Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Hii mada dada mh ngoja waje wenyewe.
Mimi ningependa kujua mbinu za kuwashawishi kwenda kucheck afya zao.

MJ1, Hili Wanaume wengi linatusumbua sana si uongo. Mambo ya kwenda kuchokonolewa chokonolewa lete hiki lete kile ahhhhhh! yanatukera sana wengi wetu...mpaka pale tunapokuwa hoi bin taabani ndiyo tunaona umuhimu wa kufanya hivyo. Na hii tabia ni kwa Wanaume wote hata wa majuu.
 
3. Baba akimwambia maam twende ukapime mama atadai "huniamini?" even to some % kwa wanaume pia.

Mi naamini wewe Nguli hujawahi dumisha mila out lakini wife akikwambia twende tukapime utamwelewaje?
 
Mi naamini wewe Nguli hujawahi dumisha mila out lakini wife akikwambia twende tukapime utamwelewaje?

Sisubiri aniambie kila miezi 3 nafanyaga full body check up. Kwa vile na uzee nao unakaribia nacheki cholestral level, ini-bilirubin total na level, figo, moyo etc.
 
bht,

Sifichi kichwa, tatizo langu ni majibu ya kumwambia mtu ataishi kwa matumaini! Frankly speaking sielewi maana ya neno "kuishi kwa matumaini" - To me that sounds like "a death row"!

kwani hata hapo ulipo si unajua kuna siku (isiyojina) utakufa??
tayari sote tupo kwenye death row hapa.....
sasa uoga unatoka wapi tena nyie wababa
mkapime huko mjitambue, mjilinde na kuwalinda wengine pia....
 
yaani bubu hapo ni pachungu KULIKO VVU yenyewe!

mimi huwa nikiwaza kwamba nikirudisha namba kuna lijitu litamkanyaga mshiki wa x-pin LOL!NACHANGANYIKIWA!najikuta naagiza valuu ya nne ghafla
😀😀😀

Kuna mtandao mmoja wa Wamarekani weusi una umaarufu mkubwa hata kwa Watasha pia. Jamaa mmoja miaka ya nyuma akaanzisha swali kwa Wanaume je kama wanakufa na wanapewa ruhusa ya kuzikwa na kitu chochote kile cha chaguo lao wangechagua kuzikwa na nini? Nilishangaa sana namba kubwa kidogo walitaka wazikwe na wake zao kwa sababu tu njemba nyingine zisiendelee kufaidi uroda wao. Mhhhh! Hii inaonyesha kwamba Wanaume tuna wivu sana kuliko Wanawake.
 
MJ1, Hili Wanaume wengi linatusumbua sana si uongo. Mambo ya kwenda kuchokonolewa chokonolewa lete hiki lete kile ahhhhhh! yanatukera sana wengi wetu...mpaka pale tunapokuwa hoi bin taabani ndiyo tunaona umuhimu wa kufanya hivyo. Na hii tabia ni kwa Wanaume wote hata wa majuu.
BAK nimewaelewa na niliposoma post yako liknijia jambo hivi iwapo ikatokea wanawake tumepewa semina na ujuzi wa kucheck afya utakuwa tayari ucheckiwe na mkeo nyumbani? Au suala ni kujijua kama unao au la na si sehemu ya kupimia?
 
Sisubiri aniambie kila miezi 3 nafanyaga full body check up. Kwa vile na uzee nao unakaribia nacheki cholestral level, ini-bilirubin total na level, figo, moyo etc.

Kwa hiyo HIV test tu ndo huifanyi mkuu?
 
Mhhhh! Hii inaonyesha kwamba Wanaume tuna wivu sana kuliko Wanawake.

Hii mkuu ni dhahiri angalia kwenye mafumanizi nani mwenye machungu zaidi kati ya mwanamke akimfumania mwanaume yupo na nyumba ndogo au mwanaume akimfumania mwanamke na kaserengeti boy au jibaba nani atakae react zaidi?
 
