Bird Watcher
JF-Expert Member
- Aug 19, 2013
- 3,151
- 6,261
Nimekumbuka mbali kweli siku moja nimefika Mkoa fulani mpya mida ya saa tano Usiku nkatafuta bar nipozee Walau Koo, Ile sehemu nilikuwa n Rafiki yangu wa kike ambae tangu mchana nilimpanga kuwa ntashuka hapo nimsalimie na tupate dinner pamoja bahati mbaya bus ilichelewa sana ivo nkafika night kali saa tano, Nikapiga vyombo mpaka saa sita ivi then nkamcheki bibie kuwa natafuta Lodge nilale tutaonana kesho, Binti aligoma akadai nikalale kwake nisihangaike na Lodge sasa Vyombo vilikuwa vimepanda kichwani nikajiripua kwenda kwa uyo mdada, Basi cha kwanza demu akasema Ngoja nikuitie boda boda wangu akufate duh nkashikwa na machale kuwa uyu msela isije akanipeleka then akauza gemu nkafatwa usiku usiku nkamuliza kwako ni mbali demu akasema Yes akaforce uyo boda akaja mpaka pale bar nilipo, Jamaa alinipakia uku akiniuliza maswali mengi sana, Jamaa ni Bishoo bishoo mi nilikuwa nimekula pensi na Tshirt na Sendo simply nipo Simple tu uyo boda boda alihoji maswali mengi kweli mara huyu demu wako nkamwambia hapana rafiki tu akauliza sasa unaenda kulala kwake? Nkamuambi hapana ntasepa amenifikisha kwa demu jamaa hakungoja ata demu afungue geti wasalimiane yani alisepa haraka, Kesho kapigiwa simù aje anichukue hakupokea kabisa, Alinuna