Mke wangu wa ndoa kapewa Mimba na mtu mwingine

Mke wangu wa ndoa kapewa Mimba na mtu mwingine

Kwa scenario hii hata Rc wanavunja hii ndoa unless hutaki ivunjwe,uamuzi ni wako
 
King'asti nachoomba ushauri je naweza oa kwa ndoa tena kwa hyo scenario


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Huyu Mwanaume Anatufanya Sisi Watoto!eti Sikupewa Likizo Miaka Mitatu Mara Oooh Sikukutana Na Mke Wangu Miaka Kadhaa,yaani Unataka Kusema Na Mkeo Nae Hakupewa Likizo Pia?na Je Huyo Bosi Asiyekupa Ruksa Kwenda Kwa Mkeo Yupo?mimi Nahisi Huko Mkoani Ulipata Demu Mpya Ukasahau Mkeo Dar,nae Akakuchukia,matokeo Yake Wote Mkaangukia Pua Ktk Mahusiano Yenu Ya Nje!ww Utakuwa Umeachwa Na Unapoachwa Unakuta Kurudi Kwa Mke Hakufai Kashajazwa Mimba!kifupi Hapa Hakuna Mke Wala Hakuna Mume!wote Hovyooooo!
 
Nadhan ww ni mmoja kati ya ambao manfanya jamii forum isiwe jukwaa la watu wanao fikir
Unachosha mkubwa...hii kitu wala si ya kuleta JF..kila kitu kipo so open like vazi la kahaba then huna macho ya kuona...!!
Hata ushauri unaoutaka hautakusaidia chochote kama primarily wewe mwenyewe hujitambui!!
 
Piga chini huyo mzinzi!! Ushauri tu kwa akina mama waliolewa au wanawake walio na commited relationship!! Ni kwamba hawara anakupenda ukiwa kama ulivyo kwa kuwa anajua kuna mwanaume anakupa msaada au vinginevyo!! Siku ukiachika kwa mumeo au ikitokea umepata mimba na ukikataa kuitoa jua ni mwishoa wa kukukimbia jumla!! Hapa mkeo ameshakimbiwa na sasa anatafuta pa kukimbilia na si mapenzi toka kwako!! Ila nashangaa kwa upuuzi huu bado unauliza ushauri!! It is straight forward hata kwa dini za kikristu mke huyo anapaswa talikiwa!!!
 
Pole sana kaka, kwanza ujue huyo mwanaume wake ameshampiga chini ndio maana anajifanya kukunyeyeke.
Wewe nenda kamuone aliyekufungisha ndoa kama unataka kufunga ndoa nyingine, huo ni uzinzi ambao ni sababu inayopelekea ndoa ya kikristo kuvunjika. Ameona kumbe upendo wa dhati unao wewe, ila yeye ni mwanamke ambaye hana msimamo na mzinzi mkubwa tena hafain katika jamii, unaweza kulea mtoto cos hana kosa, ila kwa style hiyo mnayoishi baada ya mwaka atakuwa na mimba nyingine kisha atajinyenyekeza kwako ili ulee mtoto wa watu kwa mara nyingine, halafu akikutana na bwana ake wanakucheeeka na kuchekaga.

Fanya uamuzi wa kiume, na hilo si kosa mbele za Mungu kwa kuwa huyo amezini, n i aibu ilioje kwa mwanaume aliyeoa kulea mimba ya mwenzake na kisha kuendelea na mwanamke huyo!! huyo lipo lililompata kwa huyo mwanaume, kama anaomba msamaha akuombe wewe, wachungaji kanisani na familia zote mbili!
 
sali salam maria mara saba,kisha mwambie Mungu asante kwa kujua Ukweli then usimtafute kabisa huyo mke endelea na shughuli zako
 
Yaani duh!kweli tunatofautiana!! kuna cha kuuliza mara mbili kweli hapo?...mwanamke hana matatizo ,ni wewe mwanaume una udhaifu ambao ndio anautumia......muda si mrefu atakuzalia mtoto wa pili , watatu nk
 
pole sana story yako kidogo ifanane na ya uncle wangu, yeye alianza na vikao na familia mbili yani ya mke na yake
Baada ya vikao hivyo akaandika barua kanisani kwao wakaa vikao kadhaa na. Wazee wa kanisa na padri baada ya hapo wakapata kibali cha kupeleka kesi mahakama ya usuluhishi kurasini baraza la maaskofu then hapo ndipo wakabatilisha ndoa ndio akaenda mahakamani ila unaitaji mda sana sababu yeye ametumia miaka miwili ndio amepata kibali cha kuoa tena.



Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Yaani daaah! Yaani diiih! Yaaani duuuh! Huyo mkeo kimeo hachana nae kama mimba kakuletea ya nje hata ngoma atakupa na zaidi utaletewa mpaka mtoto mchina huyo kicheche uliharakisha kuoa... Ndoa si mchezo ndoa sio lelemama mtu wa kuoa inabd umsome kitambo ndo ufanye maamuzi ya agano la maisha kumbuka ww ni mkristo kuwa hakuna kitakachowatenganisha zaidi ya kifo na ndo maana sasa unapata shida... Ila haina jinsi mpige chini amekuzalilisha sana anza kurasa mpya!!!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wana jamvi naomba msaada
wenu katika jambo hili;Mimi mwaka 2009 nilifunga ndoa na binti mmoja
ambae nilikutana nae kazin na baada ya kama miez kadhaa tuliamua kufunga
ndoa kanisani lakin wakati nafunga nae ndoa yeye alikuwa tayar kaacha
kaz katika shirika tulilokutana so baada ya kufunga ndoa maisha
yaliendelea lakin mie nikikaa mkoan yeye akikaa Dar kutokana na majukumu
ya kikazi mie nafanya mkoan yeye Dar kwan alipata kaz nae baada ya
kukaa mtaan muda flan.
Mahusiano yaliendelea vizur tu lakin nikaja gundua ya kwamba anachat
na mtu ambae tuliwah ishi nae mkoan na nilipoamua kumtafuata akasema
binti alimwambia hajaolewa,akakubali kuacha kuchat nae.Vitimbi vikawa
vingi sana hatak kuja tena mkoan kuniona mpaka mie niende Dar na kwa
bahat mbaya mie nilikosa likizo kwa miaka 3 mfululizo na nikawa kama
kuja Dar ni training ya cku mbil mpaka tatu nikawa nakutana na vituko
sana mara ninuniwe mara kahama nyumba wakati yy yupo pale pale,stand
kuja kunipokea hatak na wakat tuna gar la kutumia nyumban.
Mahusiano yakawa yanaenda kwa mazoea tu mwaka jana kuna mtu akanipigia
cm kunipongeza kwa ujauzito wa mke na nilipata shock ukitegemea nina
mwaka cjaonana nae kimwili kwan nikienda training fup mara nyingi
anasema yupo period,nikazima so kwa kukubali ile hongera nikaanza
upelelezi na wakati huo alikuwa anaweza akakaa hata wiki asipokee simu
yangu na akipokea da sio dharau hizo kwamba anitak.Kupitia dada ake
mmoja akakubali kuniambia ukwel wa jambo hilo kwamba ana mimba na wao
wamejua co yangu kumuuliza hawaezi nikawa na uhakika na jambo hilo
nikaamua kumwambia tuweke sawa kwan naamin kateleza na tuendelee na
maisha kama kawaida akasema hatak na niendelee na maisha yangu kama
kawaida japo nilimbembeleza sana
Mwez wa kwanza nikaamua kwenda Dar kwan nilipata ruhusa kama ya siku
9,ndugu zangu wakasema niende nikahakikishe kwa macho yangu na kwa
msaaada wa yule dada alinicholea mchoro muda ambao yupo nikaenda
nilimkuta na yy ndio alinifungulia mlango kwanza aliponiona kidogo
asifungue mlango ila akaamua baada ya dk kama tano akafungua nikawa na
aman sana kumwona na ile hali japo yeye alikosa raha kabisa nikajaribu
kumsocialise asijione mkosaji nikapiga stori baada ya dk kumi nikaaga
kuondoka kwan cku iliyofuata nilikuwa narud mkoan japo nilimwambia
ntaenda kesho yake na ndio nikathibitisha ya kwamba ana mimba
Baada ya kurud mkoan akawa amerudisha sana mapenz kama mwanzo simu za
mara kwa mara na msg sasa mie nami kuogopa acjepata matatizo wakat wa
uzaz nikawa namjal kama mie ndio mwenye mimba na akawa na aman kila ktu
akawa ananiambia kuhusu mimba hyo,Juz Mungu kasaidia kajifungua mtoto wa
kike nikaambiwa na mpaka sasa kila ktu maambiwa mtoto anasumbua hik
mara kile kwa kifup kaona kama mtoto wangu
Picha ya cku ya harus aliitoa sebulen muda sana lakin sasa nimeambiwa
kaiweka sebulen tena na anaonesha kukumbuka kuna mtu alimpenda,sasa wana
jamvi mie naomba ushauri wenu nafanyaje ktk suala hilo,mimba sio yangu
na je kama nikiamua kuwa na mtu mwingine je ntafunga nae ndoa kwan mie
ni mkristo?


ntampata wapi mwanaume mwenye mapenz ya dhati kama ww mie ee Mungu why kwenye miti hakuna wajenzi? endelea tuu kuvumilia kama unamoenda ila alichofanya huyo dada mie binafsi nakiona nikitendo cjha kigaidi mbayaaaaaaaaa
 
Wewe utakuwa kilaza, huyo mtoto ni wa kwako ,kitanda hakizai haramu kamfanyie shopping haraka..
 
Kama kuna sumu hatari duniani ni mapenzi. Mtoa uzi anampenda sana mkewe. Pamoja na kuzaa na mwingine yeye bado anampenda. Watoa ushauri mtambue hilo na mlizingatie ktk ushauri wenu. Hii fani mie naiogopa kidogo
 
Kitanda hakizai haramu, we tunza mimba nawewe upachike ya kwako.
 
