Geographical location ya mkoa wa Kagera na rasilimali zake haziuruhusu uchangie pakubwa kwenye pato la taifa. Hakuna viwanda, nani ajenge kiwanda kipo more than 1000km kutoka bandarini? Malighafi zitafikaje na finished products zitafikaje.
Hakuna migodi wala utalii wa maana sasa kodi serikali ipate kutoka wapi.
Mkoa umezungukwa na nchi maskini Rwanda, Burundi na Uganda ambazo nchi hizo zina mazao yaleyale yanayopatikana mkoa huo. Hakuna exchange ya products.
Mkoa hauna miradi ya uzalishaji ya serikali. Hutosikia kimejengwa kiwanda cha kahawa, wala mazao ya mbao, wala soko la mataifa jirani.
Serikali haitaki kuona mkoa unaendelea kwenye kilimo. Ikitokea fursa yoyote ya kilimo serikali inaona wivu, hivi Tanzania hii kuna zao linaloshushwa bei mara 10 kama ilivyo kwa vanilla? Leo kilo ni 100,000 mwakani kilo 10,000 na wanunuaji hamna. Hilo zao lingekuwa kubwa huko kuliko mkoa wowote.
Mikoa inayolima mahindi na mpunga haizuiliwi kuuza nje hata kama inapandisha gharama ya chakula kwa soko la ndani ila Kagera kuuza kahawa nje ni jambo gumu sana, wakati nchi ikikosa kahawa haina hamna kinachobadilika.
Mkoa unapakana na nchi nyingi hivyo ni hatarishi kwa magonjwa ya kuambukiza, vita na uhamiaji ikitokea machafuko kwa majirani. Hayo yote yanatokea na hakuna jitihada za serikali kupunguza madhara, kwanini baada ya vita ya Kagera tulilipwa reparations na Uganda. Kwenye hiyo hela kuna iliyoenda mkoa ule kufidia athari? Majengo, madaraja, shule na vifo vingi vilitokea kule ila hela ya fidia haikwenda.
Tetemeko lilitokea michango jamaa akaipeleka anakojua yeye.
Kuna tofauti ya eneo kuwa maskini na watu wa eneo kuwa maskini. Wapemba wana maduka Kariakoo na wamejaa nchi nzima wakinunua na kuuza bidhaa, ambaye hajawahi kwenda kwao hawezi amini ukimwambia hawana hata vyoo wanajisaidia baharini na vichakani.
Serikali ikiwa na wivu na eneo haliwezi endelea. Pwani inapewa kila kitu na haijulikani kwanini. Shinyanga ina umaskini sana na matukio ya kutisha ukiachana na migodi ya wazungu. Morogoro imejaa wageni kuna fursa za kutosha ila kuna makabila uko wakimaliza mavuno wanapiga sherehe mazao yanaisha wanasubiri msimu mwingine. Hii nchi distribution kwa mikoa ya mbali ni ndogo.