BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Ripoti kutoka kwa Mganda Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Alfred Mwakalebela imeeleza kuwa idadi hiyo ni wastani wa Watoto 2 hadi 3 kwa wiki ambao hufanyiwa ukatili wa Kubakwa na Kulawitiwa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Kilolo, Omary Juma, amesema Watoto 30 walibakwa na Kesi ziko Mahakamani lakini bado wanashindwa kudhibiti tatizo kwa sababu familia za Waathirika hazitoi ushirikiano kwa Vyombo vinavyofuatilia taarifa.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu hali ya Kimataifa ya Kuzuia Ukatili dhidi ya Watoto ya mwaka 2020 ilionesha nusu ya Watoto duniani (Takribani Watoto Bilioni 1) wanaathirika na Ukatili wa Kimwili, Kingono, Kisaikolojia na Kujeruhiwa.
===================
ULAWITI na ubakaji siyo tena msamiati mgeni masikioni mwa wengi, licha ya kuwa na athari nyingi za kiafya kwa watoto wa kike na wanaume.
Vitendo hivyo mbali na kuacha ulemavu wa kudumu kwa watoto na kuwaathiri kimwili, kisaikolojia, huwaachia majeraha hata ujauzito, maradhi, baadhi yao hupoteza maisha na kukosa haki ya msingi ya kuishi.
Taarifa kutoka Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Iringa, inaripoti kuwa watoto 12 kila mwezi hufikishwa hospitalini hapo ukiwa ni wastani wa watoto wawili hadi watatu kwa wiki, kesi za kubakwa na kulawitiwa.
Mganga Mfawidhi, Alfred Mwakalebela, anasema matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto yanaongezeka mkoani humo, licha ya hatua mbalimbali ya kudhibiti kuchukuliwa.
Anasema Iringa ni miongoni mwa mikoa inayokabiliwa na matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa kwa kiwango kikubwa.
“Kesi za ubakaji katika hospitali yetu kwa wiki tunapata kati ya watoto wawili hadi watatu na kwa mwezi kesi za kubaka watoto na wanawake tunazipokea kuanzia 12, kwa hiyo ubakaji kwa Iringa ni mwingi na idadi itakuwa kubwa zaidi huko mitaani,” anasema Dk. Mwakalebela.
Aidha, takwimu za Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa mwaka 2019 matukio 15,680 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto ukiwamo ubakaji yalirekodiwa kitaifa na kwamba matendo hayo yamekuwa yakiongezeka kila mwaka. Mathalan, 2017 polisi inasema yalikuwa 13,457 na uliofuata yakawa 14,419.
SABABU ZA UKATILI
Ulawiti na ubakaji unaongezeka mkoani Iringa, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Kilolo, Kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa, Omary Juma, anasema zaidi ya watoto 28 katika kata yake, wameathirika.
“Watoto takribani 30 walilawitiwa na walibakwa, kesi ziko mahakamani, tunazifuatilia na katika mtaa wangu wa Kihesa Kilolo tatizo ni kubwa Shule ya Igeleke na zinazopakana na hizo, tatizo hili ni kubwa.”
“Tunashindwa kulidhibiti kwa sababu familia hazitoi ushirikiano, watoto wale wale waliobakwa wako bado kwenye mazingira magumu, wanaachwa peke yao hakuna anayewasimamia, wala anayewafuatilia, wamebaki wanafanyiwa ukatili, wameachwa huru,” anaongeza.
Mwenyekiti Omary, anataja kukosa malezi sahihi ya wazazi na kutumbukia katika mikono isiyo salama kuwa ni sababu ya matukio hayo kushamiri.
“Tatizo kubwa liko kwenye malezi ya familia watoto wanajilea wenyewe, kuanzia asubuhi hajamuona mama wala baba wanatafuta maisha. Analelewa na watu wengine na mwisho wa siku ndiyo wanaotengeneza mazingira na kumbaka, wazazi na walezi hawana habari,” anaongeza Omary.
Anautaja ushirikina na ukosefu wa maadili kwenye jamii ukiwamo matumizi ya dawa za kulevya na makundi rika yanayoendekeza tabia hatarishi kuwa ni chanzo.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kimataifa ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto ya mwaka 2020 inabainisha kuwa nusu ya watoto duniani sawa na takribani watoto bilioni moja kila mwaka wanaathirika na ukatili wa kimwili, kingono au kisaikolojia na kujeruhiwa.
Watoto hao husababishiwa ulemavu wa kudumu na wakati mwingine kifo kwa sababu serikali zinashindwa kufuata mikakati iliyowekwa ya kuwalinda watoto.
