Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Wengi wao maisha yao yote walikuwa wanategemea mishahara.

wanapostaafu wakiwa kwenye 50s au 60s inabidi waanze kujitafuta upya kwa mafao wanayopewa.

Hapo kichwa huwa kinawaka moto wafanye biashara ipi, huwa wana utofauti mdogo sana na wanachuo wanaoingia mtaani kwa mara ya kwanza kuanza biashara, walichotofautiana ni mitaji tu lakini uzoefu hakuna.

Mzee anatia mtaji wote zaidi ya asilimia 80 ya mafai yake jana uzoefu anadhani biashara ni mtaji tu, wala hazijui changamoto, risks, n.k.

Mzee anaona anunue bajaji / bodaboda bila kuzijua stress za vijana walivyo wasumbufu, Mzee anafungua duka anaweka mtaji mrefu bila kujua ushindani ulivyo, Mzee anafungua biashara bila kujali location, wengine wanapigwa na watoto wa mjini, n.k.

Mafao yote yamedumbukizwa kwenye biashara ambazo hawana uzoefu nazo, stress zinaanza kuziona changamoto za wafanyakazi wezi, hawajakaa sawa taskforce ya Tra wanachomoa kodi zao kwenye account za benki, ushindani umepamba moto sivyo walivyodhani, n.k. stress zinakuwa mara 10 zaidi
Stress huanzia moja kwa moja kwenye kikokotoo kisicho rafiki. Kwa hutwo tuela twa mboga tu unaanzaje kututumia kufungulia biashara? Lahaula lakwata!
 
Kabisa, vibaya sana.....

Nafsi yangu ilijisikia kudhalilika sana, yani napiga simu kusalimia inapokelewa eeeh unasemaje😹, dah nilikaa kando almost a year, baada ya kuisha ndo tukaanza kuwasiliana vizuri haloo haujambo mwanangu usiwe unakaa kimya hivyo

Mi ndo maana huwa sijipi umuhimu kwa mtu jamani, mama, ndugu, mme sijipi umuhimu kabisa.....labda nitakomaa kujipa kwa watoto ila kwingine hapana.

Sitaki kudhalilika kwa namna yoyote ile. Mtu akiona mimi nafata chochote kwake basi nakua wa kwanza kumkimbia kabisa.
Mbona alikua anakujibu vizuri tuu🤣🤣, wewe mbona unatuuliza tupo wapi?
 
Kuna mwalimu jiran na home yeye kafuta Coster ya biashara aiseee gari ilileta ugomvi mkubwa kwa watoto na gari ilianza kutafuna pesa baada ya kuingiza pesa saiz hana kitu amebaki na ugonjwa wa presha na kuota ndoto ngumu usiku.
 
kinachowaponza watumishi wakianza biashara wakiwa kazini,ni kupata hela kila mwezi. hii inamfanya akipata changamoto kidogo kwenye kabiashara kake alikokafungua anatukana na anaifunga kwasababu anajua tarehe ikifika anaenda kukinga ananunua mahitaji ya nyumbani.akishtuka bado miaka mi3 astafu na bado ahajipanga kwa lolote.

hii ni kwasababu watanzania wepesi kulizika hasa akiwa na kasent mfukoni.
mtumishi ukiwa kazini ukifungua biashara hakikisha unapambana na changamoto yoyote inayokuja mbele yako na sio kuifunga na kukimbia changamoto. maana ukiikimbia changamoto hutoweza kujifunza biashara wala kufanikiwa. kama umekimbia changamoto ukiwa kazini hata ukipata hayo mafao changamoto zile ulizozikwepa zitakusubili palepale. na hapa ndipo wanapofeli.
 
Mmh hapana nliona mambo ni mchanganyiko asee nikimpigia sijui alikua anahisi nataka hela zake, anapokea hasemi halooo akipokea "eeh unasemaje" nikaona hapana.....

Mi mbona sitoleagi mate mali ya mtu yoyote nkaamua kukaa kimya kwanza.
🤣🤣🤣maza wetu ni nomaaa alikua anaona km unampigia kelele 🤣🤣🤣
 
Daaah me hii naona asilimia kubwa ya wastafu inawakuta hii,mzee alistafu nakumbuka kila nikimuuliza kapewa kiasi gani anasema kidogo tu,kuna siku nilikuwa namrekebishia smart phone yake ile kupita pita kwenye msg nakuta nakutana na salio la account yake sio chini 100mln nilistuka ila nikakausha tu.juzi kati alikuwa anafanya rekebisha nyumba yake ya biashara naona kaenda kukopa bank ili wawe wanamkata kwenye accont yake ya nssf nikajuliuliza ina maana zile milioni 100 zimeyeyuka..siku uliza kwa vile pesa ni zakee ...hawakawihii kusema unataka kumuua
 
