Mke wangu ndiye ukoo wangu, ndugu huna nyongeza yoyote

Mke wangu ndiye ukoo wangu, ndugu huna nyongeza yoyote

Niende kwenye hoja ,kumekuwa na desturi za ndugu na jamaa kuingilia Mambo ya NDOA za watu na kutoa ushauri utadhani wao walisona vyuo vya ndoa.
Ninavyojua Mimi ndoa haiwezi kua na amani maisha yenu yote Kuna siku mnatofautiana

Mtu unamsema mke wa mwenzio vibaya Mara siyo lika ,lako Mara ni mfanyakazi atakunyanyasa ,Mara mchoyo ,Mara hapendi ndugu, Sasa Kama mawifi ni wanafiki asiseme eti kwa sababu kaolewa????

Binafsi sipendagi ujinga Kama huo nikimuacha mke wangu NAOA ndugu Sasa ili tuone hatima yake

Nawasalimu kwa jina la jamhuri..
Inaonekana hujawai kuwa na mahusiano mazur na familia yako baba yako mama yako dada zako ambao umeish nao nusu ya maisha yako under same roof..umekuja kutana na stranger in a year umeoa sasa unaona ndugu zako si chochote si lolote..

Kwel mbuny.e ni silaha hatar zaid ya WMDs.

Mwanaume hajawai shinda kihistoria tangu ulimwengu huu uanze...
 
Pale ambapo utamuhusisha sana mkeo na ndugu ndio hupelekea mazoea hayo. Principles zangu,
1. Mke ni wangu na hawezi kuwaridhisha ndugu zangu wote japo hawezi wadharau,
2. Sijazi ndugu nnapoishi na mke wangu, mimi, mke na watoto..kuja kusalimia sawa ila sio kuishi pamoja
3. Nasaidia ndugu wakiwa mbali sio kuchagamana nao,
4. Mambo ya familia/ndugu nawambia wanitafute mimi, kila ndugu yako akiwa na ukaribu na mkeo kwa familia za kiswahili ataambiwa mambo yako mpaka ya utoto, weka mipaka
5. Above all, wazazi wangu ni muhimu kuliko mtu yyte, ninapofanya mambo yawahusuyo inabidi atulie!
N.B mke sio ndugu yako, ni life partner, hivyo basi ishi nae kwa akili usivuruge ndoa kwa ajili ya ndugu zako and virse versa is true!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo 5 na NB ndo umeuwa sasa,hongera

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mmh huko ujaluoni bana shida yenu moja....nilishakuambia 😂
Hahaa Mi siku nkipata mtoto ntafanya hivohivo..kuna baadhi ya ndugu NI nuksi maradufu.kuna mwenzangu ye yamemkuta hayo hana hamu.eti Wifi kaja anamuogesha mtoto wake wa miaka 2 akaanza kumzungusha vile yupo uchi eti "ohh huyu mtoto hafanani kabisa na naniliu(kakake)..yaani hawafanani kabisa"

Huu si ushetani lakini?
😄😄😄hahahaha
 
Pale ambapo utamuhusisha sana mkeo na ndugu ndio hupelekea mazoea hayo. Principles zangu,
1. Mke ni wangu na hawezi kuwaridhisha ndugu zangu wote japo hawezi wadharau,
2. Sijazi ndugu nnapoishi na mke wangu, mimi, mke na watoto..kuja kusalimia sawa ila sio kuishi pamoja
Kamwe usiruhusu mke wako au ndugu zako kujua msimamo wako maana ndio utakua udhaifu wako, na ndio chanzo kikubwa cha migigoro. We hakikisha unaenda sambamba na yeyote atakaeleta bangi. Mke akijua unamfavour atadharau ndugu zako, vilevile ndugu ukiwafavour watamdharau mke wako.

Hata hivyo mimi sijaoa najua nini[emoji28][emoji28].
 
Nakumbuka mama mkwe wangu aliwai kuja kusimamia kijana anifukuze eti acha akusanye kila kilichochake, mpishe kwanza....akamchukua wakatoka akijua kijana kanipa muda hatorudi siku iyo analala kwao [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] jioni mr akarudi Kwake km kawaida na mahaba na kuomba msamaha juu eti ndugu zangu waache ndoa ni mimi na wewe! Mama akagundua kijana hakulala kwao asubui saa 12 kafika eti mumeo yupo nkamwambia yupo akamfuata chumbani bado amelala hana habari nliona mama anatamani kulia
[emoji23][emoji23][emoji23]
Wamama wa mjini wa shida sana!

