Halafu jamani kuna kitu kimenijia akilini
Ukiangalia hili swala la HIV/AIDS limekuwa popularised sana sana, hasa kwa nchi za ulimwengu wa tatu
wakati huo huo, kuna magonjwa kama malaria, hayapewa attention kama ya ukimwi
naanza kuhoji nia na madhumuni ya kuwataka watu kupima kwa sana kama sio kwa madhumuni ya research zaidi, yaani kujua sasa wangapi wamekamatika na hence DAWA (ARVS) kiasi gani kinahitajika? mjue sio watu wote wangependa kuona kwamba hawapati faida...
Huenda makampuni haya ya dawa yangependa kupata faida hasa kwa kuuza ARVS kwa bei ghali kwa walioambukizwa tayari..lakini kweza kujua soko limekaaje, inabidi kufanya utafiri..hence hili la 'kulazimishana' kupima
manake sawa sio LAZIMA lakini the way linavopigiwa kelele, unajiuliza he mbona kama lazime, eti uwezi KUISHI KWA MATUMAINI?
Mimi bado analogy ya AK47 inahold, hasa ninapofikiria upande wa pili wa shilingi
Hivi niwaulize kuna mtu alishaangalia filamu ya "the Constant Gardener" au kusoma kitabu chake? mi nimefanya vyote na kusema kweli nilikuwa shocked!
haya ni mawazo yangu tu wajameni..sipingani na juhudi za kuutokomeza ukimwi...huenda utatokomea au kuwa kama ilivo gonno ay syphilis...