Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Lindi ndo mkoa utakaonishinda ila mikoa mingine yote kwangu fresh
Bora ya Lindi unaweza kwenda DSM na kurudi.Mziki huu hapa Kigoma huko barabara ya vumbi,umasikini mwingi mpaka kero.
 
Kuzuri balaa, fikiria mie nimeishi 1979 to 1984 lkn bado napakumbuka Sana pale regional block, katandala, sumbawanga wenyeji, Regina Mundi, chanji, izia, bangwe, jangwani, mazwi nk. Shule yangu Jangwani Primary school, ndugu zangu walisoma sumbawanga primary school na Mama yetu alifundisha hapo. Nakumbuka kanisa katoliki kila jpili tulikuwa hatukosi enzi za Bab askofu Kalolo Msakila alikuwa jemadari haswa. Nakumbuka ule uwanja wa zamani pale karibu na dimba la Nelson Mandera tulikuwa tunaenda angalia mechi kati ya Ujenzi na RTC, Ujenzi wakipigwa bao. Mdau fika uuone uzuri wa Sumbawanga!
Karibu tena Sumbawanga,usafiri umeimarika sana,waweza kwenda Mbeya na kurudi,fursa nyingi sana sana
 
Wew nyumba na gari ndio umeona vitu vya thamani dunian?
Utakuwa unatoka familia ya kimasikini.Yaani gari na nyumba unaona dili sana eee.Wengine sisi vyote hivyo tumezaliwa tumevikuta tunachoangalia ni kuwekeza popote pale ukiwa na hela hata jangwani unaishi acha tabia za kimasikini.Naomba niambie kama Dodoma hakuna mchaga nipe ushahidi mimi nikupe gari.Hapa namanisha kule unakoona hakufai kuishi basi ndio pa kukimbilia wakiamka wewe uko mbali sana.Unaonekana maisha yako ni yale ya kuamka asubuhi huna plani ya siku au mwaka ujao utakuwa nani.
 
Bora ya Lindi unaweza kwenda DSM na kurudi.Mziki huu hapa Kigoma huko barabara ya vumbi,umasikini mwingi mpaka kero.
Kigoma ukiwa na pesa kuzuri sana nimekaa kigoma 2010/2011. shida ilikuapale tu unapotaka kusafiri lakini ukiwa huko poa sana. Nilikua naishi uzunguni mjimwema huko toto kali za kinywranda ushindwe wewe tu. viwanja vya starehe nakumbuka kizota ilikua kila jumatano ni taarabu mpaka asbh hapo unakuta totoz za mwanga, ujiji bangwe. Alhamisi club ukumbi wa stanley, ijumaa live band pale lake tanganyika hotel, jumamosi unashinda bangwe beach jumapili upo kibo kwa mtei
 
Utakuwa unatoka familia ya kimasikini.Yaani gari na nyumba unaona dili sana eee.Wengine sisi vyote hivyo tumezaliwa tumevikuta tunachoangalia ni kuwekeza popote pale ukiwa na hela hata jangwani unaishi acha tabia za kimasikini.Naomba niambie kama Dodoma hakuna mchaga nipe ushahidi mimi nikupe gari.Hapa namanisha kule unakoona hakufai kuishi basi ndio pa kukimbilia wakiamka wewe uko mbali sana.Unaonekana maisha yako ni yale ya kuamka asubuhi huna plani ya siku au mwaka ujao utakuwa nani.
Hivi huyo unaemkaripia umeelewa alichokiandika kweli?au una hangover ya k vant?
 
Umekaa hapo kwa shemej mguu juu unasubir ule chakula cha mchana alaf undelee kuangalia Tv jion ukazurure huku umevaa soks na malapa meupe jion urud uoge usubir chakula cha jion ala uangalie sultan ya azam tv ndo maana unapata ujasiri wa kuandika huu upuzi
Maisha hajakupiga spana bado
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] jioni ukazurure huku umevaa soksi na malapa meupe [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Katika sehemu zilinifanya nienjoy japo sikuwa na pesa ni Tanga mjini nako pazuri ukiwa una pesa hauchoki wala kudhoofu afya.
Moshi Kilimanjaro au Arusha mjini mpaka hiyo meru ni kuzuri good Weather.
Iringa nayo nimekaa kidogo sana napo patakuwa pazuri.

Dodoma kama huna kipato au pesa ni ngumu kwako na ukaamua kuishi ili mradi siku ziende. Nyumba mbovu, msosi duni lazima Upauke kila kitu kuanzia ngozi, nywele, nguo unayovaa tena ukute ni moja, utachomwa na jua kali na vumbi kwako la upepo kama lote na usiku baridi ni yako na kipindi cha mbuu ni chako, maji ya kunywa ya chumvi kali kiu haikati[emoji28]
Dodoma ya watanzania bhana [emoji28] ukitaka uishi pale vizuri basi Shariti uwe na kipato na pesa ya uhakika lakini vinginevyo lazima ufubae na hizo ghasia hapo, nimeishi huko napajua. Ankara lazima kwa dodoma.
Dodoma kuzur, watu wanasagia kisa makao makuu, serikali ndo hipo kule, likizo zangu zote naenda Dom, sehemu yangu ya kutembea royal, karibu kwa wazir mkuu, au dodoma hotel karibu na steshen.
 
Back
Top Bottom