Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Mkong'oto wanaotembezewa wastaafu wanaotumia mafao kuanzisha biashara ni funzo kwamba uzoefu ni muhimu, Biashara zinabuma stress zinawamaliza wazee !

Haha kuna mwalimu mmoja alikuwa anapenda nafasi fulani ndani ya chama cha CCM ambayo aliona inamarupurupu mazuri zaidi ya kazi yake ya uwalimu,wanaccm wenzake wakamshauri kuwa kama anataka nafasi hiyo anatakiwa astafu kwa hiyari ili aweze kukitumikia chama angali kijana.

Mwalimu aliomba kustaafu kwa hiyari na kwa kuwa maombi ya kustaafu yalikuwa na mkono wa chama twawala majibu yake na mafao yake hayakuchelewa kutoka.

Na kwakuwa nafasi aliyokuwa anahitaji ilikuwa siyo ya kupewa bure ilikuwa ni ya kugombea na alikuwa ameaminishwa kuwa atapitishwa bila kupingwa,uchaguzi ulipofika alishangaa kuwa hakuwa peke yake kama alivyoahidiwa kuwa hatakuwa na mpinzani atapitishwa bila kupingwa.

Hivyo ilibidi atumie Sera ya CCM ya mkono mtupu haulambwi na toa kitu upate kitu,Siku ya siku mwalimu kaangukia pua,mafao yake yamepigwa na wapambe waliomwaminisha kuwa watampitisha bila kupingwa mpaka sasa hivi mwalimu yuko juu ya mawe kama gari iliyokosa mataili na wenye kumpitisha bila kupingwa nao hawaonekani tena.
Kuna mlezi wangu nae anastaafu mwaka huu sasa ana kanafasi nafasi huko kazini kwake, mwaka huu mwanzoni nilipita kumsalimia nikaambiwa hizo habari za kutaka kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kutumia sehemu ya mafao yake, wanae wapambe na mkewe wote wamesimamisha vichwa nikaamini kweli watz tuna akili finyu sasa hao wapambe bora wanatafuta kula sasa hao watoto na mke wameshindwa kweli kumshauri, nikampa maoni yangu na kumtahadharisha juu ya hizo siasa akaitikia km kanigwa mfupa, nasubiri nione itakuwaje, kabla hajastaafu ana mradi mzuri tu hakosi mil 2-3 faida kwa mwezi ni sehemu ndogo tu inahitaji kuuongeza nguvu na atakuwa mbali hicho kipato huenda kikazidi mara mbili au tatu kabisa, ila ndo kupenda sifaaaa

Halafu bahati mbaya kabisa sehemu anayotaka kuingia mshindani wake ni kijana na yuko vizuri anakubalika ni waziri na kazipurula za kutosha, wajumbe/wapambe sio watu wazuri
 
Inasikitisha sana. Kuna mmoja jirani yetu ye alistaafu udereva wa malori. Akanunua fuso tandamu hata mimi nilimsapoti sababu najua hajatoka kwenye career yake.
Gari ilipiga tripu mbili tu chali ye mwenyewe majeruhi.
Likaanza kutafuna pesa ya mafao mpaka likakaa sawa. Akampa dereva mana akajihisi yeye age go.
Dere tiripu moja tu tandahimba limeacha njia limeingia maporomokoni limetokq skrepa limeuzwa chuma chakavu na yeye magonjwa nyemelezi yakamuandama mpaka avyopumzika milele.
Kingine madereva wanajikutaga wanayajua sana magari. Wengi huishia kununua magari mabovu wakijiaminisha watayamudu. Kukuta dereva ana gari ya maana ni kazi sana.
 
Inasikitisha

Mimi Mzee wangu alivyostaaf , bi mkubwa alimpa plan Safi Kwa wakati huo eneo alipokuwa amejenga maji yalikuwa ya shida akamshauri wajenge kisima halafu wasambazie watu maji, 2 watafute banda la bei rahisi wanunue wakarabati waweke wapangaji, na tatu wajenge pale hom frem hata mbili Kwa ajili ya biashara ya duka na nyingine wapangishe na mzigo bado ungebakia .

Mzee aligoma akampa bi mkubwa mil 5 tu katika mzigo aliopata, bi mkubwa hakuchoka akatafuta dalali amtafutie banda uswazi, likapatikana Kwa mil 7, akarudi Kwa Mzee , bi mkubwa akawa Yuko tayari kutoa pesa Yake Mzee amalizie mbili banda walichukue Mzee akagoma, mpaka watoto kuingilia akakubali kutoa 4 mil na bi mkubwa akaweka Yake 3 wakalizuia.

Mil 2 iliyobakia bi mkubwa akaanza ujenzi pale nyumbani wa frem zake za biashara, akasimamisha frem 2 aliongezea pesa vikoba, akaja akafungua duka la mahitaji ya nyumbani na grocery ya vinywaji...

Turudi Kwa Mzee yeye akaenda kukodi eneo la mtu akalifanyia ukarabati wa kutosha akafungua bar, na mini supermarket Kwa mbele biashara ilifilisika yote pesa ikakata mwenye eneo akamtimua.

Wakati huo bi mkubwa ana wasiwasi anafanya biashara zake bila ghasia Mzee akakusanya Vitu vilivyobakia katika biashara zake akazirudisha nyumbani kwenye goli la bi mkubwa tukawa tunaishi tunategemea biashara za nyumbani na lile pagale hapo limekarabatiwa pesa mzee mkali Nazo Kodi anazuia yeye wakati mwanzo hakutaka...

Swala la kisima bi mkubwa alikuwa anasikitika Sana mpaka Leo hi ...,.