Hii dhana ya kwamba wanaume wengi hawataki/hawapendi kupima ukimwi inatoka wapi? Kuna takwimu zinazounga mkono dhana hii au ni kitu kinachodhaniwa tu?
 
yani hapo kwenye kupima wanaume ndo tunaponyeshaga uanaume wetu kwani ukitaka kujua kama mzima unamforce wife au demu wako akapime yani unakuwa mkali kweli kiasi kwamba yule demu kama na yy ni mwoga kupima itabidi akapime tu kwa mkwara ila nawapongeza mademu kwa kuwa na ujasiri wa kupima kwani wanaume wengine wanapima kwa kuwapa mimba wake zao ili wakienda kupima waulize majibu yani we acha tu
 
BAK nimewaelewa na niliposoma post yako liknijia jambo hivi iwapo ikatokea wanawake tumepewa semina na ujuzi wa kucheck afya utakuwa tayari ucheckiwe na mkeo nyumbani? Au suala ni kujijua kama unao au la na si sehemu ya kupimia?

Mhhh! labda kama ni Dr. lakini sioni ubaya wowote wa Mama mwenye mali zake kuzicheck kama kila kitu kiko sawa.
 
Unacheck unamaana mkeo humwamini?
Mi ukweli na uwazi sicheck kabisa najiamini.

Hivi ukimwi unapatikana kwenye ngono tu? dispensari tunazopima pima malaria unaziamini sio? ni mfano tu iko mingi sana.
 
Hivi ukimwi unapatikana kwenye ngono tu? dispensari tunazopima pima malaria unaziamini sio? ni mfano tu iko mingi sana.

Wengi wanaamini maambukizi ya ukimwi 99% yanatokana na ngono tu haya maambukizi kwa njia nyingine jamii sasa imesha elimika na inajizuia sana hata wale mangariba wamesha elimika siku hizi.
 
Halafu kati ya wanaume na wanawake, ni kundi lipi ambalo limedhurika zaidi na ukimwi? Kuna mwenye takwimu?
 
1. Kwanini wanaume wengi hawataki kupima na kujua afya zao ( majority wanajua kabisa kuwa wanaishi maisha hatarishi ( risky life styles)
2.Mbinu gani zitumike kuwashawishi wanaume wasiotaka kujua afya zao kupima kwa hiari?
Suala la HIV na UKIMWI na kupima na kupokea majibu ni gumu sana kwa kweli,na ugumu unakuja pale mtu unapoambiawa kuwa wewe ni seropositive inamaanisha kuwa ni kifo tu,ingawa kila nafsi itaonja mauti lakini HIV ni suala zito sana.
Mbinu ya kutumika hapo ni kuwaandaa watu kisaikolojia pia kwa jinsi UKIMWI ULIPOKIJA NA jinsi ulivyosemewa kwenye media ni kama ugonjwa wa aibu,sasa basi ili kufuta hilo vichwani mwa watu ili waone UKIMWI ni kama labda magonjwa mengine yasiyokuwa na tiba mfano cancer na kadharika.
 
1. Mtu akiitwa polisi akaogopa ana tatizo(labda ni mhalifu wa aina fulani)
2. Hakuna kitu kama kuishi kwa matumaini ila kuna neno "courage" pia inategemea na aina ya maambukizi kwa mfano kwenye ajali au kuhudumia mgonjwa wa ukimwi. Pia kuna watu wamezaliwa na baraka za kuwa na furaha muda wote ataapate msiba anacheka, ni watu wachache sana haa duniani tuko hivyo,hata akikuta ana UKIMWI atatabasanu na huyu mtu ataishi muda mrefu sawa na ambaye hana ukimwi,tu kuna jina la kitaalamu la aina hii ya watu ila nimesau kidogo hapo, mfano hai hapa JF ni Chrispin.
3. Baba akimwambia maam twende ukapime mama atadai "huniamini?" even to some % kwa wanaume pia.
Umekamata SENKSI hapo. Nawaomba kinadada wausome huo mstari kwa makini. Narudia tena KWA MAKINI
 
Back
Top Bottom