Mke wangu ni mama wa nyumbani, darasa la 7 lakini ana maono, yuko smart na anaona mbali kuliko mimi

Inasemwa hivi hakuna kitu kikubwa katika maisha kama attitude,,ndio maana tembo ni mkubwa kuliko simba na ana nguvu mingi lakini ni chakula ya simba

Simba ana attiude kwamba atamla tembo na ni chakula chake,,haijalishi tembo ni mkubwa kiasi gani

Na wasomi wengi wana skills lkn hawana mtazamo wa mafanikio ndio maana wasio kuwa na elimu wana positive attitude huwaajiri wasomi,,mfano bakharessa na wengineo

So it's all about attitude
 

Si walisema ukipenda boga upende ya lake?

Wengine nao wakasema mapenzi upofu?

Inaweza kuwa huu wako ndiyo upofu wenyewe sasa; tena kwenye ubora wake.
 
Umeandika kitumwa....yahn hata kama mtumwa ila kwa vile nalipwa vizuri sawa sishangai wengi tupo hili kundi.
 
Comments reserved
 
Ukioa mke angalia vipaumbele vyako mwenyewe.
Kuna watu wanasema waif lazima awe presentable mbele za watu, mwingine chura Mimi binafsi Nina flat screen yangu, inachakarika kuliko nyuki.
Waliooa wake wenye master's degrees na PhD Sasa hivi wanajuta, wanakunywa pombe sio kwamba wanapenda pombe.
 
Siyo kwamba anaakili sana ila we ndo kilaza zaidi yake mbona mambo uliyoandika ni ya kawaida tu ilitakiwa usishauriwe na mtu yeyote kama ubongo unafanya kazi
 
Nilichogundua wewe una wivu na hao wanaosimama nyuma ya rais.Ni mjinga pekee anayewasilisha mada Kwa mgongo wa mtu mwingine.pamoja na kwamba kazi za kuajiriwa zinakunyima uhuru lakini naamini wewe kwa fikra zako huwezi kulingana nao kimaisha na hao wanaosimama nyuma ya rais.maana wao wakienda nje wakikaa wiki wewe na biashara Yako ni mapato ya mwezi au miezi kadhaa.
 
Wewe na huyo mke wako ni wajinga wawili mlio kwenye penzi zito. Wote ni vipofu. Kimsingi huyo mkeo hana akili yoyote zaidi ya kuwa na inferiority complex kama vilaza wengine ambao hawakwenda shule. Kudharau kazi ya ADC wa Rais ni upumbavu usioelezeka. Nyumba ya 20m kwa Dar ni nyumba ya kimaskini. Na usikute hapo mlidunduliza na kujenga taratibu. Kumkataza mtoto kufanya anachopenda ni upuuzi mwingine. Mwanaume unatakiwa uwe miles nyingi sana kifikra kwa mkeo. Yeye akiwaza leo wewe uwe unawaza mwakani. Vinginevyo ataishia kukuvuruga. Usipojirekebisha utakuja na uzi mwingine wa kumlalamikia.
 
Wanawake hakika wana upeo kutushinda wanaume,
Kabla sijamaliza kusoma bandiko lako rekebisha kwanza hii kauli yako sema "mwanamke hakika ana upeo kunishinda mimi.." usitujumuishe wanaume wote isee.
 
Wamama zetu wengi hawajasoma na mpaka leo wanaongoza familia kwa weledi na fikra ndefu
Ingawa vijana wengi wanakataa ndoa ila kuna wanawake wana uwezo sana kifikra kama wakiamua kuendeleza familia
 
Mbona kawaida, maana wengi mama zetu hawakusoma vidato, waliishia STD 7 lak I wana akili na maono kuliko vibinti vyenye Master's na Degree 😢
 
Hongera kwa kuwa na mke bora kiongozi, Wengine wana mabumunda yanajua tu kuangalia mezani umeacha nini kila ukitoka, Kazi ni kukopakopa hela kwa wakopeshaji na Vikoba.
 
Hivyo ni gharama ya vyumba viwili. Usidharau shule kama vilaza akina Mbunge Msukuma
 
Nilikuwa natafuta comment kama ii ili nisirudie kuandika safi, mke mwenye maono mngekuwa na mali nyingi uo ni ushubwada anamiliki motivation speaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…