Mkeo ana bodaboda wake?

Mkeo ana bodaboda wake?

Kwa mazingira yetu "bodaboda wako" ni muhimu tu kuwa nae. Kama wa kuliwa aliwe tu ila kuna mahitaji lazima umtume bodaboda.
 
Kuna jamaa kamnunulia mkewe gari mbili
Still mmama gari hatumii
Kazi kumtuma boda Tu..
Na akilewa usiku bar boda ndo anamfata
Jamaa yupo nje ya nchi
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukisikia mama au dada anakwambia ngoja nitamtuma 'bodaboda wangu' basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake kweli kweli.

Ninamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM. Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300,000, nikamwambia makato upande wako. Akaniambia basi acha 'namtuma bodaboda wangu'.

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe. Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama wana deal na vidume. Hawataki kupotezewa muda na mahesabu ya gharama wanakuwa makini but kwa wadada watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo.

Achilia mbali wale boda wanaokunywa na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo.

Nawauliza Wana JF, mkeo ana bodaboda wake?
Utasikia nina bodaboda wangu nakuja nae...
 

Attachments

  • VID-20210403-WA0025.mp4
    1.5 MB
Kuna bodaboda mmoja huku mtaani ni mbea hatari! Alikuwa na abiria wake Ana mdada amempangishia chumba mtaani! Bodaboda ndie alikuwa anatumiwa na jamaa kupeleka matumizi n.k! Bwana weee bodaboda c Kendamwambia mke wa jamaa full story kampeleka mpaka mpaka kwa huyo mchepuko! Story zmeenea mtaani nadhan saiv Hana wateja wengi maana ni mbeaaa[emoji2]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lol
 
Mkuu sababu haswa ya msingi ni hulka tu ya wamama, wadada kupenda kuwa na mtu wanayemuamini...

Kama kuna mengine zaidi ya hayo ni udhaifu tu wa kibinadamu..

Nje ya mada, hata sisi wanaume tuna barmaid wetu hao asipokuwepo bar vyombo havishuki

Au ukiwa maskani unajipata una kochi lako hilo au kiti chako hupati amani ukikaa pengine...
 
Ndugu Tafuta PESA wanawake hata malaika wamewashindwa
Nadhani Wanawake Hawajui Ni Nini Wanataka, Fikria Uwe Tajiri Watakusaliti Uwe Hauna Kipato Pia Utasalitiwa.. Kijana Wawatu Kutoka Ukingani Fredy Ngajiro Aka Fredy Vunjabei Kashalizwana Mobeto Hamisa, anabaki Tu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huu ndio ujinga wanaume huwa tunafanya kwa wanawake /wake zetu, unamnunuliaje mtu mmoja gari mbili wakati watu watano wanaweza kutumia gari moja ?? Kama sio uzumbukuku ni nini ??
huyo zoba nina amini anaweza kuwa na ndugu zake huko kwenye asili yao wana dhiki kama nini !!,

Yaani unajidanganya kumnunulia mwanamke magari mawili ukidhani ndio atakupenda saaana, umelogwa tu, wanawake hawa hawaelewagi hata wenyewe wanataka nini, utashangaa pamoja na magari hayo mawili aliyonunua bado mwanamke anaweza kufanya mambo ya hovyo ikiwemo uzinifu na hili bodaboda, hala wewe umekalisha nanihii zako kama bwege, kwani gari moja haimtoshi mtu kutembelea ??
Dah...mkuu...lakini kuna aina 6 za msingi za magari ya kutembelea....na bado kuna sehemu nyingine hakuna gari inayofika [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa kamnunulia mkewe gari mbili
Still mmama gari hatumii
Kazi kumtuma boda Tu..
Na akilewa usiku bar boda ndo anamfata
Jamaa yupo nje ya nchi
Lakini si haitakiwi kuendesha gari ukiwa umelewa???
 
Back
Top Bottom