Mke wangu vitendo ulivyomfanyia Mama yangu sitosahau kamwe

Mke wangu vitendo ulivyomfanyia Mama yangu sitosahau kamwe

Hii story nimeisoma kama story zingine tu kama za somebody iddi makengo sijui iddi matengo.
Iddi makengo anadanganya wanawake sana nawaonea huruma wanaomfwata ushauri wake anatunga stori watu wanaamin kwa sisi high intelligent people na charismatic kama gentamycin tunaelewa wats going on
 
Ilikuwa ni mwishoni mwa Mwaka jana 2022.

Basi kutokana na kazi nyingi za kijamii huku ikizingatiwa kuwa Taifa tulikuwa bize ktk kujenga nchi, huku wengine tukihitajika zaidi katika maswala ya kitaifa ikiwemo swala la maridhiano, katiba Mpya, mfumuko wa bei ya bidhaa, kuifungua nchi na harakati za hapa na pale.

Basi nikamuomba msamaha Mama yangu mzazi kuwa kutokana na muda kubana basi nilipaswa niende mimi kumtembelea kijijini huko mkoani. Na kwakua nina muda mrefu sijaenda nikasema basi nimtumie nauli aweze kuja kwangu Mjini tuonane na kupiga stori za hapa na pale.

Basi mipango ikaanza kuwekwa sawa nikamjulisha Mke wangu kuwa Mama yangu mzazi atakuja muda ukifika kadiri atakavyoona yeye ataniambia tarehe na siku.

Mke wangu huyu akaniambia basi Nashukuru kwa taarifa hiyo na nipe kazi hiyo ni wajibu wangu niachie mimi nilishughulikie.

Nikasema sawa Mke wangu. Nilimwamini atalisimamia vema. Huwa haniangushi ktk mambo mengi makubwa na mazito.

Mambo ya ajabu aliyotenda dhidi ya Mama yangu yalikuwa ni haya.

1. Alisimamia safari yake kutoka kijijini hadi kufika mjini nilipo, safari ya takribani masaa 36. Huku mimi nikiwa bize aliweza kuwasiliana naye muda wote kuhakikisha anafika salama. Hapo alimtumia pesa zaidi kama pocket money na dharura mbali mbali asipate taabu njiani.

2. Mama yangu alionekana ni mtu wa furaha muda woote akiwa kwangu. Niliporudi usiku alipenda sana lazima tuonane na kusalimiana.

3. Mama yangu alinambia tangu amefika kwangu ameanza kunenepa na kusahau shida na tabu za tangu awali tukiwa kijijini akihangaika kutulea kwa shida


4. Mama yangu alinambia hajawahi kutembea sehemu yoyote na kupewa heshima kama aliyopewa akiwa nyumbani kwangu.

6. Mama yangu alinambia tangu yeye anakuwa na hadi sasa amekuwa mzee hajawahi kulalia mashuka meupe pee, mashuka safi ya kung'ara ambayo hubadilishwa kila siku na kuwekwa mengine.
Anaongeza kwa kusema alikuwa akitandikiwa Net ya Mbu safi kuhakikisha analala usingizi Fofofo. Usingizi usio na mawaaa!.

5. Mama yangu alinambia Mke wangu alikuwa akimpikia siku zote alizokuwepo nyumbani miezi mitatu asubuhi, Supu, chapati, juice, au maandazi na vingine mbali mbali.

7. Mama yangu alinambia Mke wangu akiwa anapika chakula akiwa bado anachemsha mboga let say Kuku au nyama au Samaki basi alikuwa anampakulia kidogo kwenye kibakuli aonje huku msosi wa nguvu ukiwa unaandaliwa.

Mama yangu alinisimulia haya tukiwa tumekaa kwenye kochi huku akicheka machozi ya furaha yakimtiririka, tukigongeshana mikono ya furahaa " Mwanagu rastaman mke wako amenirudisha utotoni" napakuliwa kibakuli cha supu nionje kabla hakijamaliziwa kupikwa, mbarikiwe sana na nyie watoto wenu wawafadhili kama mlivyonifanyia.

8. Jambo lingine Mama aliniambia alitendewa ni mavazi, baada ya kufika tu mjini alipumzika kama siku tatu akapelekwa shopping na kununuliwa mavazi mapya yote muhimu ya kike na ya Kama Mama.

9. Wakati tukiendelea mama alizidi kunifanulia kuwa ameweza kupata marafiki wapya mjini kwani hata inapotokea Harusi au Send off za Mashoga zake mke wangu basi Mke wangu alikuwa akimvalisha na kwenda naye kula bata huko za kike.

Mam yangu aliondoka kurudi nyumbani akiwa na zawadi kede kede na huku akijitazama miguu na mikono jinsi alivyo nawili na kuwa softi. Mama alinitania akisema mwanangu narudi nyumbani Baba yako ataniona Mpyaaa!! 😅😅😅

Hivi ndivyo Mke wangu alivyoniwakilisha kuhakikisha Mama yangu anapata huduma Bora za kifamilia na kukirimiwa kama Mgeni Rasmi kipindi chote ambacho mimi nilikuwa bize na kazi zingine.

Sijutii kuwa katika Ndoa ya namna hii.

Ukiwa na Mke mwamini mpe nafasi ajitanue. Usimwingilie fanya yako afanye yake utafurahi mwenyewe.
Mi nasikitika kutokuwepo kwa baba mkwe baba mzazi wa mkeo
 
Saafi sana kwa mkeo amefundwa akufundika,, sema hapo inabidi siku mama Yake akija usiwe mchoyo.
 
Hongera mama na wife wako wote si wachoyo,
Mana angekua mama mwingine hata asingekupa huo mrejesho na ndo kwanza angesema mkeo anamnyanyasa,
 
Hongera mama na wife wako wote si wachoyo,
Mana angekua mama mwingine hata asingekupa huo mrejesho na ndo kwanza angesema mkeo anamnyanyasa,
Mama yangu alikuwa mwazi na mimi niliridhika kuwa mama amekuwa mtu wa furaha kipindi chote
 
Ni katika wale wa " kataa ndoa" wanaozaa nje na kutelekeza watoto
Hivi unajua katika makuzi na malezi tunasema fainali uzeeni baba akizeeka hathaminiwi tena, mama chap anakimbilia kwa wanawe na kuanza kumkandia msure ambae katika ujana wake alihakikisha watoto wanasoma na kupata mahitaji muhimu
 
Hivi unajua katika makuzi na malezi tunasema fainali uzeeni baba akizeeka hathaminiwi tena, mama chap anakimbilia kwa wanawe na kuanza kumkandia msure ambae katika ujana wake alihakikisha watoto wanasoma na kupata mahitaji muhimu
Ni kweli mkuu lakini sio kwa hawa " wakataa Ndoa"
 
Iddi makengo anadanganya wanawake sana nawaonea huruma wanaomfwata ushauri wake anatunga stori watu wanaamin kwa sisi high intelligent people na charismatic kama gentamycin tunaelewa wats going on
Acheni kujidanganya.
 
Hongera kwa kuwa na mke mwema na mama mwenye kurejesha fadhila
 
Nakiri kusema Kwa furaha hio ya mama utabarikiwa maradufu
Nilipoona tittle ya thread nikajua ni mambo ya kutisha atakua amefanya kumbe jambo la heri
Huyu ni mwandishi mzuri, kichwa Cha habari kinavutia kujua yaliyomo ndani.
 
Back
Top Bottom