma lakini huwezi jua nini kilitokea
 
Dah mwanamke mwenzetu huyo ujue..
Kosa moja na kuachwa juu
Q
Hata kama weee ni single maza mwanaume hana haki ya kubadili jina la mwanao bila kukaa na wewe kwanza na kujadiliana.
Angechukulia tu kibinadam amsamehe kwa kuwa ameomba msamaha kwa majibu mabaya
Nakuelewa binamu sana tu na namuonea huruma huyo Dada, busara inapaswa itumike amsamehe lakini ujue mwanaume kua na singo maza ni maamuzi ya kiume mnoo!familia nyingi zinakataa na ukute alikua anamprotect against all odds Leo Dada alipaswa akae chini ajiulize kabla hajafanya maamuzi ya kukataa ubini wa msweden!
Msweden msamehe WiFi yetu
 
Kaka achana nae huyo Dada!yaani ukatae mtoto bado nkubembeleze Mimi huyuu!
Sijui nimeumbwaje aseehh!!nna roho mbaya sana!!yaani sina mda huoo! Huyo bado ana interest na mshikaji wake
Mimi sioni kosa la mke hapo, mke anachosema ni fact.

Ni fact kwamba huyo mtoto ana baba yake (tena bado anaishi), na ni haki ya mtoto kulijua hilo bila kujali baba kakataa mimba au hajakataa.

Suala la mtoto kuitwa jina lake ni suala la maelewano kati yake na mke wake (ikiwa baba halisi hayuko kwenye picha) na sio alazimishe.

Kama vipi asubiri mtoto akue amchague yeye kua baba kwenye majina yake[emoji16][emoji16]
 
Dah mwanamke mwenzetu huyo ujue..
Kosa moja na kuachwa juu
Q
Hata kama weee ni single maza mwanaume hana haki ya kubadili jina la mwanao bila kukaa na wewe kwanza na kujadiliana.
Angechukulia tu kibinadam amsamehe kwa kuwa ameomba msamaha kwa majibu mabaya
Suala la kubadili jina mostly ni maamuzi ya mama mtoto. Hivi mwanaume anaanzaje kulazimisha mtoto wa mtu mwingine awe wake? Kwani ye hazalishi?
 
Mzee baba ..huyo mnyooshe tu kwa MDA lakini usimuache.....

Wanakushauri hapa utamu na Raha za shemeji / wifi unazijua wewe...

Naona kabisa unavyo hangaika ..una mapenzi makubwa na hao Ni wenzio... ..

Kama hakuna baya lolote zaidi ya hili usimwache Ila muonyeshe kwa mfano hai Kama ujuba hautakiwi na ajue anaishi vipi na Nani!
 
Huu ni ushauri mbovu kabisa ...
Ukiendeshwa na hisia za mapenzi badala ya kutumia akili kinachofuata nimaumivu tu !
hakuna mapenzi ya kweli kama hauna hisia.
Tatizo akili zako zimesinyaa upande mmoja. Weka thamani ya utu.
kile usichopenda watu wakutendee,,, wewe usiwatendee pia.
kama unaona ni vema huyo mdada akazaakwa mala ya pili bila kufunga ndoa,,,, nenda kazae wewe kwa niaba yake. ila yeye anataka kuziishi ndoto zake. hata huyu mtoa mada analijua hilo.
 
Hii ndio sababu siwezi kuoa single mother, na hii ni bado, huyu unaita mke wako yaonekana bado anangogwa na baba ya huo mtoto wake, shidaiko wapi mtoto kuitwajinalako na ile wewe ndio unalipa ada, unanunua chakulana kila kitu, anyway kaa utamuoa basi ni mali ya wewe pamoja na baba ya huo mtoto wake,na huwa najiuliza kwani mabinti ambao hawana watoto wameisha ndio nioe single mother, bado huyu unaita mkeo atakuwa analiwa na huo baba ya mtoto wake,
 
Ingekua tupo kijiweni unatupa hii stori ningekulamba vibao vya kutosha asee una bahati sana

Kuishi na singo mama ni laana labda awe amefiwa mume wake ila huyo ambae bwanaake yupo we unaishi nae wa nn sasa? Yan kamshinda mwanaume mwenzako tena alianza nae akiwa hana mtoto we unaenda kujibebesha limwanamke shindikanaa likiwa na mtoto kabisa?$

Comments kama hizi mwaka 2022 ni aibu sana. Hivi hujui kuna wanaume wakatili, wanazalisha na kukimbia? Hujui kuna wanaume wanapiga? Hujui kuna kuachwa kwa ajili ya uzinzi? Kwahiyo hao wanawake hawana nafasi ya pili ya kupendwa? Jesus, I am very disappointed. Comments au thread za namna hii ni za kuondolewa mara moja. Mnapandikiza roho chafu ndani ya wanaume sahihi. Na nawaombea nyinyi wanaume mnaotukana single mothers vizazi vyenu vyote viee single mothers. Shenzi kabisa wewe.
 
Sasa unataka atumie jina lako umem- adopt??? Vyeti vya kuzaliwa vimeandikwa ubini gani???

Embu usitake kumchanganya huyo mtoto bila sababu ya msingi. Kama ungekuwa na akili na unaona ni jambo la msingi mtoto kutumia jina lako (for whatever reason 😏😏) then ulipaswa kujadiliana na mama yake kabla ya kujipa mamlaka ya kumpatia jina lako.
Jamaa yetu Msweden unafanya mambo kienyeji sana.....🙄
 
Back
Top Bottom