Mkoa wa Kagera na Ufukara

Ok
 
Kwa nini makampuni hayaji kwenu? Nyanda za Juu Kusini Kuna makampuni ya Wazawa unadhani ni Shinyanga kule? Au Geita Kwa mzungu?

Kama haupo top 10 au hujafikisha 2.8mln wewe ni maskini tuuView attachment 2784567 View attachment 2784567
Unaruka ruka tu nakupa mfano mmoja, njombe kuna uzalishaji mkubwa wa bidhaa za mbao lakini mashamba asilimia kubwa wamewekeza watu au makampuni machache na raia wengi wamebaki kuwa vibarua na mwisho wa siku pato la hayo mashamba wanahesabiwa raia ambao hawanufaiki zaidi ya kuwa vibarua, ila njoo Kagera mashamba yote ya miti yanamilikiwa na wananchi japo sio kiwango kikubwa sana lakini ela inaenda moja kwa moja kwa watu
 
Bora umesema kweli, kuna watu uwezo wa kufikiri kwao ni mdogo sana, kwa Kagera hamna viwanda vikubwa au migodi wala utalii wowote kinachoonekana kwa Kagera ni direct kutoka kwa wananchi
Kwa i Njombe kuna viwanda gani ? Mbona Pwani wana viwanda vingi lakini ni maskini kama Kagera tu ?
 
Kwa i Njombe kuna viwanda gani ? Mbona Pwani wana viwanda vingi lakini ni maskini kama Kagera tu ?
Unapopima GDP per capital usisahau na population ndugu ndo maana Marekani sio namba moja kwenye kipimo cha per capital japo ina uchumi mkubwa
 
Kwa hiyo wewe ndio unanifundisha Mimi kuhusu Njombe kwetu au? Acha ujinga wewe ,90% ya mashamba ya miti ni watu binafsi ,hayo makampuni ni kiduchu sana.

Mfano mzuri ni Wilaya ya Makete ilikuwa ya mwisho Kwa mapato miaka 3 tuu Iliyopita,tangu Barabara zifunguke inaongoza Mkoa wa Njombe Kwa mapato hivyo hivyo Kudewa inaelekea huko.

Endeleeni kutafuta excuses za uvivu mtaishia hivyo hivyo
 
Mbona Ruvuma ni mbali na Bandari lakini ni matajiri ? Huna hoja kabisa. Kagera ni maskini kwa sababu hawana ardhi, wana urasimu, mzee hawezi kuruhusu mtoto wake alime shamba lake mpaka afe na akifa anatoa wosia na kurithisha mtoto mmoja wa kiume anayempenda.
Baada ya tukio hilo watoto wengi hukimbilia mikoa mingine kuja kuwa boda boda au kwe ye vibanda vya mpesa na wasichana kuwa maabamedi.
 
Simiyu labda inaweza kuwa iko chini kwenye makusanyo ya Serikali ila sina uhakika kama ni mkoa fukara kwa sababu ni mojawapo ya mikoa yenye ng'ombe wengi hapa Tanzania.
Kumbuka kuwa Tanzania ni ya pili DUNIANI kwa uwingi wa ng'ombe, ya kwanza ikiwa ni Ethiopia
 
Endelea kuisikia Kagera kwenye makaratasi ila uhalisia huku pesa zipo kwa wananchi tofauti na huko zinamilikiwa na watu wachache
 
Alafu hao ndo wamejenga Kagera majumba mazuri au na hilo utabishi???
 
Kwanza waelewe kwamba huko Shinyanga wanakodharau ndio kuna wakulima stadi wa mpunga, unakuta msukuma mmoja tu kwa mwaka anavuma magunia mpaka 800 ya mpunga. Mhaya anaweza hiyo ? Nenda Kyamuyorwa na Buligi huko hata Karagwe wasukuma wemeingia huko na wamenunua mbuga na wanapiga mpunga hadi wahaya na wanyambo wanashangaa. Bado msukuma ana ng'ombe na kila siku usukumani miji midogo ya kibiashara inazaliwa kutokana na uchapakazi wa wasukuma. Angali Katoro Geita, Lunzewe, Masumbwe, Nyarugusu, Lamadi, Humgumalwa, kagongwa, n.k. kwa vyovyote vile lazima Shinyanga iwe juu tu ya Kagera
 
Endelea kuisikia Kagera kwenye makaratasi ila uhalisia huku pesa zipo kwa wananchi tofauti na huko zinamilikiwa na watu wachache
Huko Kwa maskini nimeghairi kuja ntapoteza pesa zangu Bure,Bora niende Kigoma nimeona kunakucha sana
 
Yani mchango wangu wote umeona nimetaja umbali pekee? Ina maana vyote nilivyotaja hujasoma umesoma tu suala la umbali.

