Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mimi Nina mtazamo tofauti na wa kwako;ambaye mchawi ni mamaake..Kwa nn?

Siku jamaa anaitwa na mdada wa kazi kuna tatizo nyumbani,alipofika mkewe Tyr alikuwa ameshapandisha majini na majini yakamwelezea hatari iliyopo mbele ya mke wake kwamba yanaelekea kushindwa vita, meanwhile mamaake anampigia simu sense kwao kuna tatizo kubwa na alipofika mama akaanza kujiliza na kutoa ushuhuda kwamba mkewe ni mchawi ..Alafu katumia defensive mechanism kwamba ooh unajua Mimi tangu nipo mtoto sijui bla bla,ili kumuwin jamaa

Moja ya Tabia ya wachawi ni unafiki,mchawi anaweza kukuloga usiku kucha asubuhi akaja kukujulia Hali,si umeona alichokifanya mama? Aliposhtukiwa deal limebumbuluka akamuwahi mtoto wake fasta kumstakia kwamba mkewe mchawi

Kinachotokea Kwa huyu jamaa ni kuuziwa ugomvi(vita) baina ya hawa wawili,mama na mke
Mama ana Tabia za ulozi na mke ana wadudu kichwani wanaomlinda,sasa kuna vita baina ya hawa wawili na anayeelekea kushinda ni mama,maana wadudu wa mama wamekili wanaelekea kulamba mchanga.Ni alert Kwa jamaa

Mkuu The MaskmaN hapo maamuzi ya Suleiman yanahitajika..Hekima ndy itaamua.Ila usimwamini mamaako pia,ni tishio Kwa mkeo
Km ni mmristo Sali na kufunga km kiislamu watakupa mwongozo
Man, this shit is correct. Mummy appears to be the problem and the wife appears to be the solution. I mean huyo mama is a witch and the wife is a witchdoctor. One has to neutralise the other
 
MAMA AKO NA MKEO WOTE NI WACHAWI, WAN WALIKUWA WANAJUANA KAMA NI WACHAWI ILA KUNA MAMBO WAMETOFAUTIANA TU NDIO MAANA WANA MWAGIANA SIRI ADHALANI, NA WEWE FANYA JUU CHINI UINGIE KWENYE MAMBO AYO ILI MUWE WATATU
Home Win & Both Team To Score [emoji2]
 
Kwa jins Mungu alivyoniumba ningewaita wote home na mzee na kama wazee wawili. Naweka kabisa bastola mezan. Kitakachofuata mzee kila mtu ataimba pambio aisee
 
Mimi Nina mtazamo tofauti na wa kwako;ambaye mchawi ni mamaake..Kwa nn?

Siku jamaa anaitwa na mdada wa kazi kuna tatizo nyumbani,alipofika mkewe Tyr alikuwa ameshapandisha majini na majini yakamwelezea hatari iliyopo mbele ya mke wake kwamba yanaelekea kushindwa vita, meanwhile mamaake anampigia simu sense kwao kuna tatizo kubwa na alipofika mama akaanza kujiliza na kutoa ushuhuda kwamba mkewe ni mchawi ..Alafu katumia defensive mechanism kwamba ooh unajua Mimi tangu nipo mtoto sijui bla bla,ili kumuwin jamaa

Moja ya Tabia ya wachawi ni unafiki,mchawi anaweza kukuloga usiku kucha asubuhi akaja kukujulia Hali,si umeona alichokifanya mama? Aliposhtukiwa deal limebumbuluka akamuwahi mtoto wake fasta kumstakia kwamba mkewe mchawi

Kinachotokea Kwa huyu jamaa ni kuuziwa ugomvi(vita) baina ya hawa wawili,mama na mke
Mama ana Tabia za ulozi na mke ana wadudu kichwani wanaomlinda,sasa kuna vita baina ya hawa wawili na anayeelekea kushinda ni mama,maana wadudu wa mama wamekili wanaelekea kulamba mchanga.Ni alert Kwa jamaa

Mkuu The MaskmaN hapo maamuzi ya Suleiman yanahitajika..Hekima ndy itaamua.Ila usimwamini mamaako pia,ni tishio Kwa mkeo
Km ni mmristo Sali na kufunga km kiislamu watakupa mwongozo
Sawa mkuu nimekupata vyema saana..sehemu panapo nipa utata kama bi mkubwa ni mchawi why nae anipe dawa ya kumuona mke wangu?..anajiamini nini kuwa nitamuona mke wangu?
 
Hii kitu kama ni yakweli inaweka njia panda.

Je mkeo kwa miaka yote hiyo majina yanapambana mpaka majuzi????? Hiii

Je mama yetu ,miaka saba hakuona uchawi, mpaka majuzi hiii ????.

Mama yetu ni Mwanga , Mkeo ni MTU wa waganga sana.

Na nguvu zao zinashindana !!!.

Cha kufanya .... Wewe Jikite kwenye maombi ya kweli na yamoyoni., umlilie Bwana Yesu, Bwana wa Majeshi , Mfalme wa wafalme, Mungu wa Miungu.

