Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Hapo mimi ndio nachoka kbsa mbona mtu akiambiwa na presha-low/hyper blood p. au Kisukari haogopi kivile?

Kwani pressure, kisukari etc vinatokana na uzinzi? Watu wengi wanapenda sana kazi za nje (ngono za wizi) ila nani anapenda kuitwa mzinzi/mwasherati?

Tatizo ni jinsi UKIMWI uliyokuwa mediatized.Kwa hiyo hulka hiyo ikajengwa kwenye mind za watu na kuuona UKIMWI ni ugonjwa wa aibu na wa ajabu.
Kuna magonjwa mengi tu hayana dawa ila mtu akiambiwa akafanye scanning ya kuangalia cancer wala haogopi,mwambie akapime HIV.

Kuna VCT moja niliwahi kutembelea, hata wagonjwa mahututi hawaangaliani usoni. Ni kama kila mtu anamshangaa mwenzake kwamba alikuwa kiwembe? Ukimwi tuusikie tu na kuuongelea kwenye hizi PC. Ni zaidi ya OSAMA!

Tuwaambie nini kwani ninyi simmepima involuntary??? isingekuwa hizo mimba je, mnge-volunteer???? Kigezo hicho mmeonekana mashujaa wa kupima.

Hapo kuna hoja. Ni wanawake wangapi wangependa kupima kama siyo kwa ajili ya mimba?

Kama serikali ikipitisha sera kuwa kila mgonjwa akifika hospital apimwe kila kitu ikiwa ni pamoja na VVU, watu watapima tu. Kuna nchi moja ya kusini mwa Afrika (nadhani ni Bots) wana hiyo sera na mambo ni mswano. Hakuna sababu ya kupima kwa ajili ya kujua tu bila mpango mkakati uliowazi na unaokubalika kwa wahusika.
 
DC,
Hili ni wazo zuri sema tu inabidi kuongeza budget ya afya ili kuboresha hsp zetu za serikali. Nyingi ya hizi hsp zina hali mbaya sana kuweza kuhimili mpango kama huu.
 
DC,
Hili ni wazo zuri sema tu inabidi kuongeza budget ya afya ili kuboresha hsp zetu za serikali. Nyingi ya hizi hsp zina hali mbaya sana kuweza kuhimili mpango kama huu.

Basi suala la kupima au la liachwe wazi ili mtu mwenyewe aamue. Pia wake zetu wafundishwe huko MCH kwamba wasilazimishe waume zao. Kwani mara nyingi inakuwa kama anatafutwa mtu wa kubebeshwa lawama.
 
Kama serikali ikipitisha sera kuwa kila mgonjwa akifika hospital apimwe kila kitu ikiwa ni pamoja na VVU, watu watapima tu. Kuna nchi moja ya kusini mwa Afrika (nadhani ni Bots) wana hiyo sera na mambo ni mswano. Hakuna sababu ya kupima kwa ajili ya kujua tu bila mpango mkakati uliowazi na unaokubalika kwa wahusika.
Wanaopitisha sera na sheria si wabunge!! labda isime hii iwe kwa watu wa kawida tuu isiwashirikishe hapo sheria itapitishwa!!
 
Kwani mara nyingi inakuwa kama anatafutwa mtu wa kubebeshwa lawama.

Hilo haswa ndio mimi naona kuwa ni tatizo. Karibu kila kitu ikija kwenye mambo ya mahusiano wa kulaumiwa ni mwanaume. Mwanaume hivi mwanaume vile....kila kukicha nyimbo ile ile tu na hakuna jipya. I guess labda kwa vile wanawake wana asili ya kulalama lalama ndio maana kila mara wanapenda kuwalaumu wanaume kwa kila baya litokealo kwenye mahusiano.
 
Wao wana tamko la Beijing imefika muda nasi tutoe Tamko; Chagueni Mji mie napendekeza Russia!
 
Mbu sweetie hebu jibu bana mie nisikukatishe tamu ati!

...no way mamie,nimekataa...🙂

yaani nitoe mbinu hadharani? acha tu, acha kabisa!
Sitaki kuwasaliti wanaume wenzangu mydear na ndivyo tulivyofundwa huko Jandoni enzi zile tunatafuta 'IQ'...

