Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Stress huanzia moja kwa moja kwenye kikokotoo kisicho rafiki. Kwa hutwo tuela twa mboga tu unaanzaje kututumia kufungulia biashara? Lahaula lakwata!
 
Mbona alikua anakujibu vizuri tuu🤣🤣, wewe mbona unatuuliza tupo wapi?
 
Kuna mwalimu jiran na home yeye kafuta Coster ya biashara aiseee gari ilileta ugomvi mkubwa kwa watoto na gari ilianza kutafuna pesa baada ya kuingiza pesa saiz hana kitu amebaki na ugonjwa wa presha na kuota ndoto ngumu usiku.
 
kinachowaponza watumishi wakianza biashara wakiwa kazini,ni kupata hela kila mwezi. hii inamfanya akipata changamoto kidogo kwenye kabiashara kake alikokafungua anatukana na anaifunga kwasababu anajua tarehe ikifika anaenda kukinga ananunua mahitaji ya nyumbani.akishtuka bado miaka mi3 astafu na bado ahajipanga kwa lolote.

hii ni kwasababu watanzania wepesi kulizika hasa akiwa na kasent mfukoni.
mtumishi ukiwa kazini ukifungua biashara hakikisha unapambana na changamoto yoyote inayokuja mbele yako na sio kuifunga na kukimbia changamoto. maana ukiikimbia changamoto hutoweza kujifunza biashara wala kufanikiwa. kama umekimbia changamoto ukiwa kazini hata ukipata hayo mafao changamoto zile ulizozikwepa zitakusubili palepale. na hapa ndipo wanapofeli.
 
Mmh hapana nliona mambo ni mchanganyiko asee nikimpigia sijui alikua anahisi nataka hela zake, anapokea hasemi halooo akipokea "eeh unasemaje" nikaona hapana.....

Mi mbona sitoleagi mate mali ya mtu yoyote nkaamua kukaa kimya kwanza.
🤣🤣🤣maza wetu ni nomaaa alikua anaona km unampigia kelele 🤣🤣🤣
 
Daaah me hii naona asilimia kubwa ya wastafu inawakuta hii,mzee alistafu nakumbuka kila nikimuuliza kapewa kiasi gani anasema kidogo tu,kuna siku nilikuwa namrekebishia smart phone yake ile kupita pita kwenye msg nakuta nakutana na salio la account yake sio chini 100mln nilistuka ila nikakausha tu.juzi kati alikuwa anafanya rekebisha nyumba yake ya biashara naona kaenda kukopa bank ili wawe wanamkata kwenye accont yake ya nssf nikajuliuliza ina maana zile milioni 100 zimeyeyuka..siku uliza kwa vile pesa ni zakee ...hawakawihii kusema unataka kumuua
 
Kuna mwalimu jiran na home yeye kafuta Coster ya biashara aiseee gari ilileta ugomvi mkubwa kwa watoto na gari ilianza kutafuna pesa baada ya kuingiza pesa saiz hana kitu amebaki na ugonjwa wa presha na kuota ndoto ngumu usiku.
Inasikitisha sana. Kuna mmoja jirani yetu ye alistaafu udereva wa malori. Akanunua fuso tandamu hata mimi nilimsapoti sababu najua hajatoka kwenye career yake.
Gari ilipiga tripu mbili tu chali ye mwenyewe majeruhi.
Likaanza kutafuna pesa ya mafao mpaka likakaa sawa. Akampa dereva mana akajihisi yeye age go.
Dere tiripu moja tu tandahimba limeacha njia limeingia maporomokoni limetokq skrepa limeuzwa chuma chakavu na yeye magonjwa nyemelezi yakamuandama mpaka avyopumzika milele.
 
Nimeshaanza kuishi kama mstaafu, japo nipo kazini..!
Nimewekeza mifuko ya uwekezaji na sitarajii kufanya biashara za mtaani...
Niliajiriwa nikiwa nina miaka 23 na nitastaafu nikiwa na miaka 40.
Miaka 17 inatosha kuwa chini ya mtu, nitaenda mtaani sasa.

Hii ndio plan yangu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kuna jamaa tuko nae ofisi Moja yy anasema akifikisha 15 years kwenye anakopa ⅓ ya mshahara wake,asepe Ili aendeleze biashara zake Ili asistaafu akiwa Mzee kazini.
Niliajiriwa nikiwa nina miaka 23 na nitastaafu nikiwa nina miaka 40.
Hii ndio plan yangu.
Ila nimeifanya siri sanaa, SIKU YA KUONDOKA SITOMWAMBIA YEYOTEE.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 

We jamaa umenivunja mbavu zangu eti pesa ziliisha salama...hahaha
 
We mjinga nini unataka mtu alipwe pesa inayokaribia mshahara Ili sisi wananchi tuhenyeke yeye awe anapata hela kirahisi tu boya wewe unafikiri hizo hela wanatoa ccm au raia Hali ya chini ndio Kodi zinapelekwa Kwa hao wazee
 
At some point, around miaka 45 amua kuhusu hatima yako. Biashara sio ya kila mtu, kuna namna nyingi za kuwekeza zinazoweza kuja kukusaidia kuendesha maisha bila kufanya biashara
Kwa kweli. Biashara ni kama fani nyingine tu. Huyu anajua yule hajui, maisha yanaenda. Shida ni pale kutaka kila mwenye pesa afanye biashara. Mi huwa ninawaza, hivi fixed account inalipa ili kula faida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…