Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

MAMA AKO NA MKEO WOTE NI WACHAWI, WAN WALIKUWA WANAJUANA KAMA NI WACHAWI ILA KUNA MAMBO WAMETOFAUTIANA TU NDIO MAANA WANA MWAGIANA SIRI ADHALANI, NA WEWE FANYA JUU CHINI UINGIE KWENYE MAMBO AYO ILI MUWE WATATU
Ahahaaaaa....! Aingie wawe watatu. Na akiingia afanye juhudi awazidi nguvu upande huo
 
Mimi Nina mtazamo tofauti na wa kwako;ambaye mchawi ni mamaake..Kwa nn?

Siku jamaa anaitwa na mdada wa kazi kuna tatizo nyumbani,alipofika mkewe Tyr alikuwa ameshapandisha majini na majini yakamwelezea hatari iliyopo mbele ya mke wake kwamba yanaelekea kushindwa vita, meanwhile mamaake anampigia simu sense kwao kuna tatizo kubwa na alipofika mama akaanza kujiliza na kutoa ushuhuda kwamba mkewe ni mchawi ..Alafu katumia defensive mechanism kwamba ooh unajua Mimi tangu nipo mtoto sijui bla bla,ili kumuwin jamaa

Moja ya Tabia ya wachawi ni unafiki,mchawi anaweza kukuloga usiku kucha asubuhi akaja kukujulia Hali,si umeona alichokifanya mama? Aliposhtukiwa deal limebumbuluka akamuwahi mtoto wake fasta kumstakia kwamba mkewe mchawi

Kinachotokea Kwa huyu jamaa ni kuuziwa ugomvi(vita) baina ya hawa wawili,mama na mke
Mama ana Tabia za ulozi na mke ana wadudu kichwani wanaomlinda,sasa kuna vita baina ya hawa wawili na anayeelekea kushinda ni mama,maana wadudu wa mama wamekili wanaelekea kulamba mchanga.Ni alert Kwa jamaa

Mkuu The MaskmaN hapo maamuzi ya Suleiman yanahitajika..Hekima ndy itaamua.Ila usimwamini mamaako pia,ni tishio Kwa mkeo
Km ni mmristo Sali na kufunga km kiislamu watakupa mwongozo
Kama nimekuelewa hivi.
 
Asslm Alykum Warahmatullah, Ndg Nikueleze Tu Kuwa Hapo Hakuna Mchawi Kati Ya Mkeo Na Mamayo Ila Wanachokitaka Masheitwani Ni Kuivunja Hiyo Ndoa Yakoh Mashetani Wanaichezea Akili Yakoh Ndg Kama Upo Dar Nicheki Nikusaidie Mashetani Walishaapa Kuwapoteza Wanaadamu Na Kuharibu Vizazi Vyao Nitafute Kwa Msaada Zaidi Wasijuchanganye Kichwa Hao Ni Vitu Vidogo Sana...Nawasilisha
Tayari ameingia anga
 
yni uyo jini wa mkeo kwanza kaleta uchonganishi kukwambia mama ako ni mchawi ndo yalivo ayo majini kazi yao ni kufitinisha wala usiwaamini
Umegeuka tena?. Au ndio msaada uliosema?.

Mbona alivyofika tu kwa mama,tofauti na siku zingine,leo alimkumbatia kabisa,akamwambia mkeo mchawi na mengine mengine. Kwa tabia aliyoionyesha mama,yeye ndio mwanga
 
Kama stori yako ni ya kweli, hapo wote wachawi hao...

Mama yako kakiri kuwa na 'karama ya kuona' watu wabaya, halafu kakupa nawe dawa ili uweze ona mauzazuza ya mkeo, kuwa na karama haina maana unakuwa na uwezo wa kutengeneza dawa...kama anatengeneza dawa huyo ni fundi tayari

Pia kwa mkeo ni wale wale tu, ana uchawi wa maruhani, na kitendo cha yeye kukupa dawa ina maana na yeye ni fundi...

Nina swali moja, kama mama yako ana karama ya kuona mauzauza, iweje hakuona kabla mwanamke uliyenaye hajawa mkeo?
Umewaza kama mimi nilivyokuwa nawaza
 
Hao wana misunderstanding zao binafsi, wametumia neno uchawi kama njia ya ku articulate feelings zao.

Ningekuwa ni mimi, hapo uliposema unapata upepo ndio ningeitumia kuwa alika kila mmoja bila wao kujua kua watakutana halafu wanatoa dukuduku zao na ku press reset button kumaliza fitna zao

Hakuna uchawi
 
Mwanaume hutakiwi kukimbia changamoto, hilo.ni jambo dogo sana jamaa akituliza akili vizuri kila kitu kinakaa sawa.
Ningekuwa mimi ningekata mawasiliano nao na kwenda kuishi mbali kabisa wasinijue.
Siwezi nikakaa chini kangaika na maujinga yao
 
Umegeuka tena?. Au ndio msaada uliosema?.

Mbona alivyofika tu kwa mama,tofauti na siku zingine,leo alimkumbatia kabisa,akamwambia mkeo mchawi na mengine mengine. Kwa tabia aliyoionyesha mama,yeye ndio mwanga
Sipendi kulumbana kwaio kma hujaelewa bora uniulize
 
Back
Top Bottom