Mkoa nitakaoweza kutoboa kimaisha kirahisi kati ya Dar na Mwanza nikiwa na mshahara wa laki 5 na point

At least unajua kama huwezi kutoboa kwa mshahara.... nenda ukabanane Tanzania ila hapo kwenye kuanzisha biashara uwe makini kwa maana watu wengi huwa wanatamani waanzishe biashara ila badala yake wanajikuta wanajitengenezea kazi nyingine ukiachana na ile kazi waliyo ajiriwa nayo.

Sasa na wewe ukiingia kwenye huo mtego wa kujianzishia kazi nyingine nje ya kazi unayofanya sasa hautoweza kuzimudu zote mbili na badala yake utaopt kuachana na moja ili uende na moja and mara nyingi kazi ya awali inakua na nguvu kuliko ile uliyoianzisha mwenyewe.

Anyway, tunakumbushana tu, all the best mkuu.
 
Sbte sana ndugu kwa ufafanuzi mzuri Sasa ngoja nitulize hiki kichwa changu nichanganue
 
Si Mwanza,Dar, hapo ulipo au popote pale patakufanya ufaninikiwe. Mafanikio yanaanza kwenye akilia yako, ukiwa na akilia ya kimafanikio hata nyasi unaweza kuzifanya zikawa pesa.
Nashukuru kwa ushauri
 
Asante sana kwa Hilo angalizo ntajitahidi nisijichanganye
 
Unatafuta side hustle if yes jaribu kuja DSM

Tafuta chumba maeneo ya uswahili ambayo ni cheap

Then tafuta location ufungue duka la matumizi.

Ahsubui uwe unamuacha Kijana anakimbiza hadi saa 12 jion then wewe unaanza jioni na kumaliza hadi saatano usiku.

Kupitia duka la matumizi Kwa maeneo ya uswahili mzunguko ni mzuri.

Hivyo duka lako ulitunze na kulikuza zaidi mpaka ifike wakati mashahara wako usiwe unautumia.

Fanya hivyo Kwa 1-3 then ndo ufungue duka la pili na ununue Bajaji toyo ya Kuwa unasupply bidhaa.
 
Nenda Mwanza ni jiji ambalo lina fursa nyingi upande wa Kanda ya Ziwa ukiwa Mwanza utahisi upo Mkoani kwenu kwa Mazingira,maisha na hakuna changamoto nyingi kama jiji pendwa....gharama za maisha zipo chini sana kwa Mwanza ni sehemu nzuri kwa mtu anaejitafuta.

Dar es salaam jiji kuu lenye kila aina ya biashara na shughuli nyingi za kiuchumi kila mmoja ametumwa pesa watu wanashughulika sana masaa 24/7 watu hawalali sio kwa kupenda hapana ni kulazimishwa na maisha ya jiji hilo kiufupi watu wanateseka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…