...😀
 
Hilo haswa ndio mimi naona kuwa ni tatizo. Karibu kila kitu ikija kwenye mambo ya mahusiano wa kulaumiwa ni mwanaume. Mwanaume hivi mwanaume vile....kila kukicha nyimbo ile ile tu na hakuna jipya. I guess labda kwa vile wanawake wana asili ya kulalama lalama ndio maana kila mara wanapenda kuwalaumu wanaume kwa kila baya litokealo kwenye mahusiano.

😀, i bet hata mama "Hawa" alimlaumu baba "Adamu" kwanini alikula lile tunda ilhali mwenyewe ndiye alimyemshawishi..
 
Mie nadhani jamii bado hija elimishwa vizuri au wamekataa kuelimika kuhusu umuhimu wa kupima afya yako kila baada mda fulani na jinsi gani inasaidia kupambana na magonjwa haya utakapo gundua mapema kama umeathirika.

Kuhusu sisi wanaume pia nadhani swala ni hilo hilo hapo juu kutojua umuhimu wa kupima hili kama ni muathirika utaweza kupambana nagonjw ahili mapema kabla alijatushambulia zaidi.

mimi binafsi nilipima 2006 mwezi wa nane na nashukuru mungu nimetokea mzima wa afya.nikapima tena 2008 mwezi wa nne majibu nayo yalikuwa mazuri nashukuru mungu.

kilichonifanya nipime ni kutaka kujua kwani nishajionea jinsi watu wanavyo taabika na gonjwa hili kwahio nimeona ni vizuri kutoa uoga na kupima hili niweze kukabiliana nalo lolote nitakalo likuta huku pia naendelea kujikinga kikamilifu.

kwa vile sipendi kutumia mpira niliamua kuwa na mpenzi mmoja na ambaye sasa hivi ni mke wanguna tuna mtoto mmoja.

nawashauri ndugu zangu humu muende kupima,ni uamuzi mgumu sana lakini ni wa maana sana kwani kama ni muathirika utaweza kuwahi mapema kuanza dawa na kufanikiwa kupambana na hili gonjwa.na kama huko negative basi utaendelea kujikinga zaidi na kujiepusha zaidi kwani utakuwa umepata unafuu ndani ya nafsi yako.

tusiache kutumia kinga wakuu,hili gonjwa watu wanalidharau lakini hesabu ya wanaopotea ni wengi mno .
 
Sioni sababu hata kidogo kwanini ukaamshe watu waliolala, ni bora waachwe walale mpaka siku watakapoamua kuamka wenyewe, yanini mtu ufe kwa wasiwasi? kingine cha kusikitisha baadhi ya mahopsitali yetu bomu, Miaka michache iliyopita mtakaokumbuka kuna jamaa alitaka kuoa kwakuwa agakhan ndo inajulikana ndo penyewe kaenda kupima jamaa kakutwa positive, mke mtarajiwa kusikia kachapa mwendo,jamaa hakuamini alipoenda muhimbili kapima kaonekana negative, kaenda tena sehemu nyingine negative, mbona alishia kuipeleka Aghakhan kwa pilato na kudai fidia kubwa kwanza kwa kusababishwa kukimbiwa na mchumba na usumbufu alioupata,

Nivema mwizi asikupe taarifa kwamba anakuja kukuibia unaweza kufa kabla hata hajaja, ni mtizamo tu
 
Hii dhana ya kwamba wanaume wengi hawataki/hawapendi kupima ukimwi inatoka wapi? Kuna takwimu zinazounga mkono dhana hii au ni kitu kinachodhaniwa tu?

Bila hata kurejea popote.... michango hapa tu inaongea volumes! Hapo bado hatuja nukuu ma researches kibao.
Wewe nini maoni/mtazamo wako? utasaidia kujenga hoja.
 
Halafu kati ya wanaume na wanawake, ni kundi lipi ambalo limedhurika zaidi na ukimwi? Kuna mwenye takwimu?
According to Tanzania latest stats -2007-08 Tanzania HIV/AIDS and Malaria Indicator Survey,katika kundi la wanawake wenye umri wa kati ya 15-49 - 6.6% walionekana HIV+ ambapo wanaume umri huo huo ni 4.6%. hata hivyo kiwango kimeshuka toka 7.7% ( wanawake) na 6.6 ( wanaume) mwaka 2003-2004.

