Mke wangu ndiye ukoo wangu, ndugu huna nyongeza yoyote

Kazi iendelee
 
kazi kweli kweli , kila ndoa na changamoto zake hazifanani ila zipo
 
🤣🤣🤣 hapa mjini nimeona style moja, wakaka wengi mke akijifungua anamtafutia mti mzima au nurse mstaafu wa kumuhudumia, mama mkwe na mawifi hukooo, sijajua kwa nini labda wakaka watuambie sababu
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] hapa mjini nimeona style moja, wakaka wengi mke akijifungua anamtafutia mti mzima au nurse mstaafu wa kumuhudumia, mama mkwe na mawifi hukooo, sijajua kwa nini labda wakaka watuambie sababu
Hahaa Mi siku nkipata mtoto ntafanya hivohivo..kuna baadhi ya ndugu NI nuksi maradufu.kuna mwenzangu ye yamemkuta hayo hana hamu.eti Wifi kaja anamuogesha mtoto wake wa miaka 2 akaanza kumzungusha vile yupo uchi eti "ohh huyu mtoto hafanani kabisa na naniliu(kakake)..yaani hawafanani kabisa"

Huu si ushetani lakini?
 
Kwa tuliopitia mafundisho ya ndoa, mke na mume ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu umoja wao,hakuna cha baba, mama wala ndugu wanaoweza kuingilia ndoa yenu. Wazazi na ndugu walikuwa na nguvu kabla ya kufunga ndoa, ila kama umefunga ndoa...pambana na mwenzako
 
🤣🤣🤣 hapa mjini nimeona style moja, wakaka wengi mke akijifungua anamtafutia mti mzima au nurse mstaafu wa kumuhudumia, mama mkwe na mawifi hukooo, sijajua kwa nini labda wakaka watuambie sababu
Unaepusha shari na misongamano isiyokuwa ya lazima
 
Kazi kwelikweli, kwa sasa naona mjini hawakaribishi mawifi wala mama mkwe, kuna mmoja aliniambia amemuajiri nurse mstaafu kumuhudumia mzazi na anamlipa shilingi laki tatu kwa mwezi, baada ya mwezi mke anakua ameshakua sawa anasaidiwa na dada wa kazi, anasema kuna wakati mama yake mzazi alikuja kumuhudumia mke wake nyumba haikukalika, mke akipikiwa supu mama anasema mnatumia gharama nyingi, mke akitaka matunda mama anasema anajidekeza, mke akilala mama anasema mzazi huyu legelege, mama anapanga ratiba ya chakula ambayo wao hawajaizoea, mama anademand mpaka wanajuta, gharama za maisha zikawa kubwa na wakato mama anaondoka kurudi kijijini anadai na hela ya mtaji akafanye biashara, bado hujamfanyia shopping, bado nauli, na mambo mengine mengi, anasema alikwazika ila walavumilia muda ulipoisha mama akaondoka

Kuanzia hiyo siku hajawahi kumwita mama wala ndugu kumuhudumia mkewe, wanacheza show wenyewe na maisha yanasonga
 
NB. Ili umuamini zaidi mkeo pia jitahidi akupatie watoto wa kutosha, ila ukiishia mtoto mmoja au wawili ipo siku atakutenda na kuanza kuwakumbuka ndugu au wazazi wako uliowapa kisogo; kuchapiwa ni siri ya ndani
 
Huyu mama mmhh
Mi kuna kitu sielewi,inkuwaje unakaribishwa kwenye nyumba ya mwingine halafu unaanza kuwapangi a vile unavotaka wewe waishi?
Hata huyu pia hivohivo.mgeni ni Wifi anafokafoka tu hii nyumba mnakula ovyoovyo.kisa ye msabato akiona mtoto kashika soda anampush huko.akiona keki hataki
Ye anataka mpike makande tu na mboga za majani.hataki nyama wala samaki wala dagaa
 
Hahhaa ila nimecheka jamani, eti akiona mtoto ameshika soda anampush, watu wengine wana tabu sana, sijui huwa mentality zao zimejaa kitu gani
 
Mkuu acha masihara utakaoa kadada kako kweli .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…