Mke wangu vitendo ulivyomfanyia Mama yangu sitosahau kamwe

Mi nlijua mke wako alimnyoosha bi mkubwa??kumbe alimfanyia mambo mpwito mpwito!!!kwa nukta hiyo itoshe kusema mke wako ameupiga mwingi hadi umemwagika.
 
Mi nlijua mke wako alimnyoosha bi mkubwa??kumbe alimfanyia mambo mpwito mpwito!!!kwa nukta hiyo itoshe kusema mke wako ameupiga mwingi hadi umemwagika.
Aliucharaza mpaka basi yaani
 
Kwa hiyo mama akiwa kijijin umeshindwa kumtengenezea mazingira mazuri kama mashuka,chakula
Kila jambo ni hatua kwa hatua kadiri Mungu anavyotujalia. Huo ni mwanzo tu
 
Yes sio kila siku vilio tuu, threads kama hizi ndio mapigano dhidi ya wazee wa Kataa ndoa.
Tumewapiga 3 bilaπŸ˜…πŸ˜….

Wasione tumenyamaza wakajua hatuna cha kushuhudia.

Ndoa tamu bwana asikwambie mtu.
 
Mwenzio huyu hapa

Ili uolewe sasa. Maana mwanaume kama huwezi kuoa mwisho wa siku utaolewa wewe
 
Hongera kwa Mkeo lakini hongera zaidi ziende kwa Mama, hakika Mama yako ana Utu wa kupenda kukirimiwa na akakubali, kuna wamama wengine mtihani akiona maisha mazuri anaanza kuonesha wivu na choyo kwa mkeo yan ataona kama mkeo anafaidi maisha, ataanza kufanya visa, atakumbuka huko kijijini kuna binti wa shoga ake yupo tu atataka umuoe akiamini atafaidika zaidi yeye na shoga ake,

Atajisononesha, atakua mkali, hatothamini kila anachofanyiwa na mkeo, vurugu zitaanza, utaanza kumuona mkeo ndie mkorofi na kuhisi ana roho mbaya kwa mzazi wako, mkeo atachoka kuvumilia, ugomvi utazidi kua mkubwa hatimae mnaachana,

Utaletewa huyo mdada wa kijijini, baada ya kukaa kwa miezi mitatu watakuja kutembea mama ako na shoga ake ambaye wewe ni mkweo, mtu na mwanae wataanza kumnyanyasa mama ako, kwa aibu hatokwambia atavumilia, ataanza kukonda, utahisi mama anaumwa, mkeo atakwambia amemiss kwake, utamsafirisha yeye lakini shoga ake/mama mkwe wako atabaki, mkeo ataanza kukupanda kichwani, utakua unarudi usiku hawajapika lakini yeye na mama ake wamekula, ukihoji utaambulia maneno ya kashfa, utamkumbuka mke wako wa kwanza utaona kuna tofauti, utamtafuta atakujibu alishaolewa, utampigia simu mama yako na kulalamika, atakufungukia na kukuomba msamaha lilikua kosa lake, mkeo alimtendea mazuri lakini yeye hakuridhika, utakasirika, utamfukuza mkeo na mama yake kwako, utaishi maisha ya majuto, utaichukia ndoa na wanawake.
 
Inauma pale unapojua ushachelewa tayari.
 
Mbona Dingi nae hakuja sasa?
 
Hongera...Ndoa ina muda gani mpaka sasa mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…