Mkoa wa Pwani una vijiji na Mapori ya kutisha sana

Kweli kabisa nakuunga mkono,nilitembea mara Kwa mara Kuna kipindi hapo tu kimanzichana ndani ndani karibu kilometa kama 16 kutoka kimanzichana center kuelekea njia ya bungo ndani Kwa ndani, aisee japokuwa Kuna watu wanachoma mkaa na nilikuwa napishana sana na pikipiki zilizobeba gunia kubwa za mkaa kuanzia tano lakini bado Kuna mapori ya kutisha sana.
 
Wakuu hayo mapori fursa,hizo pori uki iangusha ukatia ufuta,mkorosho mixa minazi utajiri huu huu hapa.

Kila kitu usikiangalie kwa jicho hasi.
 
Niliwakuta Wasukuma wengi wamehamia maeneo ya Kibiti, mapori hayana muda mrefu yote yataiisha. Jamaa hawana urafiki kabisa na misitu tuwape muda patakuwa peupe.
 
Mkuranga ndiko alikozaliwa na kukulia Bibie FaizaFoxy
 
Pwani ni rahisi kuficha majambazi na magaidi
Upo sawa mkuu nimewahi ishi kisarawe huko ndani ndani
mzenga,gwata,chore, mto ruvu asee kuna mapori ajabu .
daima nilikuwa nawazaga kama wewe na zaidi niliwaza hii ardhi ingepewa wasukuma kwa jinsi ilivyo na rutuba hivi
hakika wangekuwa mbali sana
 
mfano kuna eneo liko hapo karibu na kiwanda cha SSB cha juice mwandege.lile pori limezungukwa na makazi ya watu kwa 100% na yamekuwa maficho ya wahalifu .Pale wangeweka hata huduma za kijamii soko kubwa kuhudumia mikoa ya kusini .nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…