Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu
Mkuu kma hutojali njoo pm tuongee nikusaidie
 
Wote wachawi, katika uislam tunaamini majini hupanda Kwa watu waovu na washirikina.
We achana nao, waache warogane wauane wakuache upumzike.
Usiseme ivo wauane wakati msaada unaweza kupatikana m nimemwambia nitamsaidia kma hatojali wala sitanii
 
Wote wachawi, katika uislam tunaamini majini hupanda Kwa watu waovu na washirikina.
We achana nao, waache warogane wauane wakuache upumzike.
Mtu yeyote yule atakaekua na shida kama hizi m akinambia naweza msaidia wala si uongo ni ponyo haswaa
 
Hii kitu kama ni yakweli inaweka njia panda.


Je mkeo kwa miaka yote hiyo majina yanapambana mpaka majuzi????? Hiii


Je mama yetu ,miaka saba hakuona uchawi, mpaka majuzi hiii ????.



Mama yetu ni Mwanga , Mkeo ni MTU wa waganga sana.

Na nguvu zao zinashindana !!!.


Cha kufanya .... Wewe Jikite kwenye maombi ya kweli na yamoyoni., umlilie Bwana Yesu, Bwana wa Majeshi , Mfalme wa wafalme, Mungu wa Miungu.



Ukijiingiza kwenye mtego wa Waganga, au kuegemea mahali Fulani , WEWE MWENYEWE UTAKUFA.

MKEO ASIPOKUUA, MAMA YETU ATAKUUA.
 
Mama yako ni MCHAWI.

Wakati mkeo amepandisha mashetani na kutoboa siri, mama yako akawa ameshaona kwenye vioo vyake na antena zake za kichawi.

Ndio maama ulivyomfwata mama yako akaanza kukulaghai laghai. Ndivyo wachawi walivyo. Wadanganyifu.

Mkeo ana mizimu ya nyumbani kwao.

Nguvu za uchawi na za mizimu zinasigana.
 
Asslm Alykum Warahmatullah, Ndg Nikueleze Tu Kuwa Hapo Hakuna Mchawi Kati Ya Mkeo Na Mamayo Ila Wanachokitaka Masheitwani Ni Kuivunja Hiyo Ndoa Yakoh Mashetani Wanaichezea Akili Yakoh Ndg Kama Upo Dar Nicheki Nikusaidie Mashetani Walishaapa Kuwapoteza Wanaadamu Na Kuharibu Vizazi Vyao Nitafute Kwa Msaada Zaidi Wasijuchanganye Kichwa Hao Ni Vitu Vidogo Sana...Nawasilisha
Tamaa mbele...
 
Wanga huwa hawajulikani na sisi watu tusio wanga...labda uwe mtu wa dua/maombi sana au nawe uwe fundi fulani...
Mama yako uliyekaa nae miaka nenda rudi lazima ujue kama ni mchawi. Utasimangwa mtaani, shuleni au ukimkosea yeyote hasa utotoni utasikia "ndio maana mama yako mchawi". Mimi nilimjua mama wa kambo kwa kuishi nae mwaka tu, nikiwa mdogo. Baba alikuja kumjua miaka mitano baadae sasa unashindwaje wewe.

Kama majirani hawajawahi mzushia ile serious basi hayuko hivyo. Hata hicho "kipaji" utasikia majirani wanasema. Alafu dawa inakuaje tena, nacho ni kipaji?

Mkeo naye walewale team kupuliza usiku. Dawa asingekupa
 
Mke na mama yako wote washirikina,pengine wamekuwa wakishirikiana kufanya mengi kabla hawajakosana na kuanza kufichuana hadharani.
 
Back
Top Bottom