Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Kweli kabisa Kaka haujapigwa na maisha, kama umepigwa kisawasawa usiombee utatamani kuishi hata pangoni.[emoji16][emoji16]
 
Ila kuna sehemu unaweza kuidharau lakini watu wanafanikiwa hiyo hiyo sehemu..mfano wilaya ya Mwanga Kilimanjaro mi naiona ya hovyo lakini kuna vijana wanakuja na kutajirikia pale pale
 
DAR ES SALAAM DAR ES SALAAM DAR ES SALAAM
 
Naweza kuishi sehemu yoyote as long as ni sehemu ambayo inanifanya nipate mahitaji yangu muhimu.
 
Sumbawanga!
Kuzuri balaa, fikiria mie nimeishi 1979 to 1984 lkn bado napakumbuka Sana pale regional block, katandala, sumbawanga wenyeji, Regina Mundi, chanji, izia, bangwe, jangwani, mazwi nk. Shule yangu Jangwani Primary school, ndugu zangu walisoma sumbawanga primary school na Mama yetu alifundisha hapo. Nakumbuka kanisa katoliki kila jpili tulikuwa hatukosi enzi za Bab askofu Kalolo Msakila alikuwa jemadari haswa. Nakumbuka ule uwanja wa zamani pale karibu na dimba la Nelson Mandera tulikuwa tunaenda angalia mechi kati ya Ujenzi na RTC, Ujenzi wakipigwa bao. Mdau fika uuone uzuri wa Sumbawanga!
 
kweli iasee umeish.huyo msakila alikua yupo huko eenz za Ufipa rukwa
 
Pemba unaweza ishi na familia yako salama kabisa
Wakinga wa makete nao hawataki hata kusikia habari za kurudi makete[emoji28] ndo maana wanapambana ya hela yote. Kolodeness na vilima vya makete sio poa.
 
Wakinga wa makete nao hawataki hata kusikia habari za kurudi makete[emoji28] ndo maana wanapambana ya hela yote. Kolodeness na vilima vya makete sio poa.
Njombe kuna Hali ya hewa safi sio huko Dar sijui mnapapendea nn.
Mm kwangu nyanda za juu kusini yaani Iringa,Njombe,Mbeya,Songwe na bila kuisahau Swax ni sehemu poa sana kwa kuishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…