Mke wangu ni msumbufu, mwenye ulimi mkali na mkorofi

Fanya ishu zako, hakikisha unalea watoto...
 
Aisee pole Sana Mkuu, wanaume tunateseka Sana.

Mkeo ana chanzo chake cha kupatia hela ama mnapokuwa 6by6 humseketui fresh?
 
Kwa mambo kama haya yatafanya wengi waogope kuingia kwenye ndoa.
 
Polee sana. Mimi huwa nasema kuingia kwenye ndoa ukitegemea mtu atabadilika ni uongo. Mpende mtu ukijua kabisa utaweza himili mapungufu yake. Yapo yanayoweza badilika lakini sio tabia ya mtu. Hata iwe miaka 20 ile tabia bado atakuwa nayo tu.

Cha kukushauri tu. Jenga ukaribu na watoto halauf andaa talaka. Najua talaka ni mada kubwa na pana ila furaha yako kwanza then ya watoto. Ile talaka itakupa wewe nguvu ya kufanya yaliyo na afya kwako kiakili na kiujumla
 
Habar za saa hizi jameni...

Nimeoa mke miaka 6 iloyopita.. Nilidhani mambo yatabadilika ila Tabia ilizidi kuwa sugu kila kukicha... Tabia yenyewe anaulimi mkali saana... She don't have respect in brief.
Pole sana mkuu, binafsi nimeshindwana na hao watu na nimeamua kulea watoto wangu 3 peke yangu sema wangu ni wakubwa.
Bwana wanawake wanaopata bahati ya kuolewa huwa wasumbufu sana sijui ni kwanini, kila ukijaribu kuwa mpole anazidi kukupanda kichwani, ukimuomba msamaha ndio balaa kabisa anakuchukulia dhaifu. Kero zinakuwa nyingi ndani mpaka unahisi muda wowote unaweza kufa kwa kiharusi.

Mimi watoto wangu siwezi warudisha kijiji nakomaanao hapa mjini coz ndio furaha yangu, nipo kwaajili yao kila ninachopambania ni kwaajili yao so siwezi wapoteza mpaka kieleweke.
 
Mbona umesema kwamba ulijua,ila ulidhani atabadilika?
Kwenye uchumba mambo yalikua tofauti sana kila mtuu alinipongeza kwa kweli hata wazazi pia... Mambo yali badilika alipofika ndani... Hapo ndipo nikaona nisicukuwi uamuzi haraka nikizani atabadilika..
 
Ni ngumu sana hakika, Nini kinapaswa kifanyike sasa kaka mkubwa maana hali inazidi kuwa mbaya kila uchwao..!
 
Duuuh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…