Mkeo ana bodaboda wake?

Mkeo ana bodaboda wake?

Nimekumbuka mbali kweli siku moja nimefika Mkoa fulani mpya mida ya saa tano Usiku nkatafuta bar nipozee Walau Koo, Ile sehemu nilikuwa n Rafiki yangu wa kike ambae tangu mchana nilimpanga kuwa ntashuka hapo nimsalimie na tupate dinner pamoja bahati mbaya bus ilichelewa sana ivo nkafika night kali saa tano, Nikapiga vyombo mpaka saa sita ivi then nkamcheki bibie kuwa natafuta Lodge nilale tutaonana kesho, Binti aligoma akadai nikalale kwake nisihangaike na Lodge sasa Vyombo vilikuwa vimepanda kichwani nikajiripua kwenda kwa uyo mdada, Basi cha kwanza demu akasema Ngoja nikuitie boda boda wangu akufate duh nkashikwa na machale kuwa uyu msela isije akanipeleka then akauza gemu nkafatwa usiku usiku nkamuliza kwako ni mbali demu akasema Yes akaforce uyo boda akaja mpaka pale bar nilipo, Jamaa alinipakia uku akiniuliza maswali mengi sana, Jamaa ni Bishoo bishoo mi nilikuwa nimekula pensi na Tshirt na Sendo simply nipo Simple tu uyo boda boda alihoji maswali mengi kweli mara huyu demu wako nkamwambia hapana rafiki tu akauliza sasa unaenda kulala kwake? Nkamuambi hapana ntasepa amenifikisha kwa demu jamaa hakungoja ata demu afungue geti wasalimiane yani alisepa haraka, Kesho kapigiwa simù aje anichukue hakupokea kabisa, Alinuna
 
Kuna bodaboda mmoja huku mtaani ni mbea hatari! Alikuwa na abiria wake Ana mdada amempangishia chumba mtaani! Bodaboda ndie alikuwa anatumiwa na jamaa kupeleka matumizi n.k! Bwana weee bodaboda c Kendamwambia mke wa jamaa full story kampeleka mpaka mpaka kwa huyo mchepuko! Story zmeenea mtaani nadhan saiv Hana wateja wengi maana ni mbeaaa[emoji2]
[emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji3][emoji3]huyo bodaboda mbea hvyooo!!
 
Kuna kipindi nilikuwa na boda mmoja hivi Sasa mi kikawaida huwa sipendi kumtreat mtu vibaya, lugha nzuri, samahani km nikimchukulia muda wake kunisubiri, salamu endapo tukikutana pahala nk, ikawa nikienda shopping nae nampatia chochote kwa ajili ya familia yake nk, mkewe akajifungua akanambia nikaenda msalimia na zawadi ya khanga na kitenge Sasa jamaa sijui akahisi anaweza kuboresha kutoka kuwa boda na mteja iwe mtu na hawara yake akawa anapiga simu ovyo ovyo kilichoniboa Ni simu zake za usiku ,aagrrrrrggh nilimpa onyo na karipio kali hakuwahi nitafuta tena, akafie mbele huko, mfyuuuuu

Ila sikuwahi kumuamini mtu baki yeyote kunishikia kadi ya ATM hata kwa robo saa tu ije kuwa kutoa hela!! Labda babe nae Ni kwa vile mzigo anauweka mwenyewe benki
Aisee naomba na Mimi nikuwekee mzigo bank
 
Tatizo la boda boda wanauza Sana gazeti,kulikua na manzi wangu mmoja akitia timu maskani,nilimuelekeza kwa boda boda Fulani awe anamleta ,akwa anamleta Sana,he si ndiyo na yeye akaingiza vocal kwa manzi wangu[emoji15][emoji15]bahati nzuri yule manzi akaniambia,Yule boda kaingiza vocal kwake,nilimfuata maskani kwa nilimmaindi kinoma[emoji34][emoji34] na kumpaka Sana.
Shortly,wanauza Sana magazeti,ukikaa maskani zao,Siri zoote za madem unazijua kwa urahisiiii[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji3047]
 
ukiona mke wa mtu anatoka na bodaboda basi ujee huyo ni tabia yake tangu utoto - si ajabu hata kabla hujamuoa alikuwa antoka na shamba boy wao... na ukiona mumeo anatoka na H/girl wenu basi ujue hiyo ni tabia yake, si ajabu hata kipindi hamjaoana alikuwa anakula H/girl wao ama wa mtaani.
Umeongea point
 
Yap hiyo nimeiona sana, unakuta demu kaja kwenye kijiwe cha bodaboda kasimama takriban lisaa lizima anamsubiria bodaboda wake.

Mi nikamuuliza kwani huyo jamaa huwa anakubebaga bure? Kwanini usichukue hizi za hapa uwahi kuliko kuendelea kumsubiria huyo huoni kua unazidi kuchelewa

Akasema "Aah nimemzoea tu naogopa kubadilisha bodaboda mwingine naona anaweza niangusha maana huyu nimemzoea hakimbizi sana"
Hakimbizi sambusa yake sanaa
 
Honestly hata Mimi kuna dogo ametokea kuwa Boda sahihi sana kwangu, naeza mpatia pesa hata Mil 10 apeleke mahali na zinafika salama. Hata nikiwa na safari ya haraka inayohitaji Boda huwa nakuwa at peace kupanda Boda boda yake kuliko boda zingine.

Na huyu Dogo nimejuana naye kupitia kwa wife. [emoji28][emoji28]
 
Sentensi ya mwisho [emoji16][emoji1787][emoji1787]
 
Ukisikia mama au dada anakwambia ngoja nitamtuma 'bodaboda wangu' basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake kweli kweli.

Ninamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM. Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300,000, nikamwambia makato upande wako. Akaniambia basi acha 'namtuma bodaboda wangu'.

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe. Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama wana deal na vidume. Hawataki kupotezewa muda na mahesabu ya gharama wanakuwa makini but kwa wadada watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo.

Achilia mbali wale boda wanaokunywa na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo.

Nawauliza Wana JF, mkeo ana bodaboda wake?
Ni kweli hawa boda boda wanasaidia sana mfano hapa mimi wife ana boda wake ambaye hata kama sipo huwa anakuja nyumbani anamsaidia mpaka wife kufagia uwanja nk.
Pia huwa ndo anampeleka kwenye vikao vya vikoba, misiba, harusi nk.
Hata juzi mke wangu alienda kwenye sherehe usiku akarudi mida ya saa sita usiku aliletwa na boda wake.
Huwa sina mawazo hata nikiwa safari najua huyo boda anamsaidia wife mambo mengi
 
Ukisikia mama au dada anakwambia ngoja nitamtuma 'bodaboda wangu' basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake kweli kweli.

Ninamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM. Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300,000, nikamwambia makato upande wako. Akaniambia basi acha 'namtuma bodaboda wangu'.

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe. Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama wana deal na vidume. Hawataki kupotezewa muda na mahesabu ya gharama wanakuwa makini but kwa wadada watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo.

Achilia mbali wale boda wanaokunywa na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo.

Nawauliza Wana JF, mkeo ana bodaboda wake?
Consider this,"Freedom of choice and liberty"
 
Back
Top Bottom