Mkoa nitakaoweza kutoboa kimaisha kirahisi kati ya Dar na Mwanza nikiwa na mshahara wa laki 5 na point

Mkoa nitakaoweza kutoboa kimaisha kirahisi kati ya Dar na Mwanza nikiwa na mshahara wa laki 5 na point

At least unajua kama huwezi kutoboa kwa mshahara.... nenda ukabanane Tanzania ila hapo kwenye kuanzisha biashara uwe makini kwa maana watu wengi huwa wanatamani waanzishe biashara ila badala yake wanajikuta wanajitengenezea kazi nyingine ukiachana na ile kazi waliyo ajiriwa nayo.

Sasa na wewe ukiingia kwenye huo mtego wa kujianzishia kazi nyingine nje ya kazi unayofanya sasa hautoweza kuzimudu zote mbili na badala yake utaopt kuachana na moja ili uende na moja and mara nyingi kazi ya awali inakua na nguvu kuliko ile uliyoianzisha mwenyewe.

Anyway, tunakumbushana tu, all the best mkuu.
 
Mkuu download chatGPT, Inaweza kukusaidia kwa ufasaha sababu ina taharifa nyingi mno, Mfano nimeiuliza imejibu hivi;

Dar es Salaam na Mwanza zote zina fursa kibiashara, lakini kila moja ina faida na changamoto zake kulingana na sekta mbalimbali.

Dar es Salaam:

Dar es Salaam ni jiji kubwa zaidi na kitovu cha uchumi cha Tanzania, na inatoa fursa nyingi za kibiashara, hasa katika sekta zifuatazo:

Biashara na Usafirishaji: Kama bandari kuu ya nchi, ni lango la biashara za kimataifa. Biashara zinazohusiana na usafirishaji, usambazaji, na huduma za bandari zinaendelea kukua.

Viwanda: Sekta ya viwanda inakua, hasa katika usindikaji wa chakula, saruji, na mavazi.

Utalii na Ujenzi wa Mali Isiyohamishika: Dar es Salaam ni jiji la pwani lenye vivutio vya kitalii, kama vile fukwe nzuri, na hivyo fursa za utalii na uwekezaji katika sekta ya mali isiyohamishika zinapatikana.

Huduma za Fedha: Jiji hili lina sekta ya benki na fedha iliyoendelea, na pia kuna fursa katika teknolojia ya fedha (fintech).


Changamoto za Dar es Salaam: Ushindani mkubwa na gharama za kufanya biashara katika jiji lenye miji mingi na miundombinu ya juu.

Mwanza:

Mwanza, iliyo kando ya Ziwa Victoria, pia ina fursa nyingi, hasa katika maeneo haya:

Kilimo na Biashara za Kilimo: Eneo hili lina ardhi yenye rutuba, hivyo kilimo na biashara zinazohusiana na mazao kama mahindi, maharage, na karanga ni faida.

Uvuvi na Usindikaji wa Samaki: Mwanza ni moja ya maeneo muhimu ya uvuvi kwenye Ziwa Victoria, na hivyo kuna fursa kubwa katika biashara ya uvuvi na usindikaji wa samaki.

Madini: Mwanza ni nyumbani kwa baadhi ya migodi ya dhahabu ya Tanzania, na hivyo kuna fursa katika huduma za madini na vifaa vya uchimbaji.

Utalii: Kwa kuwa Mwanza inapata watalii wanaotembelea Ziwa Victoria na maeneo ya karibu, biashara za utalii kama malazi, usafiri, na huduma za mwongozo wa kitalii zinakuwa.


Changamoto za Mwanza: Miundombinu ya jiji, kama barabara na huduma za umma, inaweza kuwa na changamoto, hasa ikilinganishwa na Dar es Salaam.

Hitimisho:

Dar es Salaam inatoa fursa za biashara nyingi na kubwa, hasa kwa makampuni ya kimataifa na biashara za kimataifa.

Mwanza, kwa upande mwingine, inatoa fursa katika kilimo, uvuvi, madini, na biashara za utalii zinazohusiana na Ziwa Victoria.


Kwa hiyo, uteuzi wa jiji la kuanzisha biashara unategemea aina ya biashara unayotaka kuanzisha. Dar es Salaam ni bora kwa biashara kubwa na za kimataifa, wakati Mwanza inafaa zaidi kwa biashara zinazohusiana na kilimo, madini, na rasilimali za Ziwa Victoria.
Sbte sana ndugu kwa ufafanuzi mzuri Sasa ngoja nitulize hiki kichwa changu nichanganue
 
Si Mwanza,Dar, hapo ulipo au popote pale patakufanya ufaninikiwe. Mafanikio yanaanza kwenye akilia yako, ukiwa na akilia ya kimafanikio hata nyasi unaweza kuzifanya zikawa pesa.
Nashukuru kwa ushauri
 
At least unajua kama huwezi kutoboa kwa mshahara.... nenda ukabanane Tanzania ila hapo kwenye kuanzisha biashara uwe makini kwa maana watu wengi huwa wanatamani waanzishe biashara ila badala yake wanajikuta wanajitengenezea kazi nyingine ukiachana na ile kazi waliyo ajiriwa nayo.

Sasa na wewe ukiingia kwenye huo mtego wa kujianzishia kazi nyingine nje ya kazi unayofanya sasa hautoweza kuzimudu zote mbili na badala yake utaopt kuachana na moja ili uende na moja and mara nyingi kazi ya awali inakua na nguvu kuliko ile uliyoianzisha mwenyewe.

Anyway, tunakumbushana tu, all the best mkuu.
Asante sana kwa Hilo angalizo ntajitahidi nisijichanganye
 
Unatafuta side hustle if yes jaribu kuja DSM

Tafuta chumba maeneo ya uswahili ambayo ni cheap

Then tafuta location ufungue duka la matumizi.

Ahsubui uwe unamuacha Kijana anakimbiza hadi saa 12 jion then wewe unaanza jioni na kumaliza hadi saatano usiku.

Kupitia duka la matumizi Kwa maeneo ya uswahili mzunguko ni mzuri.

Hivyo duka lako ulitunze na kulikuza zaidi mpaka ifike wakati mashahara wako usiwe unautumia.

Fanya hivyo Kwa 1-3 then ndo ufungue duka la pili na ununue Bajaji toyo ya Kuwa unasupply bidhaa.
 
Nenda Mwanza ni jiji ambalo lina fursa nyingi upande wa Kanda ya Ziwa ukiwa Mwanza utahisi upo Mkoani kwenu kwa Mazingira,maisha na hakuna changamoto nyingi kama jiji pendwa....gharama za maisha zipo chini sana kwa Mwanza ni sehemu nzuri kwa mtu anaejitafuta.

Dar es salaam jiji kuu lenye kila aina ya biashara na shughuli nyingi za kiuchumi kila mmoja ametumwa pesa watu wanashughulika sana masaa 24/7 watu hawalali sio kwa kupenda hapana ni kulazimishwa na maisha ya jiji hilo kiufupi watu wanateseka sana.
 
Back
Top Bottom