Ukijiingiza kwenye mtego wa Waganga, au kuegemea mahali Fulani , WEWE MWENYEWE UTAKUFA.

MKEO ASIPOKUUA, MAMA YETU ATAKUUA.
Okey mkuu nimekuelewa,je hawa wanao nifuata inbox ni waganga au watu wa maombi?..ningependa zaidi wangejipambanua maana hata mie nina hofu nikienda kiuganga nitaweza kupotea zaidi
 
Nami nimemaanisha kama ulivyoelewa mkuu...

Nimeuliza hivyo kwa kuwa mama yako kasema ana karama hiyo muda mrefu, na ninaamini endapo mkeo ni mchawi ina maana ulimuoa akiwa mchawi, hivyo mama yako angeliona hilo kabla na angekuepusha kuoa mchawi...

Unajua wachawi huwa wanajuana, na wakati mwingine huwa wanaungana kufanya mambo yao, na wakivurugani huwa ni mwendo wa kuwindana kutaka kuuana...
Wachawi huwa na Undugu kuliko Undugu wa Kuzaliwa, kuliko Bond ya Mama na mtoto....!
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu kakaa chini sebuleni kama analia afu mdada wa kazi kasimama. Nikamuuliza mdada kuna nini hapa akaniambia naona kama dada kapandisha mashetani!! Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mtu au mke wangu kapandisha mashetani, yakawa yanalia kwa sauti kubwa mnoo huku anajipiga piga chini.

Baada ya dakika 4 za kulia yakanitaka tuanze mazungumzo ila kwa sharti yule mdada wa kazi ama mie nimshike sikio mke wangu "kiti" kwa lugha yao. Kupitia mdomo wa mke wangu yale majini/mashetani yakasema kuwa yamekuwa yakipambana na MCHAWI kwa takribani mwaka sasa ila leo yameona vita inataka kuwashinda hivyo kiti "mke" anaweza akazidiwa na kupoteza maisha.

Nikawauliza huyo mchawi wamemuona wapi au anatokea wapi? Yule jini akaniambia je unatuamini? Au hautuamini? Kulingana na shauku ya kutaka kujua hilo tatizo linalotaka kuchukua maisha ya mke wangu ikanibidi niombe kutajiwa kwa kujibu "ndio nawaamini" Basi yule jini aliyepo kwa mkewe wangu akaniambia bila hata kupepesa macho kuwa "Mchawi ni bi fulani" ambaye ni mama yangu mzazi kabisaaa. Nilishtuka sana kiasi kwamba nilitamani hata kuchapa fimbo wote waliokuwepo palee ila nikajikaza na kuacha lipite. Basi hiyo siku ikapita.

Baada ya siku kama 3 nikapokea simu kutoka nyumbani kwa wazazi wangu, nikaenda bila kusita kufika tu baada ya mama kuniona akaangua kilio na kunikumbatia kwa huzuni. Ikabidi nimuulize mama kulikoni? Kuna tatizo? Au kuna msiba? Akasema hapana kuna jambo nimekuwa namuhadithia baba yako kila siku hivyo na wewe yakupasa kulijua leo. Nikamwambia sawa mama niambie...basi akaanza kusema "ujue mwanangu mie mama yako huwa nina karama kama sio bahati fulani kichwani mwangu toka nikiwa binti mdogo tu, nina uwezo wa kuona na kuzungumza na vitu/viumbe ambavyo wewe kwa jicho lako hilo la nyama huwezi kuona"....baada ya maelezo mengi tu ya historia na nguvu zake hizo ndipo mama bila kusita akasema "Mwanangu mkeo ni MCHAWI" kama utakubali sema nikupe dawa ambayo itakusaidia kumuona bila yeye kujua ili ikusaidie kusadiki haya ninayo yasema na badae uchukue hatua...

Basi nikarudi nyumbani nikiwa na mawazo mengi nisijue nini kinaendelea hapa katikati. Nikafika nyumbani ile kuingia tu mke akaanza kupiga kelele kama jogoo huku akinifuata kwa hasira na kuniomba nimpe nilichopewa na huko nilipotoka. Nikashtuka mnoo!!

Ikabidi niitoe ile dawa na kumkabidhi mke wangu, baada ya dakika 3 akaniambia sasa achana na hii dawa ngoja nikupe ya kwangu ili ushuhudie mama yako anachotufanyia usiku.

Nikamwambia kwa sasa hapana ngoja nifikirie then nitakuambia unipe...

Ndugu zangu nipo hapa Sea clif napata upepo nikitafakari nini kinaendelea kwenye familia yangu haswaa kwa watu ninaowapenda mnoo. Je yupi ni yupi?

Nipeni ufumbuzi.
Wote wanga sema wamezidiana kila mmoja anakuja pambana na mwenzake so dawa ya yeyote utakayotumia utamuona mwenzake...
 
Mkuu ukishindwa kulipatia hili ufumbuzi jiandae wewe kufa. Binafsi kwangu kauli ya Mama ni Final sinaga maswali mengi zaidi ya kutii
 
Naona Wachawi wawili wakipishana masrahi kama fisiemu
 
Back
Top Bottom