Wastaafu wengi hawachangi Karata zao vizuri na wakishapata Hela ni mtihani Sana...
 
Kwa kweli. Biashara ni kama fani nyingine tu. Huyu anajua yule hajui, maisha yanaenda. Shida ni pale kutaka kila mwenye pesa afanye biashara. Mi huwa ninawaza, hivi fixed account inalipa ili kula faida?
Fixed inalipa ila sio kubwa sana kati ya asilimia 5 mpaka 9 kutegemea na bank, kiwango na muda unaoweka fixed term.

Ila pia kuna bond za serikali au mifuko ya uwekezaji kama UTT. Bond za serikali ni option nzuri sana. Kwa 50m unaweza kupata almost 8mil kwa mwaka kama 650,000 kwa mwezi
 
We mjinga nini unataka mtu alipwe pesa inayokaribia mshahara Ili sisi wananchi tuhenyeke yeye awe anapata hela kirahisi tu boya wewe unafikiri hizo hela wanatoa ccm au raia Hali ya chini ndio Kodi zinapelekwa Kwa hao wazee
Upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Huko wanakolipwa mbona wananchi wanaishi maishi mazuri tu. Hujui serikali ya sasa inatumia fedha nyingi kwa mambo ya kifahari na nyingine zinapotea kwenye ufisadi? Tatizo lako umesoma shule za kata na mbaya zaidi hujatembea uone nchi nyingine wanavyoishi.
 
Nilivyopanga kula pension yangu ni kwamba. Kabla sijastaafu utumishi niwe na viwanja nijenge nyumba yangu na nyumba za kupangisha. My children wawe wamemaliza college hopefully maana nategemea kuwa na watoto wachache sana wawili wananitosha so far. Nastaafu sina wakusomesha. Pension ni hela ya kula sio kufanya biashara.
 
Kuna mlezi wangu nae anastaafu mwaka huu sasa ana kanafasi nafasi huko kazini kwake, mwaka huu mwanzoni nilipita kumsalimia nikaambiwa hizo habari za kutaka kuingia kwenye ulingo wa siasa kwa kutumia sehemu ya mafao yake, wanae wapambe na mkewe wote wamesimamisha vichwa nikaamini kweli watz tuna akili finyu sasa hao wapambe bora wanatafuta kula sasa hao watoto na mke wameshindwa kweli kumshauri, nikampa maoni yangu na kumtahadharisha juu ya hizo siasa akaitikia km kanigwa mfupa, nasubiri nione itakuwaje, kabla hajastaafu ana mradi mzuri tu hakosi mil 2-3 faida kwa mwezi ni sehemu ndogo tu inahitaji kuuongeza nguvu na atakuwa mbali hicho kipato huenda kikazidi mara mbili au tatu kabisa, ila ndo kupenda sifaaaa

Halafu bahati mbaya kabisa sehemu anayotaka kuingia mshindani wake ni kijana na yuko vizuri anakubalika ni waziri na kazipurula za kutosha, wajumbe/wapambe sio watu wazuri
Naamini ni jimbo moja wapo la mwanza
 
Upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Huko wanakolipwa mbona wananchi wanaishi maishi mazuri tu. Hujui serikali ya sasa inatumia fedha nyingi kwa mambo ya kifahari na nyingine zinapotea kwenye ufisadi? Tatizo lako umesoma shule za kata na mbaya zaidi hujatembea uone nchi nyingine wanavyoishi.
Ulaya unafananisha na Africa ambayo wananchi wake asilimia 80% masikini wanatafuta pesa Kwa jasho na damu yaani ulaya mpaka wanapata na pesa za kutoa misaada Africa inamaana maisha ya raia wao ni mazuri sababu pesa zinazoletwa kama misaada ni Kodi za wananchi wa nchi husika hivi unaakili timamu kweli
 
Nilivyopanga kula pension yangu ni kwamba. Kabla sijastaafu utumishi niwe na viwanja nijenge nyumba yangu na nyumba za kupangisha. My children wawe wamemaliza college hopefully maana nategemea kuwa na watoto wachache sana wawili wananitosha so far. Nastaafu sina wakusomesha. Pension ni hela ya kula sio kufanya biashara.
Kabla ya kuwa na hela kila mtu anakuwa timamu kama wewe
 
Fixed inalipa ila sio kubwa sana kati ya asilimia 5 mpaka 9 kutegemea na bank, kiwango na muda unaoweka fixed term.

Ila pia kuna bond za serikali au mifuko ya uwekezaji kama UTT. Bond za serikali ni option nzuri sana. Kwa 50m unaweza kupata almost 8mil kwa mwaka kama 650,000 kwa mwezi
650.000/- kwa kila Mwezi kwa uwekezaji wa mil 50 si haba. Ni kama unajilipa mshahara. Nadhani wastaafu wanaopata mafao ya mil 90-100 unawafaa sana hii. Kwa sababu pia huwa wanapata ile penshion ya kila miezi 3; maisha yanaenda kuliko kuishi kwa stress
 
Hivi hizi hasira zote juu ya wastasfu za nini? Ni wivu au ujinga wenu? Je mtu hana haki ya kutumia atakavyo pesa itokanayo na jasho lake? Mbona nyie mnaanzisha biashara na zinabuma? Kwani na nyie ni wastasfu.
Mbona na ninyi mkipata hela mnahonga ?Kila mtu ashinde mechi zake .Wastaafu wana haki ya kutumia watakavyo hela zao.Ninyi hamna haki ya kuwapangia nini wafanye kwakiwa sio nyie mliozisotea hizo hela.
 
Back
Top Bottom