Mkoa wa Mara washika nafasi ya 5 kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika

Mkoa wa Mara washika nafasi ya 5 kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Taarifa iiyotolewa Afisa Elimu wa Mkoa, Benjamin Oganga imeonesha pia kuwa mkoa huo umeshika nafasi ya 5 kitaifa kwa kuwa na wanafunzi wanaohitimu darasa la 7, bila kujua kusoma na kuandika.

Oganga ameongeza kuwa ufatiliaji uliofanywa unaonesha ndani ya miaka mitano, wanafunzi 350,000 katika mkoa huo hawakuhitimu elimu ya msingi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Suleiman Mzee, ameagiza viongozi wa elimu kuanzia ngazi ya shule mpaka mkoa kushirikiana na mamlaka nyingine, kutafuta kila mwanafunzi aliyetakiwa kuwa shuleni, lakini hayupo na kwamba ikiwezekana wazazi wa wanafunzi hao wakamatwe.
 
Back
Top Bottom