Mkuu hata Yesu alipohitaji usafiri aliletewa mwana punda na wengine wote wakatembea wakimshangilia kwa matawiACHA WIVU, ROHO MBAYA, NA AKILI MBOVU
Wewe ni mtu wa ajabu kumlinganisha Yesu na wezi wa Mali za umma na wabadhirifu. Punda alikua anatumiwa na watu maskini wakati huo kama ilivyo hakuna Tajiri anayepanda Punda au anayetumia punda badala ya Pick up . Kama hujui maandiko na theolojia acha kuhalalisha uovu Kwa kunukuu Biblia .Kwa muda mrefu mmetumia Biblia kujenga jamii na taasisi za watu waovu. Mnawajenga na kuwafariji wezi ,wahuni na waovu badala ya kuwaambia ukweli.
Yesu alikua ni mfalme wa wafalme na alikua Mwana wa Mungu na pia Masihi na Wayahudi walitegemea awe mfalme wao.
Wafalme enzi hizo walipanda Farasi wanyama wa Bei mbaya na waliotumiwa na wafalme na wakuu wa Jeshi kwenye Vita.
Hakuna maskini anayeweza kumiliki Farasi hata Leo. Farasi wanamilikiwa na matajiri mana mahitaji yao ni makubwa sana. Punda ni wanyama wa kimaskini.
Yesu Mwana wa Mungu aliye Hai na Masihi alionyesha mfano Kwa watawala wa Dunia. Alitumia Usafiri wa watu wa chini Kwa sababu walikua na maisha Duni kama ya kwake.
CCM mara nyingi mmekua mkitumia Biblia kinyume na kuwahadaa wananchi ili kuhalalisha ufisadi katika nchi hii.
Wewe kama sio mjukuu wa Shetani Ina maana unaona ni halali Mkurugenzi wa Halmashauri kutumia gari ya Milioni mia nne wakati Hospitali ya Wilaya Haina Ambulance ya kisasa .
Kama wewe sio mjukuu wa Shetani unawezaje kuunga mkono mtu anayechukua Milioni mia nne Kununua gari wakati watoto wake wanakaa chini shuleni.
Kuna mtu Gani kati ya uzao wenu wa nyoka ambaye akipewa Milioni mia nne wakati akiwa Hana pesa za Kununua chakula Cha watoto,nguo za watoto , nyumba inavuja na watoto wanalala chini hawana kitanda Wala godoro atazitumia Kununua Gari lakifahari la kutembelea ?Maskini mwanye akili na mwenye upendo na familia yake akipewa mil. 400 atazitumia kuondoa kwanza matatizo ya familia yake na kuanzisha miradi na Kisha Kununua safiri wa kawaida .
Nchi hii ni maskini Mikopo kila KUKICHA halafu unaweka bajeti ya Kununua magari ya kifahari?
Nakupa ukurugenzi na Gari isiyozidi Mili 120 kama ukitaka gari ya kifahari kanunue mwanyewe.
Huko Kuna wizi wa kimtandao ndio maana wananunua hayo magari. Enzi za Magufuli ukilinunua Leo kesho amekutumbua na unakaa benchi.
Raisi , Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na Mawaziri na wale wakuu wa Idara kama Wakuu wa Majeshi tuu ndio wanaostahili Kwa hadhi yao kutembelea magari ya kiwango Cha Juu na yenye usalama wa kutosha lakini sio Wakurugenzi wa Halmashauri wanashinda Saiti kusimamia shughuli za Halmashauri.
Tena walitakiwa wasiwe na gari zaidi ya Gari ya Ofisi inayorumiwa na watu wengine. Ni mifumo TU mibaya lakini hao watu ni watumishi TU kama walivyo wahasibu na mastawi jamii wengine.
Subirini 2025 ndio Mtajua kuwa Mungu anakusudi Gani na Watu aliowaweka Kwenye ardhi hii inayoitwa Tanzania yenye utajiri mkubwa lakini Watawala wasiojali watu wao wamewafanya watu wengi waishi maisha ya kumlilia Mungu Kwa umaskini mkubwa walio nao.
Hivi unafikiri Magufuli angefufuka Kwa mfano Kisha agombee 2025 unafikiri nani angeweza kushindana naye ?
Je, ni Kwa Nini watu wanasema wazi kuwa ufisadi umerudi wakati mama anafanya Kazi kubwa ?
Jibu ni kwamba matumizi yameongezeka sana. Watu wanapishana TU kwenye safari na vikao na makongamano na michezo ya kuvuta kamba badala ya kufanya kazi .
Fedha zinakwisha kabla ya kufanya kazi iliyokusudiwa. Watu Mfano Tasaf wanakaa vikao mwezi mzima na kulipana mamilioni eti kujadili namna ya kumtambua maskini na kaya maskini . Mwishowe wakishamtambua wanampa Elfu 20. !! Tulitegemea kuona Chawa wa kumuunga mkono Dr. Samia kuwataja wezi na mafisadi ili fedha anazohangaika kukopa zifanye kazi .