Wana jamvi naomba msaada wenu katika jambo hili;Mimi mwaka 2009 nilifunga ndoa na binti mmoja ambae nilikutana nae kazin na baada ya kama miez kadhaa tuliamua kufunga ndoa kanisani lakin wakati nafunga nae ndoa yeye alikuwa tayar kaacha kaz katika shirika tulilokutana so baada ya kufunga ndoa maisha yaliendelea lakin mie nikikaa mkoan yeye akikaa Dar kutokana na majukumu ya kikazi mie nafanya mkoan yeye Dar kwan alipata kaz nae baada ya kukaa mtaan muda flan.
Mahusiano yaliendelea vizur tu lakin nikaja gundua ya kwamba anachat na mtu ambae tuliwah ishi nae mkoan na nilipoamua kumtafuata akasema binti alimwambia hajaolewa,akakubali kuacha kuchat nae.Vitimbi vikawa vingi sana hatak kuja tena mkoan kuniona mpaka mie niende Dar na kwa bahat mbaya mie nilikosa likizo kwa miaka 3 mfululizo na nikawa kama kuja Dar ni training ya cku mbil mpaka tatu nikawa nakutana na vituko sana mara ninuniwe mara kahama nyumba wakati yy yupo pale pale,stand kuja kunipokea hatak na wakat tuna gar la kutumia nyumban.
Mahusiano yakawa yanaenda kwa mazoea tu mwaka jana kuna mtu akanipigia cm kunipongeza kwa ujauzito wa mke na nilipata shock ukitegemea nina mwaka cjaonana nae kimwili kwan nikienda training fup mara nyingi anasema yupo period,nikazima so kwa kukubali ile hongera nikaanza upelelezi na wakati huo alikuwa anaweza akakaa hata wiki asipokee simu yangu na akipokea da sio dharau hizo kwamba anitak.Kupitia dada ake mmoja akakubali kuniambia ukwel wa jambo hilo kwamba ana mimba na wao wamejua co yangu kumuuliza hawaezi nikawa na uhakika na jambo hilo nikaamua kumwambia tuweke sawa kwan naamin kateleza na tuendelee na maisha kama kawaida akasema hatak na niendelee na maisha yangu kama kawaida japo nilimbembeleza sana
Mwez wa kwanza nikaamua kwenda Dar kwan nilipata ruhusa kama ya siku 9,ndugu zangu wakasema niende nikahakikishe kwa macho yangu na kwa msaaada wa yule dada alinicholea mchoro muda ambao yupo nikaenda nilimkuta na yy ndio alinifungulia mlango kwanza aliponiona kidogo asifungue mlango ila akaamua baada ya dk kama tano akafungua nikawa na aman sana kumwona na ile hali japo yeye alikosa raha kabisa nikajaribu kumsocialise asijione mkosaji nikapiga stori baada ya dk kumi nikaaga kuondoka kwan cku iliyofuata nilikuwa narud mkoan japo nilimwambia ntaenda kesho yake na ndio nikathibitisha ya kwamba ana mimba
Baada ya kurud mkoan akawa amerudisha sana mapenz kama mwanzo simu za mara kwa mara na msg sasa mie nami kuogopa acjepata matatizo wakat wa uzaz nikawa namjal kama mie ndio mwenye mimba na akawa na aman kila ktu akawa ananiambia kuhusu mimba hyo,Juz Mungu kasaidia kajifungua mtoto wa kike nikaambiwa na mpaka sasa kila ktu maambiwa mtoto anasumbua hik mara kile kwa kifup kaona kama mtoto wangu
Picha ya cku ya harus aliitoa sebulen muda sana lakin sasa nimeambiwa kaiweka sebulen tena na anaonesha kukumbuka kuna mtu alimpenda,sasa wana jamvi mie naomba ushauri wenu nafanyaje ktk suala hilo,mimba sio yangu na je kama nikiamua kuwa na mtu mwingine je ntafunga nae ndoa kwan mie ni mkristo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Kwa maelezo yako inaonyesha unampenda sana mkeo-good,mtu mwingine wa nini tena?kama umeweza kumvumilia katika yote hayo.....na una uhakika gani huyo utakayefunga naye ndoa naye hatakuwa na vituko zaidi ya huyu wa sasa.cha msingi na cha maana kwa sababu ameonyesha kujirudi endelea kuishi nae.ILA kuwa mwangalifu inawezekana huyo mkeo alikuwa si mwaminifu toka mkiwa marafiki hadi unamwoa NA SIO KWELI kwamba ameteleza na inawezekana akaendelea kukusaliti mbeleni.AKIRUDIA TENA UNARUHUSIWA KUMWACHA ASIJE AKAKATISHA UHAI WAKO KWA GONJWA HILI.
 
Sasa unatafuta mke au?si useme moja kwa moja tu mpaka utusimulie
Mtafute na wewe mke wake au demu wake mpe mimbaa
 
Back
Top Bottom