Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Sijui niandike vipi aisee!
Wanawake hakika wana upeo kutushinda wanaume, na kila atakayemsikiliza mke wake atafika mbali.
Kuna jambo nilikusudia kufanya nikawa na pesa pungufu, nikataka nifanye kwa uchache wife akasema usifanye hivyo hebu tulia tunza fedha ulifanye hili jambo kwa ukubwa na kwa ubora. Ndani ya muda mfupi nikafanikiwa kulifanya kwa ubora. Bila wife kunishauri nilidhamiria kulipua chap nimalize.
Nyumba hii tunayoishi imegharimu kama millioni 20, kwa mwanamke ambaye amekulia Kijijini angeona ni smart house lakini wife anaamini ni nyumba ya kupita tu na tutahama huu mtaa twende kwenye nyumba nyingine nzuri.
Kuna biashara ya duka tuliifanya mtaa fulani hapa Dar alinishauri jambo nikapuuza nikafanya kwa ubabe duka likafa.
Wife hajasoma, kaishia la saba lakini anawadharau mpaka wale wanaosimama nyuma ya Rais, anawaona ni wajinga sana, wanafanya kazi ya utumwa. Kumbe unaweza kuwa huna pesa lakini huna mind ya kitumwa.
Wife nilimuuliza ulipwe sh. ngapi utakubali body guard wa Rais akajibu hawezi kufanya kazi ya kusimama huku anayemlinda amekaa.
Mtoto wetu wa kwanza alikuwa anaimba kuhusu jeshi. Yaani anapenda kazi ya jeshi mno. Wife anamkataza kila akitamka neno Jeshi . Anamwambia kazi gani ya kuwa mtii muda wote kana kwamba mtumwa.
Kumbe utumwa uko kwenye fikra, na hauwezi kuondoka kwa kusoma.
Ndio maana mtu ana PhD lakini bado ni mtumwa wa Wazungu, anaamini bila wao nothing impossible.