Hii inatuambia nini? Wenye kuambukizwa zaidi ni wanawake kwa sababu ya maumbile yao na uwezo wao mdogo wa kufanya maamuzi katika mambo ya kujamiiana kama tunavyoona hapa kwenye discussions.Wanaume hutumia mabavu zaidi, hakuna negotiations na huweza kutishia amani.Mwanamke huona bora nikubali yaishe nibaki na amani.
 
😀, i bet hata mama "Hawa" alimlaumu baba "Adamu" kwanini alikula lile tunda ilhali mwenyewe ndiye alimyemshawishi..
To the contrary! Adam alimlaumu Hawa..na hapo akapata adhabu ya kutokutaka kuwajibika kwa makosa yake....
 
Mie nadhani jamii bado hija elimishwa vizuri au wamekataa kuelimika kuhusu umuhimu wa kupima afya yako kila baada mda fulani na jinsi gani inasaidia kupambana na magonjwa haya utakapo gundua mapema kama umeathirika.

Kuhusu sisi wanaume pia nadhani swala ni hilo hilo hapo juu kutojua umuhimu wa kupima hili kama ni muathirika utaweza kupambana nagonjw ahili mapema kabla alijatushambulia zaidi.

mimi binafsi nilipima 2006 mwezi wa nane na nashukuru mungu nimetokea mzima wa afya.nikapima tena 2008 mwezi wa nne majibu nayo yalikuwa mazuri nashukuru mungu.

kilichonifanya nipime ni kutaka kujua kwani nishajionea jinsi watu wanavyo taabika na gonjwa hili kwahio nimeona ni vizuri kutoa uoga na kupima hili niweze kukabiliana nalo lolote nitakalo likuta huku pia naendelea kujikinga kikamilifu.

kwa vile sipendi kutumia mpira niliamua kuwa na mpenzi mmoja na ambaye sasa hivi ni mke wanguna tuna mtoto mmoja.

nawashauri ndugu zangu humu muende kupima,ni uamuzi mgumu sana lakini ni wa maana sana kwani kama ni muathirika utaweza kuwahi mapema kuanza dawa na kufanikiwa kupambana na hili gonjwa.na kama huko negative basi utaendelea kujikinga zaidi na kujiepusha zaidi kwani utakuwa umepata unafuu ndani ya nafsi yako.

tusiache kutumia kinga wakuu,hili gonjwa watu wanalidharau lakini hesabu ya wanaopotea ni wengi mno .

Umemaliza kila kitu! Kama kuna ambaye bado hajapata darasa hapa..basi.
 
Bila hata kurejea popote.... michango hapa tu inaongea volumes! Hapo bado hatuja nukuu ma researches kibao.
Wewe nini maoni/mtazamo wako? utasaidia kujenga hoja.

Mtazamo wangu ni kwamba, tumeumbwa tofauti. Ni tofauti hii inayofanya wanawake kupimwa vipimo vya kila aina kuliko wanaume. Na katika kupima huko ndio hayo mengine kama HIV huonekana.

Wanawake kutokana na maumbile yao wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi kila mwaka (mambo ya pap smear nk). Wanaume hatuna hayo mambo. Tunapeta tu. Nyinyi kila mara inabidi mjishike shike matiti kuangalia viuvimbe vya kansa. Mna mambo mengi sana ya kiafya yanayosababisha muende kwa waganga kila mara.

Kwa hiyo siyo kwamba wanawake hujitolea tu kwa hiari yao mara mbili kwa mwaka kwa mfano, kwenda kupimwa strictly HIV. Hilo nakataa. Sitaki kabisa. Ni maumbile yenu yanayowafanya muende kupimwa pimwa mara kwa mara.

NB: Itakuwa vyema kama ukileta data zinazoonesha wanawake wasio waja wazito, wasio na matatizo mengine ya kiafya, wanaokwenda zahanati au hospitalini kwa nia na dhumuni moja tu la kupimwa virusi vya ukimwi ili kujua hali zao.
 
Back
Top Bottom