Sie wengine mama zetu wapo zao kijijini huko tumewawekea tu mazingira mazuri tunatuma vihela vya chumvi na kuweka vibarua shambani, ukimpigia simu utasikia msalimie sana mama (yani mke wangu).
Habri za mnaishije kamwe huwezi kuzisikia.
 
Kila mmoja anahaki juu yako, usiache mke sababu ya ndugu na usimuache ndugu yako sababu ya mke wako.

Jipe muda kutafakari bila ushauri wa mkeo wala ushauri wa nduguyo, kisha weka kila kimoja mahala pake.

Unaweza ku guarantee uhusiano wako na ndugu yako kuwa hautoweza kuvunjika mpaka kifo ila huwezi ku guarantee uhusiano wako na mkeo kuwa hautoweza kuvunjika mpaka kifo hatakama utakuwa mwema kwake kwa maisha yako yote.

Mkeo akiwa bora kwako huwa bora kuliko hata ndugu yako, ila haiondoi ubora wa ndugu yako kwako.
Kila mmoja anaumuhimu wake.

Mke ni ndugu yako ikiwa atavumila kuwa na wewe katika hali za aina mbili: wakati wa matatizo kama kesi, kuyumba ki uchumi, ajali au maradhi. Pili ni kukuvumilia katika umri wa uzee wako maana uzee huja na mengi.
Katika maeneo mawili hayo wengi wametengwa na ndugu.

Ila unapokuwa kijana unaafya, pesa na nguvu ya ushawishi mke kwako ni rafiki mwema, muhimu ni kuishi nae kwa wema.
 
Jamaniiiiiiiii

This is my wifi kabisa

Ila nimemweka mahala pake...ni kumchorea mstari tu ajue mipaka yake

Hakuna stori salamu na kuzungumza mambo ya msingi

Na nilimueleza nanunua vyakula ilj watoto wale.....watu wazima hata wakishinda njaa hainisumbui
Huyu mama mmhh
Mi kuna kitu sielewi,inkuwaje unakaribishwa kwenye nyumba ya mwingine halafu unaanza kuwapangi a vile unavotaka wewe waishi?
Hata huyu pia hivohivo.mgeni ni Wifi anafokafoka tu hii nyumba mnakula ovyoovyo.kisa ye msabato akiona mtoto kashika soda anampush huko.akiona keki hataki
Ye anataka mpike makande tu na mboga za majani.hataki nyama wala samaki wala dagaa
 
Jamaniiiiiiiii

This is my wifi kabisa

Ila nimemweka mahala pake...ni kumchorea mstari tu ajue mipaka yake

Hakuna stori salamu na kuzungumza mambo ya msingi

Na nilimueleza nanunua vyakula ilj watoto wale.....watu wazima hata wakishinda njaa hainisumbui
Pole
Kikubwa asikukontrol uende vile anavyotaka.
Ukiingia nyumbani ya watu ishi kwa utaratibu uliokuta.huwezi ondoka
 
Niende kwenye hoja, kumekuwa na desturi za ndugu na jamaa kuingilia mambo ya NDOA za watu na kutoa ushauri utadhani wao walisoma vyuo vya ndoa.

Ninavyojua mimi ndoa haiwezi kua na amani maisha yenu yote kuna siku mnatofautiana.

Mtu unamsema mke wa mwenzio vibaya sara siyo lika lako mara ni mfanyakazi atakunyanyasa, mara mchoyo, mara hapendi ndugu, sasa kama mawifi ni wanafiki asiseme eti kwa sababu kaolewa?

Binafsi sipendagi ujinga kama huo nikimuacha mke wangu NAOA ndugu sasa ili tuone hatima yake.

Nawasalimu kwa jina la jamhuri.
UKIONA NDUGU WANAINGILIA NDOA YAKO, TATIZO NI WANA NDOA SIO NDUGU. NDUGU WATAJUAJE YA HUKO KWENU KAMA SIO NINYI MWAPELEKA?? AU NDUGU ZAKO WAMEKUWEKEA CCTV CAMERA HUKO KWENU?
 
Back
Top Bottom