Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Hivi kuna sehemu Tanzania yenye baridi kuliko Maua pale Kilema-Moshi vijijini?
 
Kweli mkuu ktk maeneo ya tz niliyotembelea hizi ni seheme za baridi
Lushoto
Karagwe-kwenda
Kipengere-makete -njombe
Mafinga-Iringa
Lkn eneo linaloongoza hapo ni Makete njombe make huku hadi barafu zinadondoka ndio eneo ambalo mie niliona nyasi mbichi zikiunguzwa na baridi kali
 
Lakini jambo moja kuhusu baridi kali. Je ni kwa nyakati gani za mwaka? Inamaanisha hayo maeneo ya baridi ni baridi mwaka mzima.

Mtujuze ili tujipange mtu anapotaka kutembelea huko.
Hii njombe ni mwaka mzima ukifua nguo subiri zikauke wiki mbili zijazo na ikifika miezi ya 6-8 kama ni mgeni waweza kufa kwa baridi huko muda wote hata mchana watu wamevaa makoti mazito
 
kama hupendi baridi kaa mbali na mkoa uitwao NJOMBE!
 
baridi ya njombe mjini ni kali kuliko ya mbeya mjini,ulizia watu walio ishi sehemu hizo mbili watakuambia
mbeya mjini kuna baridi lakini linaweza kuzoeleka ukikaa siku kadhaa..shida sasa iko njombe baridi lile halizoeleki hata wenyeji wenyewe wanaelewa ni mwendo wa masweta tu!!
nimeishi kote mbeya na njombe..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…