Na wewe unaona chanzo pekee ni ardhi hakuna sababu nyingine.
 
Sasa Msukuma mwenye familia ya watu 40 kwa nini asizalishe, Ila mwisho wa siku ukigawanya kwa hao watu hakuna alichofanya
 
Huko Kwa maskini nimeghairi kuja ntapoteza pesa zangu Bure,Bora niende Kigoma nimeona kunakucha sana
[emoji23][emoji23][emoji23] Bukoba haina hasara, ila ungekuja kutoa tongotongo maana Kagera kuna ghorofa 700+ hakuna mkoa wowote wa kusogeza pua huko kusini zaidi ya Mbeya inayobebwa na kanda
 
Sasa Msukuma mwenye familia ya watu 40 kwa nini asizalishe, Ila mwisho wa siku ukigawanya kwa hao watu hakuna alichofanya
Mbona Mwanza, Geita na Shinyanga iko juu ya Kagera ? Wahaya sasa wameamua kuhamia usukumani maana wameona kutegemea migomba tu hakuwasaidii na kwa hatua hiyo nawaunga mkono kabisa.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Bukoba haina hasara, ila ungekuja kutoa tongotongo maana Kagera kuna ghorofa 700+ hakuna mkoa wowote wa kusogeza pua huko kusini zaidi ya Mbeya inayobebwa na kanda
Hizo Gorofa 700 plus ni za Mkoa mzima sio Bukoba

Pili Morogoro nayo Iko kwenye Mikoa maskini tuu japo Ina gorofa kuzidi hata Mbeya.

Wahaya walioko Mikoa mingine kazini wanashindana kujenga majumba ya gorofa Vijijini kwao ila hayazalishi.
 
Nilifika Bukoba kwa mara ya kwanza mwaka 2020, nilienda mpaka Mutukula. Ni "nchi" nzuri iliyoshiba ukijani kutokana na ardhi yenye rutuba na hali ya hewa nzuri. Kwa mwonekano wa haraka, wakazi wake hawakumbwi na tatizo la njaa.

Mwishoni mwa mwaka Jana na mwanzoni mwa mwaka huu pia nilienda huko. Safari hii sikuishia Bukoba Mjini na Mutukula, bali nilienda hadi Karagwe na Ngara.

Katika maeneo yote niliyoyapita wilayani Karagwe, ikiwa ni pamoja na Vijijini, sikuona nyumba ya nyasi.

Pamoja na kwamba sikuuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali huko, lakini naweza nikasema haya kuhusu Mkoa wa Kagera, nikitumia wilaya ya Karagwe na Bukoba Mjini kama case study:
1. Wana ardhi nzuri

2. Ni watunzaji wa mazingira, maeneo mengi yana miti

3. Ina idadi kubwa ya wasomi

4. Ingawa na masikini wapo pia, lakini kunaonekana kuna idadi kubwa ya wakazi wa uchumi wa kati na matajiri. Majengo yao yanawaakisi. Kuna maeneo mengine japo ni migombani lakini unaweza ukakuta nyumba za kifahari hasa.

Kwa hiyo nakubaliana na hoja za wanaosema Kagera Mkoa ni maskini lakini wakazi wake si maskini.
 
Mikoa inayolima mahindi na mpunga haizuiliwi kuuza nje hata kama inapandisha gharama ya chakula kwa soko la ndani ila Kagera kuuza kahawa nje ni jambo gumu sana, wakati nchi ikikosa kahawa haina hamna kinachobadilika.
Kulima nilime mwenyewe, lakini kuuza nipangiwe na mwingine? Aaagh! Huo ni uonevu sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…