Mkoa wa Pwani una vijiji na Mapori ya kutisha sana

Mkoa wa Pwani una vijiji na Mapori ya kutisha sana

Licha ya huu mkoa kupakana na jiji la Dar es salaam ambalo ndo jiji kubwa Tanzania na Africa Mashariki Kwa ujumla, lakini mkoa wa Pwani unatishia, Mkoa wa Pwani una Mapori mazito yamefunga Giza na ya kuogopesha sana.

Me natokea Kanda ya ziwa, mkoa wa Kagera tuna vijiji na Mapori ila Kwa mkoa wa Pwani usipime
Ukitoka Dar hapo ukaingia Mkuranga tu Kuna vijiji kama unaenda Kisiju hadi huko visiwani Kwale na kama ni hatari ndugu zangu.

Ukisogea Kisarawe, Kibiti, na Rufiji huko ndo hatari zaidi. Kuna siku nilikuwa naenda kwenye Bwawa la umeme huko Rufiji panaogopesha mno. Bado Mapori ya Bagamoyo hadi msata huko ni hatari tupu.

Nashauri serikali ihamishie Kambi za jeshi za Dar huko kama za Lugalo n.k huko usalama wa jiji la Dar na taifa Kwa ujumla, maana wahalifu ni rahisi kujificha humo.
Kweli kabisa nakuunga mkono,nilitembea mara Kwa mara Kuna kipindi hapo tu kimanzichana ndani ndani karibu kilometa kama 16 kutoka kimanzichana center kuelekea njia ya bungo ndani Kwa ndani, aisee japokuwa Kuna watu wanachoma mkaa na nilikuwa napishana sana na pikipiki zilizobeba gunia kubwa za mkaa kuanzia tano lakini bado Kuna mapori ya kutisha sana.
 
Wakuu hayo mapori fursa,hizo pori uki iangusha ukatia ufuta,mkorosho mixa minazi utajiri huu huu hapa.

Kila kitu usikiangalie kwa jicho hasi.
 
Niliwakuta Wasukuma wengi wamehamia maeneo ya Kibiti, mapori hayana muda mrefu yote yataiisha. Jamaa hawana urafiki kabisa na misitu tuwape muda patakuwa peupe.
 
Licha ya huu mkoa kupakana na jiji la Dar es salaam ambalo ndo jiji kubwa Tanzania na Africa Mashariki Kwa ujumla, lakini mkoa wa Pwani unatishia, Mkoa wa Pwani una Mapori mazito yamefunga Giza na ya kuogopesha sana.

Me natokea Kanda ya ziwa, mkoa wa Kagera tuna vijiji na Mapori ila Kwa mkoa wa Pwani usipime
Ukitoka Dar hapo ukaingia Mkuranga tu Kuna vijiji kama unaenda Kisiju hadi huko visiwani Kwale na kama ni hatari ndugu zangu.

Ukisogea Kisarawe, Kibiti, na Rufiji huko ndo hatari zaidi. Kuna siku nilikuwa naenda kwenye Bwawa la umeme huko Rufiji panaogopesha mno. Bado Mapori ya Bagamoyo hadi msata huko ni hatari tupu.

Nashauri serikali ihamishie Kambi za jeshi za Dar huko kama za Lugalo n.k huko usalama wa jiji la Dar na taifa Kwa ujumla, maana wahalifu ni rahisi kujificha humo.
Mkuranga ndiko alikozaliwa na kukulia Bibie FaizaFoxy
 
Pwani ni rahisi kuficha majambazi na magaidi
Upo sawa mkuu nimewahi ishi kisarawe huko ndani ndani
mzenga,gwata,chore, mto ruvu asee kuna mapori ajabu .
daima nilikuwa nawazaga kama wewe na zaidi niliwaza hii ardhi ingepewa wasukuma kwa jinsi ilivyo na rutuba hivi
hakika wangekuwa mbali sana
 
mfano kuna eneo liko hapo karibu na kiwanda cha SSB cha juice mwandege.lile pori limezungukwa na makazi ya watu kwa 100% na yamekuwa maficho ya wahalifu .Pale wangeweka hata huduma za kijamii soko kubwa kuhudumia mikoa ya kusini .nk
 
Back
Top Bottom