Ripoti iliyopewa jina la “hali ya kimataifa katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto 2020” ni ya kwanza ya aina yake ikiainisha hatua zilizopigwa katika nchi 115 chini ya mkakati wa INSPIRE ambao unajumuisha mikakati saba kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto.
Karibu nchi zote zina sheria muhimu za kuwalinda watoto dhidi ya ukatili lakini ni chini ya nusu ya nchi hizo mikakati hiyo inatekelezwa ipasavyo.
ATHARI
Paskalina Lweve, Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Iringa, anaeleza kuwa madhara ya ubakaji na ulawiti ni endelevu hata wakiwa wakubwa, hivyo hatua za haraka zinahitajika kuwalinda watoto.
“Watoto wetu watakuwa katika wakati mgumu kwa sababu tutajua tuko na watoto wa kiume kumbe wameshaharibika, sijui niseme ni wanawake au sijui niseme ni nini kwa sababu kitakuwa ni kizazi kilichoharibikiwa ni majanga makubwa, tusifumbie macho kuna madhara kwa nguvu kazi ya taifa,” anasema Paskalina.
Peter Mkwama ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee na Ushauri Mkoa wa Iringa, anasema matokeo ya kushamiri kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti katika jamii ni kupuuzia maonyo ya wazee hasa yanayohamasisha kujenga jamii yenye maadili na haki.
Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009, inaeleza kuwa jamii ina wajibu wa kuwalinda watoto dhidi ya hatari zote hasa inayohatarisha usalama na mstakabali wa maisha yao.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, endapo mtu atafanya vitendo vinavyoharibu utu wa watoto atakabiliwa na adhabu kikiwamo kifungo.
Ikiwa jamii na familia wakizungumza na watoto na vijana wa rika balehe kuhusu madhara ya matukio hayo, huenda ikasaidia kutokomeza ukatili huo.
“Lazima, tuzungumze na familia, turudi kwa vijana wetu, tunakazana kuzungumza na watoto wetu huku vyanzo ambavyo ni familia tukiviacha, haiwezekani hadi mtoto mchanga abakwe na kulawitiwa huku kwetu mtoto amelawitiwa hadi wa miaka mitatu, wazazi na jamii iko wapi? Lazima tulitazame hili haiwezekani,” anasema Mkwama.
Viongozi wa dini nao wana nafasi kubwa katika mapambano dhidi ya ubakaji na ulawiti, kwa lugha nyingine ndiyo wana nafasi kuhakikisha matendo maovu kama ulawiti na ubakaji mkoani Iringa vinakoma.
“Lazima tufike mahali serikali, wadau mbalimbali na sisi viongozi wa dini tuweke nguvu ya pamoja kukabiliana na vitendo hivyo ili kuvitokomeza huku tukiendelea kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili dhidi ya watoto.”
UDHIBITI
Kutokana na ukubwa wa tatizo Manispaa ya Iringa imeanzisha kampeni ya kutokomeza ukatili kwa kushirikiana na viongozi wa dini.
Ibrahimu Ng’wada ni Meya wa Manispaa ya Iringa anayesema wamebaini uwepo wa utitiri wa matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto.
“Sisi halmashauri tuliitisha mkutano kwa viongozi wa dini zote, ili tusaidiane kutoa elimu kwa wananchi lakini na wao walikuja na mapendekezo kuwa ianzishwa siku maalumu ya kuadhimisha kupinga ukatili wa kijinsia mkoani humo,” anasema Ng’wada.
Jane Mwalembe ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Ukatili anasema kupaza sauti na kukemea vitendo hivyo kupunguza wahalifu kukamatwa na matukio hayo kupungua kwenye jamii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kesi za ubakaji mkoa humo, wamezidi kuongezeka na zinapewa kipaumbele na kuwatia hatiani wanaobainika kutenda makosa hayo ya ukatili.
Kesi hizo ni ubakaji Wilaya ya Iringa 35, Kilolo 19 na Mufindi kwa kipindi cha Januari hadi Septemba mwaka 2022.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Sunday Songwe, anasema jeshi hilo linaendelea na misako ili kudhibiti uhalifu huo, akiwataka wananchi kutoa taarifa za uwepo na viashiria vya ukatili mkoani humo.
“Tunapambana na uhalifu na wahalifu wa ubakaji na ulawiti kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa ili sheria ifuate mkondo wake. Niwaombe wananchi tushiriki kikamilifu kutoa taarifa na si kuliachia Jeshi la polisi pekee,” anasema Songwe.
Baadhi ya wazazi na walezi katika Manispaa ya Iringa wanakiri wazi uzembe wao unachagiza kuongezeka kwa matukio hayo na kwamba wamepata funzo kusimama vema katika jukumu lao la malezi ya watoto.
NIPASHE