Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
#Taarifabilamipaka
Elizabeth Nalem mwenye umri wa miaka 41 ambaye ni afisa wa mji wa Makutano Pokot Magharibi nchini Kenya, amewashangaza wengi baada ya kutangaza kuwa amefunga ndoa na Roho Mtakatifu.
Harusi hiyo iliyoandaliwa kwenye hoteli ya Chelang’a mjini Makutano ilihudhuriwa na wapambe wa Bi harusi huyo na kuongozwa na Kasisi Albert Rumaita wa kanisa la Full Gospel.
Akiwa amepambwa kwa mavazi rasmi ya harusi mwanamke huyo mwenye watoto sita alikula kiapo cha kumpenda na kumtumikia huyo mumewe mpya (roho mtakatifu) maisha yake yote
Mumewe aliyefahamika kama Joshua Nalem alikuwa ni kati ya mashuhuda wa harusi hiyo alipoulizwa alisema haamini kama mkewe aliyeishi naye kwa miaka 20 angefanya tukio kama hilo.
“Nimeshangaa sana. Nilitoa mahari; ng’ombe 22 na mbuzi 15 nilipooa mke wangu. Lakini sasa anafunga ndoa na mume mwingine anayedai kuwa roho mtakatifu,” alisema bwana huyo.
Bi harusi mwenyewe amesema
ametumikia dunia tangu alipozaliwa. Lakini sasa roho mtakatifu amemuagiza amtumikie Mungu.
"Roho Mtakatifu alinituma kwa Pasta Rumaita ambaye alininunulia vazi la harusi, aliandaa hafla hii na akakodisha magari yaliyotuleta haba,” akasema Bi Nalem.
Elizabeth alikiri kuwa kabla ya kuandaa sherehe hiyo iliyotawaliwa na vigeregere na nderemo nyingi aliomba ruhusa kwa mumewe ambaye alikataa jambo hilo.