Kuna mwalimu jiran na home yeye kafuta Coster ya biashara aiseee gari ilileta ugomvi mkubwa kwa watoto na gari ilianza kutafuna pesa baada ya kuingiza pesa saiz hana kitu amebaki na ugonjwa wa presha na kuota ndoto ngumu usiku.
Inasikitisha sana. Kuna mmoja jirani yetu ye alistaafu udereva wa malori. Akanunua fuso tandamu hata mimi nilimsapoti sababu najua hajatoka kwenye career yake.
Gari ilipiga tripu mbili tu chali ye mwenyewe majeruhi.
Likaanza kutafuna pesa ya mafao mpaka likakaa sawa. Akampa dereva mana akajihisi yeye age go.
Dere tiripu moja tu tandahimba limeacha njia limeingia maporomokoni limetokq skrepa limeuzwa chuma chakavu na yeye magonjwa nyemelezi yakamuandama mpaka avyopumzika milele.
 
Nimeshaanza kuishi kama mstaafu, japo nipo kazini..!
Nimewekeza mifuko ya uwekezaji na sitarajii kufanya biashara za mtaani...
Niliajiriwa nikiwa nina miaka 23 na nitastaafu nikiwa na miaka 40.
Miaka 17 inatosha kuwa chini ya mtu, nitaenda mtaani sasa.

Hii ndio plan yangu.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kuna jamaa tuko nae ofisi Moja yy anasema akifikisha 15 years kwenye anakopa ⅓ ya mshahara wake,asepe Ili aendeleze biashara zake Ili asistaafu akiwa Mzee kazini.
Niliajiriwa nikiwa nina miaka 23 na nitastaafu nikiwa nina miaka 40.
Hii ndio plan yangu.
Ila nimeifanya siri sanaa, SIKU YA KUONDOKA SITOMWAMBIA YEYOTEE.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Wazee kabla hawajapata mafao wanakuaga na mipango mizuri sana (sometimes na sisi wengine pia kabla ya kushika hela mipango kabambe imenyoooka kama rula ngoja hela ije mkononi sasa sijui ibilisi anatokeaga wapi)

Shangazi yangu: mipango ilikua anunue mashine ya kusaga tena enzi hizo daaah angekua don, baada ya kupata mafao ikawa ni kupika wali wa rangi tu leo wa kijani kesho mwekundu hatimae pesa zikaisha salama.

Bi mdashi: kwakua ametusomesha kwa kufuga tukaona ni vema aendelee na kazi yake, plan afuge kitimoto, kuku wa kutosha chakula cha mifugo kijae hapo, aishi bila mawazo kabisa....
Kilichotokea daaaah.....niseme tu nae kwakweli pesa ziliisha salama.

We jamaa umenivunja mbavu zangu eti pesa ziliisha salama...hahaha
 
CCM hoyee! Huu ujinga uko Tanzania tu ambako kila mwananchi analazimika kuwa mfanyabiashara. Nchi nyingine ukistaafu unapata pension ya kila mwezi ambayo inakaribiana na mshahara uliokuwa unapata. Yaani ukiwa mfanyakazi hutahangaika tena kujazia pato lako na biashara. Wastaafu wengi unakuta wanatumia muda wao kusafiri duniani na kula raha wakati sisi ndiyo wanaanza kujitafuta kwenye biashara. Mkiambia CCM ni janga mnaleta ushabiki wa kijinga kabisa. Wacha wale walichopanda kwani wengi ni husaidia wizi wa kura. Japo sisemi kuwa chama kingine kikiingia hali itakuwa nzuri ghafla lakini ushindani wa vyama kwenye kutawala ndiyo huleta mabadiliko.
We mjinga nini unataka mtu alipwe pesa inayokaribia mshahara Ili sisi wananchi tuhenyeke yeye awe anapata hela kirahisi tu boya wewe unafikiri hizo hela wanatoa ccm au raia Hali ya chini ndio Kodi zinapelekwa Kwa hao wazee
 
At some point, around miaka 45 amua kuhusu hatima yako. Biashara sio ya kila mtu, kuna namna nyingi za kuwekeza zinazoweza kuja kukusaidia kuendesha maisha bila kufanya biashara
Kwa kweli. Biashara ni kama fani nyingine tu. Huyu anajua yule hajui, maisha yanaenda. Shida ni pale kutaka kila mwenye pesa afanye biashara. Mi huwa ninawaza, hivi fixed account inalipa ili kula faida?
 
Back
Top Bottom