Mkuu pole sana kwa hali unayopitia, ni hatua katika mahusiano au ndoa. Binafsi sikushauri kupokea ushauri wenye lengo la kupanda mbegu hasi moyoni mwako yakuwa mwenzio sio muanimifu kwako.
Mkuu ni dhahiri umekuwa na mabadiliko substantially hasa ukiegemea kwenye ushabiki wa siasa na mahaba kwa wanasiasa, kiasi cha kukosa muda na mwenzio.
Nakukumbusha kuwa uchawa ni uraibu mbaya sana, kuliko hata Sembe mkuu!!! Nadhani kwa macho ya mwenzio anaona wewe sio yule Tlaahtlaah wa awali.
Rudi nyuma, reflect back, tafuta ulipo jikwaa sio ulipoangukia!!! Usiwekeze nguvu nyingi na muda mwingi kumbadilisha mwenzio maana siye aliyebadilika, wewe ndiye uliyebadilika, kwa hiyo jibadilishe wewe kwa ajili ya mustakabali wa Kaya yako.
Mkuu jipe likizo ya kujenga nyumba yako kwanza, usipoziba ufa huo utajenga ukuta. Siasa na mahaba kwa wanasiasa haviendi kokote, utavikuta tena vimenoga zaidi!!!
Kumalizia jivunie kuwa na mwanamke anayekutunzia heshima mbele za watu. Wewe Tlaahtlaah unafahamu fika shida ilipo, Fanyia kazi kwa umakini sababu zinazo mfanya asikupe ushirikiano.
Mkuu nakutakia maelewano, usuluhishi, mapatano chanya na upendo kwenye mahusiano/ndoa yako.